Top CCM leader secretly funding opposition party | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Top CCM leader secretly funding opposition party

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Makaayamawe, Jun 18, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Top CCM leader secretly funding opposition party

  THISDAY REPORTER
  Dar es Salaam


  A PROMINENT member of the ruling Chama Cha Mapinduzi’s (CCM) central committee has been secretly bank-rolling a rival opposition party in the country ahead of the upcoming 2010 general elections, it has been revealed.

  Well-placed sources say the heavyweight CCM politician has in fact been one of the opposition party’s main donors for quite some time now.

  Revelations that the senior CCM official is sponsoring the opposition party have caused an internal rift within the political party in question.

  Insiders say some of the national leaders of the opposition party being bank-rolled by the CCM member have now fallen out as a result of disagreements over his secret campaign contributions.

  There have been concerns that the credibility of the opposition party with a strong presence in both mainland Tanzania and Zanzibar could be compromised as a result of its ’’unholy alliance’’ with the top CCM leader.

  ’’The CCM man has actually been holding clandestine meetings with some of the top leaders of the opposition party from both mainland Tanzania and Zanzibar,’’ said an official close to the opposition party.

  He added: ’’The member of the ruling party’s central committee is also ironically involved in fund raising activities for CCM itself.’’

  It is understood that the CCM man secretly donated millions of shillings to the opposition party to finance its election campaigns in the recent Busanda parliamentary by-election in Mwanza and the polls for a House of Representative seat in Zanzibar’s Magogoni Constituency.

  ’’It is believed that this CCM leader is bank-rolling the opposition party to guarantee protection for himself in the unlikely event that the ruling party should lose the general elections,’’ said another source familiar with the matter.

  Apart from bank-rolling the opposition party in question, the ruling party official is also known to have sponsored individual parliamentary candidates from other opposition parties during the 2005 general elections.

  ’’This CCM money man has also been footing the hotel bills in Dar es Salaam for a senior member of the opposition party being personally funded by him,’’ said another source.

  Sources say the CCM official has a ’’close friendship’’ with the leaders of at least three opposition parties as part of his larger strategy to safeguard his interests.

  ’’He has been paying off some well-known opposition leaders to ensure his vast interests are protected at any costs,’’ said an official close to one of the opposition parties that has been benefiting from secret campaign contributions from the CCM man.

  Political sources say the CCM party itself is not officially aware that one of the members of the powerful central committee was financially supporting rival opposition parties.

  ’’The secret campaign contributions made by this CCM central committee member to opposition parties are intended to safeguard his own personal interests rather than looking out for the future well-being of the ruling party,’’ said one of our sources.
   
 2. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo bilionea wa CCM ni nani na hao wa upinzani wanaokula matapishi ni akina nani?

  ThisDay has never lied to us on serious issues.
   
 3. M

  Mpingo1 Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani anaongelewa RA. Na chama chenye nguvu pande zote za muungano kinaeleweka!.......
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hujaweka source ni: ThisDay na kwa kiswahili iko katika KULIKONI ya leo, mwenye soft copy aiweke hapa ya Kiswahili.
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hamna kitu wanataka kumsema EL tu.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Haya yanatokana na maelezo ya Lwakatare (aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CUF upande wa bara). Baadhi ya JF members walishatoa dondoo hapa, kumbukeni maneno ya wakuu Paparazi Muwazi na Philemon.

  Rostam amekuwa mfadhili wa baadhi ya vyama vya upinzani hasa CUF, NCCR na TLP. Lengo la RA ni kupigania nafasi yake ktk ufisadi, ili asiumbuliwe na akina Mrema na hawa jamaa wa CUF na NCCR. Pili ni kuvuruga upinzani ili wasiweze kuwa na umoja unaoweza kuitishia CCM ktk chaguzi. Tatu, ni kupata wafuasi watakao msaidia kupambana na Mengi, Mwakyembe nk. Pia anapigania nafasi ya Dowans. Rejeeni maneno ya Mrema, Mbatia na Prof. Lipumba juu ya ufisadi na suala la dowans hasa baada ya uchaguzi wa Tarime,
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  mbona unajihami mapema hivyo? umepitia nyaraka za Lwakatare alizoziwasilisha kwenye vikao vya kamati kuu ya CUF? kama bado tafuta hiyo thread.
   
 8. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  HARAKATI UCHAGUZI MKUU 2010

  Mjumbe wa Kamati Kuu CCM afadhili wapinzani

  • Alisaidia chaguzi Busanda, Magogoni
  • Sasa atafuta mtandao Zanzibar, Pemba

  MWANDISHI WETU
  Dar es Salaam

  WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 likipanda, mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametajwa kuwa mfadhili mkuu wa chama maarufu cha upinzani kwa muda mrefu sasa.

  Ufadhili wa mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM umeelezwa kutumika kufanya mikakati dhidi ya chama chake na dhidi ya vyama vingine vya upinzani, hali iliyoelezwa kuibua utata ndani ya chama chake na hata kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho anachokifadhili.

  Habari za ndani kutoka kwa watu walio karibu na kiongozi huyo wa CCM zinaeleza kwamba hivi karibuni mjumbe huyo wa Kamati Kuu ametoa mamilioni ya fedha kusaidia chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Magogoni, Zanzibar na ule wa Busanda mkoani Mwanza, lakini chama hicho kilibwagwa na CCM.

