Top CCM leader secretly funding opposition party

Mkuu mda nao ulikuwa umetutupa mkono na ukumbuke ishara ya serikali kutekeleza maagizo ya bunge ilikuwa imetoweka.Badala ya kutekeleza maagizo ,serikali ikapeleka maigizo ya kesi ya Gire.Sisi wengine kwa kuangalia athari ambazo zingelikumba taifa kwa kuingia gizani tukaona ni afadhali tuinunue hiyo Mitambo ya Dowans ambayo tunayo hapahapa.Lakini wenzetu mkakataa na sisi tukakubali ya wengi wape,rejea thread hiyo ya Dowans na ile aliyoanzisha Mwanakijiji kwa kichwa cha habari''Mwachieni Gire Nunueni Mitambo ya Dowans Yaishe'' .
Mimi ninachokipinga tabia ya watu kukosa uvumilivu ya mawazo yanayotofautiana na ya kwao na kuanza kushutumiana kuwa fulani kanunuliwa.
Mkuu Nsaji,

Nakubaliana na ulichoandika hapo juu; hilo ndilo tatizo la sisi Watanzania. Tunaangalia kila jambo kwa kutumia black and white scenario au angelikuwa Bush anasema you are either with us or with the terrorists. Ni yale yale ya pande mbili za shilingi huku ukiwa una macho yanayofanya kazi au mikono inayoweza kupapasa unaona/unagundua wazi shilingi ina pande zaidi ya mbili.

Mimi nimeshangaa hatred iliyopo kwa mhesh. Zitto kwasababu tu alitetea kununuliwa kwa mitambo ya Dowans. Watu wamesahahu mazuri yote ya Zitto na sasa wanaanza kumtukana eti kanunuliwa.

Kama nilivyoandika kwenye hiyo thread; hata mimi ningeona hiyo mitambo inunuliwe kama mambo yote mengine kuhusu uhalali wa hiyo mitambo yangewekwa wazi na pia bei yake ingelikuwa nafuu. Watu wengi walikataa; tunaojua demokrasia tunasema wengi wape. Matokeo yake miezi sasa inakatika na hakuna kinachoendelea na tunachoona ni hayo hayo matatizo ya kukata umeme.

Mhesh. Zitto amefanya mengi makubwa kuendeleza upinzani labda kuliko kiongozi mwingine yeyote ukiondoa Dr. Slaa. Badala ya kumbeza inabidi kumpa respect yake. Of course sio wakati wote atakubaliana na sisi lakini hiyo sio sababu ya kuanza kumbeza.

Badala ya kuhangaika hapa kutafuta kiongozi gani kanunuliwa, labda tuwe tayari kuvichangia hivi vyama ili viongozi wake wasiwe ombaomba. Lakini kama tunakaa nyuma na kazi zetu ni kulaumu, kweli hao viongozi wakizidiwa kuna baadhi yao watachukua fedha kwa mafisadi.
 
Nakubaliana na mdau mmoja humu kuwa hii ni yale yale maendelezo ya PAPA NA NYANGUMI.. kwa kweli tayari kuna watu wapo maalum kwa ajili ya ya kumtetea Nyangumi na yupo tayari kuhakikisha cuf inaenda chini eti tu kwa sababu Lipumba kamtetea RA lkn ni uongo mtupu,Lipumba hakukumtetea mtu bali alipinga njia alozitumia Nyangumi,.. na Lipumba ndie aleanzisha mada ya ufisadi,halafu ageuke? si kweli.

Hii yote ni Mengi kwa chuki zake binafsi dhidi ya Cuf tuliona mwaka 95 karibu na uchaguzi alivotoa picha za angola na rwanda za machafuko,tukaona 2005 karibu na uchaguzi wakati Mahita alivoonesha kisu na kitambaa kina rangi ya Cuf,ilikuwa kila wakati anatoa kwenye vyombo vya habari vyake, sasa sishangai kwa hili,na mengineo.. na ana watu nyuma yake kwa kujulikana kabisa wako kwa ajili ya kukimaliza Cuf,tunawajua. Nauliza KULIKONI ni la nani?

Uswahiba wa Jusa na RA unajulikana,si vibaya mtu kuwa na rafiki, Je alokuwa mgombea mwenza wa Cuf Nassor khamis ni shemegi yake Karume kuna ubaya? Je Juma duni ni mjomba wa Salmin amur kuna ubaya? kwa upande wa znz kule kuna wengi kama hao tena wengine ni marafiki na wakubwa wa ccm, na wengine wana uhusiano kabisa....

