TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

Naijutia kura yangu kwa wale wa sanii kina lodilofa
Usijute kwa sababu hata kwenye ndoa washenga huwa hawakosekani!

Hao walikuwa ni washenga wa kunogesha na kusindikiza wanandoa!

Kumbuka washenga huwa na maneno mengi!
 
Teh teh,cant you differenciate propagandas and true stories? these are the same stories from the same people

A grown up like you speaking shit, can't even take a step to verify the story! Can't you go to the beneficieries to dig for the truth? Kama ni umaarufu tayari Magufuli ni maarufu, kama ni kura wala hahutaji kura yako mpaka miaka 5 ijayo!, kuna sababu gani ya cosmetics? Propaganda for what? Sio ukiwa mpinzani eti usiwe na shukurani hata kidogo!
 
Teh teh,cant you differenciate propagandas and true stories? these are the same stories from the same people
Kinachoshangaza wewe unafahamu ni story lakini huchoki kuzisoma na kutoa comment!

Kwani huna suala lingine la kufanya ili uachane na stories from the same people?
 
Romantic Economist wanatuambia Uchumi unakuwa lkn ktk hali ya kawaida upo stagnant.....
Umetumia kipimo gani kinachotambuliwa kimataifa kufahamu kama uchumi wa Tanzania upo stagnant?

Nielimishe!
 
Kama ndivyo ilivyo,nimpomgeze bila UNAFIKI na nahitimisha kwa kusema hatukuwa na viongozi huko nyuma.Ila nafikiri bado kuna maeneo mengi bado hayakusanywi kodi,na tunaweza kupata hadi Trilioni 3 au 4 if we will work in harmony and increase performance,efficience plus doing production here in Tanzania through our "dead factory and Industry" kama tutavifufua.BIG UP Somebody there.
 
Romantic Economist wanatuambia Uchumi unakuwa lkn ktk hali ya kawaida upo stagnant.....

hawa TEA ndio nani na wanafit vp kwenye system za Tamisemi na Wizara ya Elimu? kweli mabadiliko sio kuzungusha mikono, watanzaniia tungejuta!
Kama ulivyokuwa ukifikiri ccm wasingeweza, ulifikiri CDM wangeweza, isipime maji kwa kuyaangalia.
 
Pamoja na yote hayo bado nchi yetu hatuzalishi tunafanya uchuuzi! Afufue viwanda na kuimarisha teknolojia vinginevyo tutaendelea kuwa watumwa wa Wachina na Mataifa ya Ng'ambo
Rais anachofanya kwa sasa ni kuweka mazingira mazuri ili mchakato wa kuanzisha viwanda usitawaliwe na rushwa/ufisadi, ubadhilifu na uzembe.

Huwezi kuanza mchakato wa viwanda wakati watumishi wa taasisi zinazohusika ni wabadhilifu, wala rushwa na wazembe.
 
DSC01113.jpg

SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.

Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.

Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.

Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.

Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.

Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18 .
 
Billion 200 yetu wameipeleka wapi?
teh teh teh teh Mtu muongo anatakiwa awe na kumbukumbu...

Too bad hata kumbukumbu za kwenye vitabu vya mahesabu zinawashinda..

Tuwaache waendelee kupika makusanyo ila muda haudanganyi... Alafu kitu kingine kinachonishangaza ni makusanyo ya January kutangazwa February 23.. Sasa hatujui hii imekaaje..
 
Back
Top Bottom