Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

O
Asante Bro. Kabombe lakini katika siku tajwa mimi na mke wangu tulikuwa wote nyumbani na gari haikutoka siku nzima

Uongo mbaya kiongozi. Una jichanganya. Wewe ulisema haya mapema baada ya kuulizwa kwenu wapi:

Kwangu mimi ni Unguja,Nyumbani kwao Hussein
Hata bara ninakuja,kuongea ya chamani
Tunapanga yenye tija,vyote ndani ya ilani
Siraaj ng'aza siraati,tuondokwe na ghururi.

Senzighe majibu yangu yanakuhusu:

IMG_20201208_091634_475.jpg

IMG_20201208_091612_299.jpg

Kwa mwendelezo huu Senzighe m-CCM wewe kusoma namba ni halali!

Kama namba mtasoma, kama tusomavyo sisi,
Awamu hii ya neema, labda kwa makasisi,
Kanda yetu ya Musoma, labda pia busisi!

Kwa kipyenga cha Senzige, Tunayeya safarini.
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
Hii ni kweli, rafiki yangu alienda ku-renew leseni akaambiwa akalipe kwanza faini ya kosa la barabarani, kosa limefanyika Dar wakati gari liko Dodoma. Hata hivyo walifuta deni hilo baada ya wiki tatu, lakini kwa kufuatilia man to man
 
Hao jamaa wa usalama barabarani(japo siku hizi ni faini barabarani) wamenifanya nidharau kazi yao, majitu hayajielewi, yanatumia nguvu nyingi akili kidogo.
Ukiona huwaelewi jua ndio umeanza kuwaelewa hivyo.
 
ikikosewa herufi au namba ya gar wakat wa uandukiaji faini inaweza kutokea Hilo tatizo kama lililokukuta, unaweza kushangaa gari yako imeandikiwa makosa ikiwa Arusha na wewe upo mbeya na wala Arusha hujaenda.. hiyo inakua ni makosa au uzembe wa askari alie andika faini

Binafsi ilishanikuta lakin nilipoenda kuwaambia walioniomba radhi wakaniambia kama hivyo nilivyo andika na wakafuta makosa hayo... Hivyo ni makosa ya uandishi Cha msingi uwahi kutoa taarifa
 
O

Uongo mbaya kiongozi. Una jichanganya. Wewe ulisema haya mapema baada ya kuulizwa kwenu wapi:

Kwangu mimi ni Unguja,Nyumbani kwao Hussein
Hata bara ninakuja,kuongea ya chamani
Tunapanga yenye tija,vyote ndani ya ilani
Siraaj ng'aza siraati,tuondokwe na ghururi.

Senzighe majibu yangu yanakuhusu:

View attachment 1644389
View attachment 1644390

Kwa mwendelezo huu Senzighe m-CCM wewe kusoma namba ni halali!

Kama namba mtasoma, kama tusomavyo sisi,
Awamu hii ya neema, labda kwa makasisi,
Kanda yetu ya Musoma, labda pia busisi!

Kwa kipyenga cha Senzige, Tunayeya safarini.
Tanzania nchi moja,popote weka makazi
Tumeungana pamoja,sihoji yangu makazi
Si Tabora si unguja,twaishi tangu vizazi
Ni jamhuri ya mungano,mimi naishi popote.
 
Usiniombee mabaya,na mimi nisome namba
Ni trafiki mbaya,kakaa kabuni namba
Lengo lake ndiyo baya,aonekane ni mwamba
Leo deni limefutwa,ila ilikuwa mbinde.
 
Kweli Tanzania moja, ila kwa hili hapana,
Bara ulisema waja, chamani kusemezana,
Makazi yako si hoja, tabu hii kukinzana,
Toka kanda ya Musoma, una haki ya Nderemo!

IMG_20201208_165955_816.jpg

Linganisha semi zako, uzione zinapwaya
Unguja kumbe si kwako, bali kanda ya wahaya,
Maarufu kanda yako, kwingine twala wa chuya,
Tuache wazanzibari, kujisemea wenyewe!
 
