TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

TRA yakusanya kwa mwezi trilioni 1.7

Tuliambiwa November 1.4 Trilioni
December 1.6 Trillioni
January 1 Trillion

Leo wanatwambia 1.7 Trillion, mbona basi Figure hazitally?

Je Huyo ng'ombe mnayemkamua mnampa majani? au mnaenjoy kukamua tu.

Sera ya Serikali inabidi iwe kuwakuza wajasiriamali na siyo kuwakamua tu
Kuna mapropagandist wapo tu ili serikali ipewe sifa
 
Tafadhari tunapenda kujua bil.200 zimekwenda wapi? Kazi ya kupongeza sio ya opposition by the way tunapongeza nini hapo? bado upotevu wa mapato ni mkubwa na wigo wa kodo ni mdogo mno,kwa mapato hayo standard gauge rail tutajenga kweli? Barabara za kilomita 2000 zitamalizika lini kama tunapeleka bilioni 58? CCM timizeni wajibu wenu tafadhari sijaona cha kupongeza hapo
 
Kinachonifurahisha zaidi ni utaratibu wa wizara ya fedha kutoa taarifa kila mwezi kuhusu mgawanyo wa pesa walizokusanya.

Natumaini wataendelea na utaratibu huu katika kipindi chote cha utawala wa Awamu ya Tano.
Kweli wanafurahisha sana.
Sasa kwenye huo mgawanyo wa pesa umeshajaribu kutoa ukaona imebaki kiasi gani from hiyo 1.7 na mkatuambia inayobaki mnafanyia nini au hiyo hatutakiwi kujua?
 
Wewe kaa ndani subiri uletewe kiroba cha mchele nyumbani kwako lakini serikali inafanya kwa nafasi yake wewe unayetaka mpaka uletewe vitumbua shauri yako.
Mwambie kazi ya serikali si kuweka fedha mifukoni mwa watu. Kazi ya serikali ni kuimarisha huduma kama barabara, elimu, afya, na kuhakikisha ulinzi wa nchi upo imara. Wewe unatakiwa kufanya kazi
 
" Serikali isiyokusanya kodi ni lege lege"- Nyerere

Naamini Nyerere is happy huko aliko
 
Billion 200 yetu wameipeleka wapi?
Hata hapa kwenye hii 1.7.. angalia matumizi yaliyoyasema then inayobaki mbona hawasemi na kama ipo kwenye reserve wawe wanatupa balance bd&bf kama wanavyotupa matumizi
 
Kama ni propaganda waambie unaowaunga mkono ambao wana access na hzo data watuambie kuwa ni uongo

Hapo umesema vizuri. Hao viongozi wa UKAWA wana uwezo wa kuchunguza ukweli wa hizo hela na ndio majukumu yao ili kama serukali inasema uongo waweze kujioatia point.
Hata waandishi wa habari pia wanauwezo huo sana.
 
Haya ndiyo mabadiliko tuliyokuwa tunayataka.

Well done Dr.JPM

Endelea na kuyatumbua ya sehemu za siri sasa.
 
Vipi unakaa ndan kulalamika au unatoka nje kutafuta

Jibu zuri.
Ndio maana watu wanshindwa kwenye biashara zao, kabla biashara haija kaa sawa sawa ule mwezi wa kwanza tu akiona kauza vizuri anataka kuleta matumizi makubwa nyumbani. Na ndio hapa sasa serikali imeanza kukusanya kwa ajili ya masuala muhimu watu wanaulizia juu ya matumbo yao.
 
Kinachonifurahisha zaidi ni utaratibu wa wizara ya fedha kutoa taarifa kila mwezi kuhusu mgawanyo wa pesa walizokusanya.

Natumaini wataendelea na utaratibu huu katika kipindi chote cha utawala wa Awamu ya Tano.
Ila huku mtaani hali imekua ngumu. Vitu tulivyonunua 250 kipindi cha mkwere sasa twanunua 400. Ukipiga mahesabu utagundua nn kimefanya huo mkusanyo uongezeke. Ningewapongeza sana endapo bei zingebaki the same huku mtaani alafu mkusanyo ukaongezeka
 
POROJO HIZI NI KWAAJILI YA CCM! HAZITUHUSU KABISA! TUNACHOTAKA NI KUSIKIA LODI INASHUKA!
 
please!
Piga hii namba ya simu ya ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango uwaulize!
+255 22 2111174
E bhana eh! Hadi viwavutie waya wizara?! Au nimpuuze tu huyu mtendaji wa taasisi nyeti kabisa nchini; Kaimu Kamishina wa TRA Alphayo Kidata manake ni yeye ndie aliyetoa takwimu za kwamba December walikusanya 1.4 Trillion lakini leo tena anasema 1.2 Trillion!!!
 
hiyo namlaka ya elimu..TEA...inahusika au inafanyaje kazi ktk mfumo wa elimu hadi ipewe bil23...anaejua please
 
E bhana eh! Hadi viwavutie waya wizara?! Au nimpuuze tu huyu mtendaji wa taasisi nyeti kabisa nchini; Kaimu Kamishina wa TRA Alphayo Kidata manake ni yeye ndie aliyetoa takwimu za kwamba December walikusanya 1.4 Trillion lakini leo tena anasema 1.2 Trillion!!!

Hata mimi nashangaa, Juzi JPM akiongea na Wazee wa DSM alisema January wamekusanya Trillion 1 , Leo hii huyo mtoa taarifa wa TRA anasema walikusanya Trillion 1.7
Naona kama hizi takwimu hazijanyooka
 
Back
Top Bottom