Kufadhiliwa Cuf na RA ni uongo mtupu,hakuna ushahidi wa hilo,tupeni ushahidi,hizo ni hao hao ambao wamepandikizwa na kina Mengi na ccm ili kuiangusha Cuf,yalitokea maneno mengi kama hayo lkn chama bado kipo strong,na CCM wameapa kwamba watafanya kila njia kuimaliza Cuf.. na hasa wakati huu wanaona kwamba Cuf wameanza kubadilisha mifumo na mbinu kwa ajili ya 2010,na kuona kuwa watu waliokuwa wanawatumia kupigwa na chini..

Wapo watu wanatoa misaada kwa Cuf lkn ni watu wana mapenzi ya dhati na Cuf na ni watu safi kabisa,lkn sio kama hao Nyangumi na Papa..
 
Na jengine sioni ni kitu gani wamefadhiliwa Cuf busanda na magogoni... labda atwambie mwandishi..
 
Nakubaliana na mdau mmoja humu kuwa hii ni yale yale maendelezo ya PAPA NA NYANGUMI.. kwa kweli tayari kuna watu wapo maalum kwa ajili ya ya kumtetea Nyangumi na yupo tayari kuhakikisha cuf inaenda chini eti tu kwa sababu Lipumba kamtetea RA lkn ni uongo mtupu,Lipumba hakukumtetea mtu bali alipinga njia alozitumia Nyangumi,.. na Lipumba ndie aleanzisha mada ya ufisadi,halafu ageuke? si kweli.

Hii yote ni Mengi kwa chuki zake binafsi dhidi ya Cuf tuliona mwaka 95 karibu na uchaguzi alivotoa picha za angola na rwanda za machafuko,tukaona 2005 karibu na uchaguzi wakati Mahita alivoonesha kisu na kitambaa kina rangi ya Cuf,ilikuwa kila wakati anatoa kwenye vyombo vya habari vyake, sasa sishangai kwa hili,na mengineo.. na ana watu nyuma yake kwa kujulikana kabisa wako kwa ajili ya kukimaliza Cuf,tunawajua. Nauliza KULIKONI ni la nani?

Uswahiba wa Jusa na RA unajulikana,si vibaya mtu kuwa na rafiki, Je alokuwa mgombea mwenza wa Cuf Nassor khamis ni shemegi yake Karume kuna ubaya? Je Juma duni ni mjomba wa Salmin amur kuna ubaya? kwa upande wa znz kule kuna wengi kama hao tena wengine ni marafiki na wakubwa wa ccm, na wengine wana uhusiano kabisa....

Kufadhiliwa Cuf na RA ni uongo mtupu,hakuna ushahidi wa hilo,tupeni ushahidi,hizo ni hao hao ambao wamepandikizwa na kina Mengi na ccm ili kuiangusha Cuf,yalitokea maneno mengi kama hayo lkn chama bado kipo strong,na CCM wameapa kwamba watafanya kila njia kuimaliza Cuf.. na hasa wakati huu wanaona kwamba Cuf wameanza kubadilisha mifumo na mbinu kwa ajili ya 2010,na kuona kuwa watu waliokuwa wanawatumia kupigwa na chini..

Wapo watu wanatoa misaada kwa Cuf lkn ni watu wana mapenzi ya dhati na Cuf na ni watu safi kabisa,lkn sio kama hao Nyangumi na Papa..

Mkuu Calipso, you sound like an insider! Mbona na wewe unakuja na allegations kama unazozikataa?? Na unakataa kabisa kuwa ni uongo na watoe ushahidi, unatumia maneno kama ya RA anayetaka watu watoe ushahidi kuwa ni mwizi?
 
Mpigafilimbi
hayo mambo mkuu wangu we acha tu.. muhimu watupe ushahidi,tutajua ni kweli,sio maneno matupu,tuliambiwa Cuf inafadhiliwa na waarabu ili kurudisha usultani,mkuu umesahau? na yapo maneno mengi tu yaliwahi kusemwa amabayo ni uongo mtupu,sasa hiyo yote ni ccm tu na watu wake kuipakaza Cuf..
 
