Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,419
- 5,021
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema imefanikiwa kukabiliana na uhaba wa mafuta Nchini ambao ungetokea kufuatia vita vya Mashariki ya Kati vilivyopelekea kuadimika kwa bidhaa hiyo muhimu ya Nishati Ulimwenguni koteAkizungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam leo, Jumapili tarehe 05/07/2026,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mussa Mohammed Makame amesema Tanzania haijashuhudia changamoto ya upatikanaji wa mafuta katika kipindi chote tangu kuanza kwa vita hivyo, na hiyo inakuja hata kwa kufanya ulinganifu baina ya Tanzania na mataifa jirani, hatua ambayo imetimiza lengo la kwanza la serikali la kuhakikisha Nchi haipati uhaba wa bidhaa hiyo
Soma:Sigrada Mligo: Wabunge tunalipwa hela ya mafuta kulingana na bei iliyoko sokoni siku hiyo ndio maana wabunge hawajadili kupanda kwa mafuta
Amesema lengo la pili la serikali lilikuwa ni kuhakikisha bei za mafuta zinakuwa himilivu Nchini, ambapo eneo hilo pia limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa bei za mafuta zilizokuwepo Nchini ni za chini ukilinganisha na mataifa mengine ikiwemo mataifa jirani"Pamoja na kutoondosha kodi zote, wenzetu katika Nchi jirani wamepunguza au kufuta baadhi ya kodi katika kipindi hiki, wengine wamepunguza hadi ubora wa mafuta lakini bado bei zao ziko juu kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na sisi" -Makame
Akizungumzia mjadala unaendelea mtandaoni kuhusu upatikanaji wa mafuta na madai ya kupanda kwa bei Nchini, Makame amesema katika kupanga bei Tanzania imekuwa ikichukua wastani wa bei ya Dunia ya mwezi wa nyuma (yaani kama huu mwezi wa Saba, wanachukua wastani wa bei za Dunia za mwezi wa Sita) katika kukokotoa bei ya mwezi husika, hata hivyo amesisitiza kuwa Nchi zote zimekuwa zikitumia bei za Kimataifa moja, hivyo madai ya kwamba bei za mafuta za Tanzania zimepanda maradufu kulinganisha na mataifa mengine hazina uhalisia"Kwahiyo kwenye hili nataka niseme kwamba huu ulinganifu ambao umekuwa ukifanyika hauko sawasawa" -Makame