Usiniombee mabaya,na mimi nisome namba
Ni trafiki mbaya,kakaa kabuni namba
Lengo lake ndiyo baya,aonekane ni mwamba
Leo deni limefutwa,ila ilikuwa mbinde.

Kwamba deni limefutwa, naona janja ya nyani,
Kwa kupisha kusakamwa, utuingize mjini,
Haya ya kamba kufungwa, tulihama migombani,
Trafiki kaza sana, hasa kwa mi-SiSi Emu!

Mi-sisi Emu mlidhani, wasoma namba si nyinyi,
Mkadhani upinzani, ni kwao tu wa Malinyi,
Uwahusu vipi kwani, si mnaye ndugu Mwinyi?
Tunayo furaha kubwa, bado kulimia meno!
 
Kwamba deni limefutwa, naona janja ya nyani,
Kwa kupisha kusakamwa, utuingize mjini,
Haya ya kamba kufungwa, tulihama migombani,
Trafiki kazi sana, hasa kwa mi-SiSi Emu!

😀😀😀😀😀

Brazajei una gubu,sisi tumeridhiana
Hussein amehutubu,ya zamani kuachana
Tusitafute sababu,tunaka kupatana
Twafungua ukurasa,mpya kuridhiana.

Sasa nakupa ukweli ,upate kunifahamu
Ninao wake wawili,Zenj na Darisalamu
Huku bara wilki mbili,Mbili kule tasilimu
Nadumisha muungano,wengine nanyi igeni.
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
Kundi za vibaka waliohusika n kuiba kura
 
Kwako ilikuwa Zenji, maneno yako thabiti,
Ukadai si Kimbiji, chamani we mwenyekiti,
Itajakuwa bajaji, ushanasa mtu kati!
Ukijifunza uongo, jifunze na kukumbuka!

Bara ulikuwa waja, kuyajenga ya chamani,
Ya wake unayotaja, wajinga wafumbieni,
Bongo za kujikongoja, twa acha je ya zamani?
Ukijifunza uongo, jifunze na kukumbuka!

Historia kumbuka, Sefu na maridhiano,
Wanaweza kufufuka, mlowatia kibano?
Nyie wa kukurupuka, Siasa si mapigano!
Wa kupongezwa ni Sefu, na Aluta Continua!
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
Kwa sasa TRAFIC ni TRA no 1. katika nchi hii Magari ni chanzo cha mapato makubwa cha wanasiasa!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Tena hao traffic wazidishe dozi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app

Habari hizi zimfikie gwiji wa chama tawala, almaarufu "Senzighe wa Senzighe ."

Lissu kuweza mwelewa, namba tuisome haswa!
Kwamba si bazazi hawa, wangapi wamewauwa?
Muda wote wamelewa, dereva awapa vichwa,
Yeye dereva wa Lori, asikilize la nani?

Hapa chini yalikuwa ya mleta mada kabla ya kibao kugeuka:

IMG_20201209_072837_483.jpg
 
Kundi za vibaka waliohusika n kuiba kura
Habari hizi zimfikie gwiji wa chama tawala, almaarufu "Senzighe wa Senzighe ."

Lissu kuweza mwelewa, namba tuisome haswa!
Kwamba ni bazazi hawa, wangapi wamewauwa?
Muda wote wamelewa, dereva awapa vichwa,
Yeye dereva wa Lori, asikilize la nani?

Hapa chini yalikuwa ya mleta mada kabla ya kibao kugeuka:

View attachment 1645164
Brazaj una ila,uchaguzi ushakwisha
Wewe siyo tila lila,kurejea yaloisha
Lissu huko anakula,anayaponda maisha
Nchi tujenge pamoja,ya namba tusiyakuze

Nawe Mrangi sikia,usizidi kuchongea
Siku wakikupatia,usije kutugongea
Akili zitakwishia,uanze kunyong'onyoea
Nchi tujenge pamoja ya namba tusiyakuze

Sefu yeye kabaini,lazima tushikamane
Ametilia maanani,Nchi kwanza si mengine
Makandokando ya nini,Hatuna kwenda kwingine
Nchi tujenge pamoja ,ya namba tusiyakuze.
 
Back
Top Bottom