Haya yote mimi naona ni hofu ya watawala kuwa sasa wanaanza kugawana ufadhili na hivyo hofu ya wapinzani imeanza kuwaingia. Kama huyu mfadhili anawapa ufadhili kwa nia ya kuwajenga na sisi hatupo tayari kuwasaidia ila kila mara tunachofanya ni kuwahukumu na maneno ya kejeli lakini hata kura hatupigi then hawana njia nyingine ya kujiendesha waacheni wapewe.

Hivi ni wangapi kati yetu tukiombwa michango na hivi vyama tupo tayari kuwasaidia? Ni wangapi tupo tayari kujiunga na nguvu walizoanzisha kubadili sura ya umaskini wa kitanzania? Najua wapo wengi watasema mpaka sasa hao wamefanya nini? Wewe utakayesema hivyo umefanya nini zaidi ya kurusha kashfa ukiwa nyuma ya pazia! Kuendesha chama kunahitaji fedha sasa lets be sincere...tutasema saaaaana lakini kama you/us, middle class na wasomi hatutachukua hatua ama za kushughulika na siasa angalau kwa kupiga kura au kwa kuwa wakweli wa dhamira zetu, kutolaumu tu na badala yake kujiunga basi katika kile chama tunachokiamini na kupeleka haya mawazo yetu katika ngazi halali za vyama vinginevyo hatuna tofauti na wale tunaowalaumu. Ni ufisadi kutegemea nchi ikufanyie mambo mazuri wakati wewe haupo tayari kuitumikia nchi yako...historia itatuhukumu...tulikuwa wapi!
 
Naona tayari watu mmeshaamini hii taarifa ni kweli na kwamba CUF, NCCR na TLP ndio wapokea dau, kitu gani kinawafanya muiondoe CHADEMA?

Haya mambo ya Mengi na RA yanatufanya wengine tujiulize kwanza kabla ya kuamini jambo.

Thisday si wataje majina tu? Mbona articles zao zingine wanataja majina bila wasiwasi mkubwa? Hata kama sio kutaja majina basi watoe ushahidi zaidi.

Hii habari imekaa kama ni mwendelezo ule ule wa vita vya Mapapa na Manyangumi. Kibaya kwenye hii vita yao wanaingiza ndani na watu ambao hawana uhusiano kabisa na hayo mambo yao.

Waya wa umeme unastahili kushtua hiyo akili yako, unaingizwa mkenge kudhani kuna ugomvi kati ya Mengi na Rostam et al kwenye masuala ya biashara, wakati hao jamaa wanajaribu ku turn issue mfikirie ugomvi wao wakiendelea kula nchi.

RA anajaribu kujiingiza katika kila sehemu ili kujihakikishia usalama kutoka kila angle. CCM - Nec - CC na General assembly alishakamata, bado bungeni ndo stratage anayokuja nayo kwa sasa. Awe na wabunge ndani ya CCM na wa upinzani pia watakaolinda maslahi yake. Tayari Lipumba alishamtetea sana kuhusu Richmond/Dowans(Hasa kwenye manunuzi ya mitambo ya Dowans)na hata kwenye issue ya Ufisadi papa.

Mtabaki kusema ugomvi wa Mengi na RA wenzenu wakitafuna nchi. Kwani ni kashfa ipi kubwa iliyompitia pembeni RA? Kwa hili hata mwendawazimu hawezi kudhani kuwa ni ugomvi, labda kwa kibaraka tu ambaye kwa namna moja ama nyingine ananufaika na Ufisadi.

Hawa Jamaa ni kuwawashia moto tu, kitaeleweka mbele kwa mbele hata ikiwa sio kweli, wao wametufanyia mangapi yasiyofaa ndani ya nchi yetu.

Ni Lazima tusimame imara Mwizi hawezi hata siku moja akakiri kuwa ameiba. Tanzania ya leo na Kesho inakutegemea wewe, Fanya Kazi kwa nguvu, ipiganie kwa nguvu, kataa wizi kwa nguvu - kuwa mzalendo.
 
Na jengine sioni ni kitu gani wamefadhiliwa Cuf busanda na magogoni... labda atwambie mwandishi..

