TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

Kinachonifurahisha zaidi ni utaratibu wa wizara ya fedha kutoa taarifa kila mwezi kuhusu mgawanyo wa pesa walizokusanya.

Natumaini wataendelea na utaratibu huu katika kipindi chote cha utawala wa Awamu ya Tano.
Hapa inakuwa vyepesi kumbana waziri mwenye dhamana pale mambo yanapo kwenda sivyo na pesa wamepewa
Naona Tanzania mpya inakuja
 
Nchi inakwenda sasa na wakiendelea hivi kila mwezi kutoa maelezo kuwa pesa zimekwenda wapi kweli wananchi wengi tutapenda kulipa kodi,mapato ya tanapa hizo dola zinapelekwaga wapi maana nazo ni nyingi kweli kweli
 
we ni mjing namba moja, ukiangalia deni tunalipa zaidi ya b800 halafu tuendelee kukopa?
Huelewi chochote inavyoonekana..wewe ni mmoja kati ya watu wa kuwahurumia tanzania.. mipango ya standard gauge railway ilikuwepo kabla hata ya Magu kudhaniwa kuwa rais.. kukopa kupo palepale..
Uwe unafuatilia mambo kabla ya kuleta makanyagio hapa
 
Ni wajibu wetu na sisi kuitumikia Tanzania, saizi ntakua nadai risiti kwa kila kitu ntakachokua nanunua niijenge nchi yangu
 
jamaa yangu tunaangushana (tuweke hasira pembeni tujadili ki-great thinkers)

Tumejipinda kukusanya 1.79 tr out of that 842.1 bl tunalipa deni la taifa ambalo mi sijui litaisha lini and then tukope tena?
Huelewi chochote inavyoonekana..wewe ni mmoja kati ya watu wa kuwahurumia tanzania.. mipango ya standard gauge railway ilikuwepo kabla hata ya Magu kudhaniwa kuwa rais.. kukopa kupo palepale..
Uwe unafuatilia mambo kabla ya kuleta makanyagio hapa
 
madeni yakilipwa yote madeni yatashuka hadi bn 700. halafu mbona hatuoni impact ya makusanyo hayo?
 
Haya yanayofanyika ni mabadiliko yenye mwelekeo chanya, lakini bado tunahitaji mabadiliko makubwa katika mfumo wetu mmbovu wa serikali kiutendaji kwa ujumla pamoja na taasisi zake. Kuboresha maslahi ya watumishi ili kuongeza ufanisi na uadilifu katika utumishi, pia kuboresha menejimenti ya Rasilimali watu.
 
Ni TRILLION 1 SIYO TRILLION 1.79 ACHENI PROPAGANDA

Soma Gazeti la Mtanzania hapa chini:
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

SERIKALI imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh trilioni 1 kwa mwezi huu, tofauti na Sh bilioni 850 zilizokuwa zikikusanywa kwa mwezi hapo awali na kuzielekeza fedha hizo katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Servacius Likwelile, wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa Sh bilioni 18.7 kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada, chakula pamoja na ruzuku.

Dk. Likwelile, alisema Mkoa wa Dar es salaam umeongezewa Sh bilioni mbili ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais Magufuli, alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao , wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, huku walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.

“Fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma, ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi ya jamii zimetolewa Sh bilioni 81.13.

“Mamlaka ya Elimu (TEA) imepatiwa shilingi bilioni 23.078, mpango wa maji vijijini Bilioni l7.1, maendeleo ya ujenzi wa barabara zimetolewa shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme vijijini zimetengwa shilingi bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni 2.034, Serikali za mitaa zimepatiwa shilingi bilioni 4.5, na Mahakama imepatiwa shilingi bilioni 12.3,” alisema.
 
madeni yakilipwa yote madeni yatashuka hadi bn 700. halafu mbona hatuoni impact ya makusanyo hayo?
mimi nadhani tukiimalisha taasisi za kifedha za ndani kama NSSF,PSPF,TASAF, n.k. tutakuwa na uwezo wa kukopa ndani kwenye mifuko hii ambapo tutapunguza utegemezi wa kukopa nje.
 
Kinachoshangaza wewe unafahamu ni story lakini huchoki kuzisoma na kutoa comment!

Kwani huna suala lingine la kufanya ili uachane na stories from the same people?
Huyo jamaa ni mpuuzi, watu wa namna hii tusihangaike nao kabisa maana hawana mawazo yoyote chanya. Wanakosoa lakini hawasemi mbadala au uboreshaji, tuwaache tu watatuchelewesha hawa
 
Ukiamua kufikiri kidogo tu utagundua wazi kwamba there's no way mapato yanaweza kufika TZS Trilion 1.79... yaani Trilioni moja na bilion 790 wakati kwa kiasi kikubwa vyanzo vya mapato ni vile vile!! Wengi wanafahamu hata mapato makubwa ya January yalitokana na ukweli kwamba, december inakuwa ni deadline ambayo wenye malimbikizo wote wanatakiwa kulipa madeni yao by December 31. Kila mwaka, mapato ya december yanakuwaga makubwa kuliko mengine.
 
Naamini tutafikia trilioni tatu mwaka huu na hapo hatutahitaji misaada ya manyanyaso
 
Wewe kaa ndani subiri uletewe kiroba cha mchele nyumbani kwako lakini serikali inafanya kwa nafasi yake wewe unayetaka mpaka uletewe vitumbua shauri yako.
ni haki yao waniletee walau mara moja kwa mwaka. Si nalipa kodi? Au nalipa kodi kujifurahisha nakuwafurahisha
 
That
SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.

Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.

Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari. Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli. Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya ishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.

Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18.

Chanzo: Habarileo

That guy alikuwa na guts na kiburi cha kupanda majukwaani na kuwaaminsha Watanzania kwamba amefakiwa kukusanya kodi kwa wastani wa Bil.900 kwa mwezi bila aibu. Leo hii JPM anakusanya mara mbili yake na yuko madarakani robo mwaka. Kwa nini asishitakiwe kwa treason!
 
Serikali ikaweke kambi na TANAPA kule nako kuna pesa nyingi sana zinavuja
 
Seriously="Steph Curry, post: 15393083, member: 114302"]teh teh teh teh Mtu muongo anatakiwa awe na kumbukumbu...

Too bad hata kumbukumbu za kwenye vitabu vya mahesabu zinawashinda..

Tuwaache waendelee kupika makusanyo ila muda haudanganyi... Alafu kitu kingine kinachonishangaza ni makusanyo ya January kutangazwa February 23.. Sasa hatujui hii imekaaje..[/QUOTE]
Seriously sick in you empty head. Just cut your head off, hakikusaidii kitu if you can't reason anything with it.
 
Back
Top Bottom