Togo: Upinzani waitisha Maandamano kupinga Ucheleweshwaji wa Uchaguzi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,043
1,682
Vyama Vinne vya Upinzani vimeitisha maandamano makubwa kuanzia Aprili 8, 2024 ili kupinga kucheleweshwa kwa Uchaguzi Mkuu uliotarajiwa kufanyika Aprili 20, 2024 huku tarehe mpya ikiwa bado haijawekwa wazi

Vuguvugu la Kisiasa limeongezeka Nchini humo baada ya Bunge kupitisha mabadiliko ya Katiba ambapo Vyama vya Upinzani vimelaani hatua hiyo vikidai inaweza kumruhusu Rais Faure Gnassingbé kusalia madarakani.

Rais Gnassingbé amekuwa madarakani tangu Mwaka 2005, alipomrithi Baba yake ambaye aliongoza Togo kwa Miaka 38.

.............


Four opposition parties and a civil society group in Togo have called for mass protest next week to demonstrate against the delayed parliamentary and regional elections.

Political tensions have heightened following parliament's approval of a contested constitutional reform last week due to replace the presidential system with a parliamentary one.

Opposition parties have rejected the constitutional change, fearing it could let President Faure Gnassingbé stay in power.

President Gnassingbe has been in power since 2005, when he replaced his father who led the West African state for 38 years.

On Wednesday, the presidency announced the postponement of the country’s parliamentary elections, which were due to take place on 20 April.

The presidency did not say the new date for the polls, citing the need for more consultations over the reforms.

Opposition leader and Togo’s first female presidential candidate, Brigitte Kafui Adjamagbo Johnson, has told the BBC that the election delay is a "power grab" and is disappointed by this latest move.

"We’re not going to accept this, and we will fight against this constitution. It shouldn't be approved by the president".

Source: BBC
 
Sasa tukija kwetu utasikia ooo wakaskazini mara watoto wao mbona hawapo mara sijui nikavunjike mguu kwaajili yao ilimradi tu mwishoe viongozi wa upinzani wakikosa sapoti yetu wanakula mlungula wanakubali kunywea, sisi wananchi hatuna msimamo wakufanya maandamano wala kulalamikia kinacho tuumiza hata siku moja TZ hatuwezi.
 
Hyu Faure inaelekea anaishi vyema na wanajeshi wake, mpaka Sasa nashangaa hajapinduliwa!

Namfananisha na yule wa Gabon. Katawala baba kisha mtoto kabla ya kupinduliwa. Natumaini Kuna kitu kitafanyika wakati wa uchaguzi kama Gabon.
 
Africa yetu wananchi washashtuka, Viongozi wanatengeneza mifumo ya kuwanufaisha watu wachache, Hasahasa wao na nafamilia zao, huku maisha ya wananchi yakibakia kuwa magumu

Tunahitaji mabadiliko ndio tiba 🙏
 
Back
Top Bottom