TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

teh teh teh teh Mtu muongo anatakiwa awe na kumbukumbu...

Too bad hata kumbukumbu za kwenye vitabu vya mahesabu zinawashinda..

Tuwaache waendelee kupika makusanyo ila muda haudanganyi... Alafu kitu kingine kinachonishangaza ni makusanyo ya January kutangazwa February 23.. Sasa hatujui hii imekaaje..
January mbona yalitangazwa?? Kama sikosei january ilipatikana around 1.06 trilion
 
Inatia moyo sana... hakuna wa kupuuza hii juhudi ya Rais Magufuli na serikali yake.... Ila azidi kutumbua majipu, hasa Makanpuni ya Simu na MIKATABA YA GAS NA MAFUTA, pia WANANCHI wakinunua kitu kokote WADAI RISITI... sijaona TRA wakihimiza sana hili... Lazima kila mwananchi ADAI RISITI akinunua kitu, hasa bidhaa ktk maduka...kwa mwezi tutafikia 4 trillions by Sept 2016... akifanya serious move ktk hizi sector mbili tu, am sure SERIKALI ITAKUSANAYA Tshs 4 trillions hadi Sept...2016

TRA, waanzishe kipindi maalum cha WANANCHI KUDAI risiti akinunua bidhaa dukani... kiwe ktk TVs kama adverts ya secs kadhaa kila siku...
 
Tuliambiwa November 1.4 Trilioni
December 1.6 Trillioni
January 1 Trillion

Leo wanatwambia 1.7 Trillion, mbona basi Figure hazitally?

Je Huyo ng'ombe mnayemkamua mnampa majani? au mnaenjoy kukamua tu.

Sera ya Serikali inabidi iwe kuwakuza wajasiriamali na siyo kuwakamua tu
Kwani haya makusanyo yanatoka kwa wajasiriamali peke yao.. ni makusanyo nchi nzima.. matumizi ya hizo pesa yameainishwa hapo pia. Sijui ni maboresho gani unayotaka kuzungumzia.. ni vizuri ukaja na maboresho ya matumizi..
 
Tafadhari tunapenda kujua bil.200 zimekwenda wapi? Kazi ya kupongeza sio ya opposition by the way tunapongeza nini hapo? bado upotevu wa mapato ni mkubwa na wigo wa kodo ni mdogo mno,kwa mapato hayo standard gauge rail tutajenga kweli? Barabara za kilomita 2000 zitamalizika lini kama tunapeleka bilioni 58? CCM timizeni wajibu wenu tafadhari sijaona cha kupongeza hapo
Standard rail gauge itajengwa kwa pesa ya mkopo.. haijengwi kwa makusanyo ya kodi
 
SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.

Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.

Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari. Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli. Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya ishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.

Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18.


Chanzo: Habarileo
Lakini jana ilikua 1. 079 imekuaje leo hiwe 1. 79?
 
Yeyote anaye jutia maamuzi yake kutoa kura kwa wanao itwa malofa ni zaidi ya lofa basi.
Unategemea CCM au Magufuli angefanya anayo yafanya leo kama Watanzania malofa wasinge amua kuwatia kashikashi na kuchagua mabadiliko??
Kumbuka "Mgema akisifiwa sana tembo hulitia maji. Kabla hamjaja hapa kulaumu (pengine anaye fanya hivyo siyo lofa halisi)"

Kura yangu lofa itaendelea kuwa ya malofa kwa sababu najua thamani ya kura yangu. Kubweteka huku naweza kukufananisha na rubani au dereva au nahodha kwamba kama chombo chake bado kipya na yupo safarini hana haja ya kuangalia mifumo mingine iwe ya kiusalama, uongozaji nk kisa kasi imekolea hakuna haja ya kuangalia unako kwenda au uliko toka maadamu chombo chako cha usafiri ni kipya, huna wasi wasi wowote, chombo kipo kwenye kasi inayo ridhisha hivyo mambo yatajipa mwanzo mwisho na utafika salama.
Ukiwa na mawazo hayo hutafika achilia mbali kufika salama!

Kura yangu itaendelea kuwa kwa wana mabadiliko iwe ni kwa Rais au Wabunge ili heshima iendelee kuwepo. Ukimpa nguvu inayo zidi atalewa sifa na atarudia yale yale ya mlikokuwa. Binafsi sipingi anacho kifanya na nitamsifu akifanya hivyo na zaidi ya hapo mwanzo mwisho. Nitafanya tathimini kila mwaka na tathimini kuu itafanyika baada ya miaka mitano yaani mwezi June 2019.

Jana kuna mzee mmoja alisema hii ni awamu ya pili, amefuta awamu zilizo tangulia ama zilizo fuata baada ya ile ya kwanza..... teh.... the
 
Hata mimi nashangaa, Juzi JPM akiongea na Wazee wa DSM alisema January wamekusanya Trillion 1 , Leo hii huyo mtoa taarifa wa TRA anasema walikusanya Trillion 1.7
Naona kama hizi takwimu hazijanyooka
Na kimsingi hata watetezi hapa JF nao wanafahamu fika kwamba takwimu zinazotolewa ni full mkanganyiko.
 
Kinachofurahisha fedha nyingi inaenda kwenye shughuli za maendeleo.

Viva Magufuli uishi maisha marefu.
Umekosea....mimi naona fedha nyingi karibia nusu ya makusanyo inapelekwa kulipa madeni, check vizuri.

Sasa effect za tawala zilizopita tunazipata kizazi kwa kizazi..kizazi cha pili na cha tatu cha........

Naunga mkono juhudi za Magufuli, maana deni lishatuletea utumwa, hatuko huru kabisa hizo zaidi ya bilioni 800 zingefanya mambo mengi
 
Lakini jana ilikua 1. 079 imekuaje leo hiwe 1. 79?
Shiiiii... ongea pole pole wewe... wakikusikia watakupa namba ya simu upige wizarani; shauri yako!!! Halafu kwa makusudi watakupa namba ya simu ya mezani!!
 
January mbona yalitangazwa?? Kama sikosei january ilipatikana around 1.06 trilion
Ndo mana yake hata jana yule katibu alitangaza trillion moja na billion sabini na tisa leo wanatuambia trillion1 na billion mia saba tisini, kuna walakini kwenye hii taarifa hawatoi taarifa sahihi.
 
Sababu Watanzania wengi wanafurahia namba kuliko maelezo wacha wawafurahishe
 
Kinachonifurahisha zaidi ni utaratibu wa wizara ya fedha kutoa taarifa kila mwezi kuhusu mgawanyo wa pesa walizokusanya.

Natumaini wataendelea na utaratibu huu katika kipindi chote cha utawala wa Awamu ya Tano.
Nimekuelewa vizuri. TRA imeassume role za wizara zote na cost centre zote nchini. Propoganda tu
 
sasa nakubaliana na hojakuwa kodiilikuwa inakusanyiwa mifukoni mwa watu...
 
Haya ni mabadiliko ya kweli!

We can do it!

Majipu yanaendelea kukamuliwa! It’s a sweet pain but it pays to open up the boils.

As a nation, we are going in the right direction!
Kweli kabisa ikiwa pamoja na ukweli na uwazi. Kila kitu kiko wazi!
 
Back
Top Bottom