Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Cuf ina wafanya biashara wengi wanaokisaidia chama sio RA.. Lwakatare hoja yake ilikuwa ni nyengine,rudia uzuri.. labda nikusaidie tu,awali wafanya biashara walikuwa wakitoa misaada ilikuwa ni siri ya viongozi na wao,lkn hivi sasa wamebadilisha utaratibu,inaekwa wazi hata kwenye vyanzo vyake.. Lwakatare alikuwa anahoji kwanini isiendelee kuwa siri? lkn viongozi wa juu wameamua kuweka wazi hilo.. rudia barua ya Lwakatare lkn isome kwa uangalifu kipengele hicho utaona,sawa mkuu..?
______________________________
CALLIPSO:
Nadhani hujaielewa kivizuri ile hoja ya Lwakatare hasa katika kifungu husika. Nakinukuu hapa kifungu chenye hiyo hoja -- ambayo nakubali kwanza ukisioma kwa haraka inaonekana ina utata -- yaani inaonyesha maana mbili ingawa maana halisi iko wazi na hasa ukizingatia ile comma baada ya neno 'naye':
"Mhe. Mwenyekiti jana na leo, nilipokuwa nikichangia na kuhoji ndani ya baraza hili kama mjumbe na hasa suala la fedha za mkutano mkuu ambazo hazikupatikana toka kwa mfanyabiashara mmoja tuliyewekeza naye, suala la kutoendelea na utaratibu wa kuifanya SIRI ya viongozi wa juu tu mikataba ya uwekezaji tunayoifanya na baadhi ya wafanyabiashara na hatari iliyopo kwa utaratibu huo, na pia suala la kutoridhishwa na namna Chama kisivyo na utaratibu mzuri wa Kuwaenzi na kuwaheshimu viongozi.....
Maana ninayoipata ni kwamba LW anaibua suala la 'kutoendelea na utaratibu' wa kufanya siri ya viongozi wa juu tu iule mikataba ya uwezekaji inayofanywa na chama na baadhi ya wafanyabiashara -- na hatari ya utaratibu huo. Ni dhahiri hapa WL anataka utaratibu uliopo usiwe siri kwa viongozi wa juu tu wa CUF.
Kuna utata kidogo, lakini haiwezekani, katika hali hii ya farakano baina yake na viongozi wengine wa chama LW akahoji vipi usiri uliokuwapo uondolewe? Bila shaka angeohoji vipi usiri uwe unaendelea? -- yaani kama kiongozi anayepigania uwepo wa uwazi katika shughuli za chama hasa kuhusu mapato na matumizi ya fedha.