TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

Huyo Prof. PLO alisema nini kinachohusiana na mada hii.
Nilisema post yako ya mwanzo inanikumbusha speeches zake.. sijasema popote km inahusiana na hii mada..ulizungumzia abt behaviour of "romantic economists with their figure show that economy is growing bt in actual sense is stagnating."

PLO huwa ni challenger. Na huwa anatoa inspirational speech.mojawapo ya speech alizowahi kutoa pale Nnkrumah, aliwa chalange wachumi na report zao za ukuaji wa uchumi usio endana na hali halisi ya maisha.
Nadhani umenielewa sasa
 
Tunaelekea katika mabadiliko ya kweli. Labda vidudu mtu vitukwamishe.
 
jamaa yangu tunaangushana (tuweke hasira pembeni tujadili ki-great thinkers)

Tumejipinda kukusanya 1.79 tr out of that 842.1 bl tunalipa deni la taifa ambalo mi sijui litaisha lini and then tukope tena?
Kwahio wewe ulitaka tusilipe au
 
Kma ni kweli wapongezwe lkn bado khari kwa wana nchi ni mbaya kweli
 
Haya yanayofanyika ni mabadiliko yenye mwelekeo chanya, lakini bado tunahitaji mabadiliko makubwa katika mfumo wetu mmbovu wa serikali kiutendaji kwa ujumla pamoja na taasisi zake. Kuboresha maslahi ya watumishi ili kuongeza ufanisi na uadilifu katika utumishi, pia kuboresha menejimenti ya Rasilimali watu.
Bado nimapema sana
kwanza tushukuru hata kwa hili
tuendako nikuzuri zaidi
 
Sasa hili gazeti la Mtanzania ndio limetuacha njia panda, limeandika zaidi ya bilioni moja, sasa hapo sio exact figure. Hatuelewi ni zaidi mpaka wapi.
Umesoma vizuri
sio bilioni moja
zaidi ya tirioni moja
ina maana si chini ya tirioni moja wala juu ya tirioni moja na bilioni999
 
Kwa mujibu wa Azam tv news .....Likwelile aliongelea makusanyo kuwa ni Trln 1.079 na na sio hiyo ya kutoka habari leo ua Trln 1.7
 
SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.

Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.

Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari. Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli. Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya ishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.

Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18.


Chanzo: Habarileo
Hiki ndicho kinachotakiwa
 
maeneo yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.
Badala ya kukaa mitandaoni na kuanza kuponda takwimu huu ni wakati muafaka wa kuanza kuzifuatilia hizi fedha..na impact yake.
 
wameunganisha makusanyo ya january na february wanakuja kutudanganya hapa,muda utasema!Tusubiri
 
Bado nimapema sana
kwanza tushukuru hata kwa hili
tuendako nikuzuri zaidi
Nakubaliana na wewe. Watu wawe na subira. Siku mia moja Magufuli hawezi kufanya miujiza wa kuwafikisha watz jwente nchi ya asali na maziwa ukiangalia hali aliyoikuta hazina. Kubana mafisadi na kuongezeka mapato ni dalili za wazi kwamba tutafika huko siku zijazo.
 
It is unnecessary accronmy to argue in someone's money expenditures. Surely the effects of these huge amount is too good to be a cetizenry asset. Time is need for visible impact. Jaman haya mahela yangekuwa basi hata na side effect kwenye household economy na hilo ndo muhimu kuliko hizi figures
 
Back
Top Bottom