CUF waje hapa jamvini watuambie huyu mfanyabiashara mkubwa mwekezaji ndani ya CUF ni nani na anapata faida gani ya uwekezaji ndani ya CUF. Wasipojitokeza we conclude ni Rostam na kwamba CUF imepoteza mwelekeo
 
Bill mkuu..
Kwanza tupewe ushahidi hao waliosema,sio waseme midomo mitupu kwa faida yao,halafu na Cuf ndo wanaweza wakajibu.. Kama ni hivo tuliskia chadema kule busanda wanagawa pesa si mchezo na mpaka waandishi wa habari walichukua kila mtu 560,000,na huku chopa ikifanya kazi mbona watu wamenyamaza kimya? au ni chadema kinachofadhiliwa na RA?
 
Ah! huu ni ugomvi wa Bw. Mengi tu usioisha. Nani asiyefadhiliwa katika dunia ya leo. Tuwe makini jamani. Tusijeingia kwenye vita vya panzi!
HEhehe hizi ni siasa za bongo.hawa wanaoshabikia upinzani waache tuu hawajui what is behind the curtain.hata chadema hivyohivyo.nao wanachota kidogokidogo ngoja wavurugane mchele utamwagwa hadharani.
 
Swala la kiongozi yeyote kumtetea RA iwe katika uwekezaji kwa sababu tuna shida ni makosa makubwa kisiasa. Hakuna mjadala..Zitto alikosea na Lipumba alikosea vile vile haihusiani kabisa na mazuri waliyokwisha yafanya.
Rostam alikwisha litia hasara taifa kwa miradi ambayo hadi hivi tunavyozungumza ina utata mkubwa na siwezi kuamini kiongozi na mbunge anapokuja na hoja ya kutetea ununuzi wa mitambo ambayo muuzaji wake ndiye mshtakiwa kwa kosa linalotokana na mitambo hiyo hiyo.

Huku nchi za magharibi mtu kama Rostam angetemwa na kila kiongozi wala hakuna mtu angetaka kujihusisha na siasa zinazoambatana na mtu huyo kama Rostam. Matatizo ya Umeme yapo, yalikuwepo, na yataendelea kuwepo ikiwa hatuwezi kuweka miundimbinu ya muda mrefu badala yake tunafikiria utatuzi wa muda mfupi ambao contract yake inaweza kuendelea hadi miaka 20 ijayo...ndio kamba wanazotufunga hawa viongozi wetu siku zote swala la muda huchukua karene nzima..

Kama kweli mitambo ile ilikuwa na manufaa kwetu mbona Songas wamekataa kuinunua? tusitake kutetea vitu ambavyo viko wazi kabisa kuwa tunapotoshwa...Zitto na Lipumba hawakutakiwa kabisa kuingilia swala hili la manunuzi ya mitambo ile kwa sababu sii kazi yao, sii serikali yao ipo madarakani wala hawakutakiwa ushauri wao ktk ununuzi ya mitambo ile..

Hawa watu walikutana na utawala wa Tanesco hotelini nje ya kazi walizoajiriwa na serikali jambo ambalo Zitto mwenyewe alimshambulia waziri Karamagi kuhusu mkataba wa madini alioweka akiwa London hotelini..Kisha maamuzi yake akayaweka ktk vyombo vya habari kwa kutumia jina la tume yake kama vile katumwa..Haya huyo Lipumba naye akaitwa mkutanoni hotelini akaja na zake kuunga mkono akisema kwamba hata mitambo mipya pia ipo feki!.. hiyo mitambo gani aliwahi kuiona yaani mtu atengeneze generator ya umeme feki kama vile mkuu huyu hajui sheria zinazoambatana na utengenezaji wa machinery..Hata hilo gari sijawahi kuliona feki likiwa BMW linatengenezwa South Afrika haliwezi kuwa feki maana lina kibali cha BMW kutengenzwa South Afrika.. inakuwa kama vile hafahamu utandawazi!

Kifupi sababu zote zilizojengwa na viongozi wetu hawa kuhusiana na ununuzi wa mitambo ya Dowans haukuwa wa busara kabisa na kibaya zaidi walitaka kulazimisha na hasira mapovu yakiwatoka..Kwa mapenzi gani ya nchi tunapoendelea kuliwa na hawa kina Rostam bado mnawajengea ngome zaidi kujikinga ati kwa sababu tuna shida.. yaleyale ya sababu za wizi na uasherati kuwa shida ndio iliwasukuma kufanya walofanya..

Jamani tumechoka enough is enough!
 
