Umelimbikiza madeni nenda kalipe na TRA wanakubali malipo kwa awamu.
Wewe hujui unalosema,nyie ndio amabo hamjui kitu kwa sababu hujawahi fanya biashara na kulipa kodi.na hujui mchango wa biashara za kati kwenye mchango wa pato la serikali. Yaani serikali zinazoendelea dunia ninkwa kuwa na mfumo mzuri wa kodi.serikali haitakiwi kuingia kufanya biashara,inatakiwa kuwezesha watu wafanye biashara ili walipe kodi.
Ni hivi mtu ulifanyiwa tax assesment miaka mingi iliyopita na hao hao maafisa tra na kulipa chao baadaye wanakuja hawa tena wanafanya upya na kusema uli underfile,so unakokotolewa kodi nyingine na ile tofauti unapigwa fine na interest.kwa nini wasianze na hao maofisa wa nyuma waliosema kila kitu kiko cleani. yaani hapa kwa nini warudi miaka ya nyuma ambayo tayari walishaicheki wenyewe. Hii nadhani inawezekana kwa some instances siyo kila assesment.yaani wanaweza pia baadaye wakarudi pia na kusema kiasi hicho kipya nacho kilikuwa wrong.
Tunazungumzia "unpridictabe enveronment" watu wanakuwa waoga kuendelea na biashara kwa sababu TRA wenyewe kwa wenyewe kila ofisa na tafsiri kivyake sheria ya kodi.
Labda tushauri yafuatayo.
1.Kuwe na TIC,kituo cha uwekezaji kwa wafanyabiashara wadowadogo wenye mitaji midogo na ya kati,mathlani mtu anataka kufungua hardware,duka la jumla,phamacy,biashara ya usafirishaji,gereji,shule,Hotel,bar,guesthouse,lodge,uchimbaji wa madini n.k kuwe kuna kitengo mahali flani serikalini (kila wilaya) cha kwenda kuomba ushauri na kusaidiwa kukamilisha vitu mhimu na kupewa elimu muhimu ya maswala ya kodi na vibali mbalimbali na kufafanuliwa kwa sheria mbali mbali kulingana na sekta ambayo biashara husika iko
2.Lile dawati la ushauri la TRA lingekuwa linafikika na wafanyabiashara wa kawaida
3.Kuwe kuna kitengo kingine cha kuhakiki ukokotoaji kodi kabla mtu hajapewa bili yake ya kodi
3.Kuwe na idara huru(Obusman).Ili wafanyabiashara wenye malalamiko wawe wanaenda kupeleka malalamiko ya unfair tax assesment.kiwe huru na kiwezeshwe kufanya kazi.na kiwe nje ya wizara ya fedha.(kiwe kina dhibiti ubabe wa TRA).yale mabalaza (tribunal) yalishashashindwa kazi zamani
4.TRA wawe na kitengo cha kumentor biashara ndogo ili ziweze kukua.Kila oficer anayekusanya kodi,biashara anayokusanya kodi ikifa naye kazi iishe.Ila ikiweza kukua na kuongeza mapato aweze kupata promotion.kwa mfano wakati wana asses performance ya mkoa wa kikodi waangalie pia idadi ya wafanyabiashara wapya waliojisajiri.ikitokea waliojisajiri ni wengi kulikowalifunga biashara basi wapewe bonas.ila biashara zilizofungwa zikiwa nyingi kuliko mpya then wapunguziwe points za performance. so in short inatakiwa biashara zikifungwa kuwe na direct negative impact kwa TRA region ofice.yaani wafike mahali wahusike kulinda biashara kufa.so zile fine na riba wanazokokotoa wazire-flect juu ya uhai wa biashara husika
Sasa hivi TRA wanaonekana miungu watu,na kituo cha uwekezaji (TIC) wanaonekana wajinga tuu.kumbe ndiyo kitengo mhimu na kilipaswa pengine kiwe ndani ya Wizara ya fedha na mipango.Chini ya waziri mmoja.aulizwe biashara kufungwa na upande wa pili aulizwe juu ya mapato toka kwa hizo biashara