Bill mkuu..
Kwanza tupewe ushahidi hao waliosema,sio waseme midomo mitupu kwa faida yao,halafu na Cuf ndo wanaweza wakajibu.. Kama ni hivo tuliskia chadema kule busanda wanagawa pesa si mchezo na mpaka waandishi wa habari walichukua kila mtu 560,000,na huku chopa ikifanya kazi mbona watu wamenyamaza kimya? au ni chadema kinachofadhiliwa na RA?


Mkuu, msingi wa hoja ya Bill hapo juu ni bandiko hili angalia ushuhuda wa Lwakatare, ametaja uwepo wa 'ushirika' kati ya viongozi wa juu na mfanyabiashara.

Sasa inatakiwa watu wa cuf waje hapa wakanushe madai hayo mkuu!
 
Mkuu, msingi wa hoja ya Bill hapo juu ni bandiko hili angalia ushuhuda wa Lwakatare, ametaja uwepo wa 'ushirika' kati ya viongozi wa juu na mfanyabiashara.

Sasa inatakiwa watu wa cuf waje hapa wakanushe madai hayo mkuu!
Wapi mkuu Mwiba? au ndio kuingia mitini hiko?
 
Cuf ina wafanya biashara wengi wanaokisaidia chama sio RA.. Lwakatare hoja yake ilikuwa ni nyengine,rudia uzuri.. labda nikusaidie tu,awali wafanya biashara walikuwa wakitoa misaada ilikuwa ni siri ya viongozi na wao,lkn hivi sasa wamebadilisha utaratibu,inaekwa wazi hata kwenye vyanzo vyake.. Lwakatare alikuwa anahoji kwanini isiendelee kuwa siri? lkn viongozi wa juu wameamua kuweka wazi hilo.. rudia barua ya Lwakatare lkn isome kwa uangalifu kipengele hicho utaona,sawa mkuu..?
 
Haya yanatokana na maelezo ya Lwakatare (aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CUF upande wa bara). Baadhi ya JF members walishatoa dondoo hapa, kumbukeni maneno ya wakuu Paparazi Muwazi na Philemon.

Rostam amekuwa mfadhili wa baadhi ya vyama vya upinzani hasa CUF, NCCR na TLP. Lengo la RA ni kupigania nafasi yake ktk ufisadi, ili asiumbuliwe na akina Mrema na hawa jamaa wa CUF na NCCR. Pili ni kuvuruga upinzani ili wasiweze kuwa na umoja unaoweza kuitishia CCM ktk chaguzi. Tatu, ni kupata wafuasi watakao msaidia kupambana na Mengi, Mwakyembe nk. Pia anapigania nafasi ya Dowans. Rejeeni maneno ya Mrema, Mbatia na Prof. Lipumba juu ya ufisadi na suala la dowans hasa baada ya uchaguzi wa Tarime,
Kwa kweli wana JF kuna haja ya kuwahimiza watanzania wawazomee viongozi wa TLP,CUF,NCCR na wengine waokula matapishi ya mafisadi.Mimi nilishakuwa na wasiwasi kutokana na kauli zao zinazo kanganya.MUNGU IBARIKI NA KUINUSURU TANZANIA.
 
Halafu jamani nauliza huyu RA ametoa wapi hizi fedha anazotapanya kila mahali,ameamua kujitoa muhanga kuiangamiza Tanzania na watu wake,huyu kweli anaasili ya wanaojitoa mhanga wa Mashariki ya kati.Lakini namhakikishia hatashinda kwa kuwa ni mdhulumaji na anapambana na wanaotetea dhuluma katika jamii ya Tanzania.
 
Come along JF members, to put 2 and 2 together to make four: The party that has one of its top brass frequently putting up in hotels in Dar ni kafu na i .na .ku .fa!!! Sasa kilichobaki, kama mwana JF mmoja alivyoshauri hapo juu ni SLAA, MBOWE na ZITTO kujihadhari na ma********* wanaohonga kutokana na fedha walizokwapua BoT mchana kweupeee tunazoziita ni za EPA.

Chadema does not need the dirty money from EPA. Walalahoi watawachangia wakihamasika kwa ujumbe wa UKOMBOZI.

Hakuna kulala, Mpaka Kieleweke!
 
Last edited:
This person lazima a chague upande yake. a ache mambo za ujinga. I know it is bad swahili but still does anyone know who this is?
 
Back
Top Bottom