  Mbali ya kujiwekea kinga ya kisiasa, kigogo huyo wa CCM ameelezwa kulenga “kusimika” wabunge wengi kutoka kambi ya upinzani na ikibidi hata mgombea wa urais, hatua ambayo inalenga kumpatia nguvu kubwa ndani na nje ya Bunge jipya, bila ya yeye kutoka CCM.

  Imeelezwa kwamba mjumbe huyo amekuwa akikisaidia chama hicho kwa muda mrefu sasa, lakini amezidisha misaada yake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kugharimia chaguzi ndogo zilizopita.

  Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM ameithibitishia KULIKONI wiki hii kwamba, kiongozi huyo wa CCM amekuwa na uhusiano wa karibu na chama hicho cha upinzani na kuna wakati hata katika vikao rasmi amethubutu kukitetea.

  Imeelezwa kwamba kiongozi huyo wa CCM ambaye amekuwa akisaidia pia chama chake kwa mbinu za kupata malipo zaidi kwa njia zisizo halali, amewahi kuthubutu kudai kwamba CCM haitaathirika ikiwa na ushirikiano na chama hicho, msimamo ambao haukuwahi kupata baraka za vikao halali vya chama chake.

  Kwa sasa sehemu kubwa ya maamuzi, ratiba na hata misimamo ya chama hicho inategemea maelekezo ya mwana CCM huyo ambaye ameelezwa kwamba amekuwa akitumia nafasi hiyo ‘kupunguza kasi’ ya watu anaowaita maadui zake kisiasa na kijamii.

  “Hivi sasa kiongozi mmoja mwandamizi wa chama hicho anakaa katika hoteli moja iliyopo Dar es Salaam ambako anakula na kulala bure. Kada huyo wa CCM ana hisa katika hoteli hiyo. Kwa kweli hiyo hali haiashirii kuwapo amani hata kidogo ndani ya vyama hivi viwili,” anasema mwanasiasa mmoja mstaafu anayefahamu uhusiano wa mwanasiasa huyo na chama hicho cha upinzani.

  Mwanasiasa mwingine ndani ya upinzani amesema kwamba, huenda hiyo ikawa kashfa kubwa kuliko zote ndani ya siasa za vyama vingi kuzingatia wadhifa wa wahusika katika ushirikiano huo aliouita mchafu kati ya kigogo ndani ya chama tawala na wa upinzani.

  “Hii si mara ya kwanza kusikia habari hizo, lakini kwa kawaida hizi si habari njema kabisa kwa wana CCM, lakini pia kwa wanamageuzi nje ya CCM. Kama ingekuwa mwanasiasa huyo ametumwa na chama chake, mkakati wake mkubwa wa kukisaidia chama hicho kiana bila wenzake kujua usingekwamishwa na NEC iliyokutana Butiama,” anasema mwana CCM mwingine anayefahamu undani wa sakata hilo.

  Uchunguzi wetu umebaini kwamba, hata viongozi wa juu wa CCM, hususan wa upande wa Zanzibar, wameonyesha kukerwa kwao na taarifa za uhusiano kati ya kada mwenzao na chama hicho cha upinzani hata kabla ya uchaguzi wa Magogoni.


  ...................................

  Source: KULIKONI NA. 673 Alhamisi Juni 18, 2009
   
  Last edited by a moderator: Jun 18, 2009
 9. M

  Masatu JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Yah Chadema!
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hivi Chadema ilishiriki uchaguzi wa Magogoni?

  soma hapa
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  aya hizi zinadhihirisha kwamba huyu mtu ni Rostam Aziz
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Seek to understand before being understood!! Pengine ipo siku tutalijua jina la mtu huyo na motive zake kama ni njema au ndo mitego ya mishe mishe zake
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  aya hii inatoka kwenye waraka wa Lwakatare... connect dots... fumbo hili ni rahisi kufumbua.
   
 14. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Unajua Dowans iliibua mengi. Alliance of the willling ilionekana na hadi kesho kutwa inajulikana. Ni kweli CUF walilainishwa in a way nobody expected. Hata Chadema, kuna watu wake arguably. Huyu si mwingine ni .. PAPA upanga
   
 15. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Kwanini hawa THISDAY hawajamtaja kwa jina? Au na wao wameanza kumuogopa? Wakishindwa kumtaja Rostam tutawashitukia na wao.

  Kwa kifupi, taarifa za uhakika ni kwamba ni RA na anaifadhili CUF kupitia kwa mwanasiasa kijana wa Zanzibar ambaye yuko karibu sana na Maalim Seif Shariff. Nina hakika Seif hawezi kukubaliana na hali hiyo japo kwa sasa CUF imeanza kupoteza mwelekeo kama haitazinduka na kuchukua hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kujirudi katika mapambano kama kilivyokuwa awali.

  Mapambano si ya kufanya fujo bali ya kupiga vita rushwa na ufisadi na uovu wote katika jamii. Prof Safari aliposema watu walimuona kama mtu asiyefaa na mwenye uroho wa madaraka, sasa watu watamkumbuka.

  Lakini hatuwezi kushangaa kwani RA mwenyewe alitoa siri ya kumpa fedha Mtikila kwa kigezo eti alimkopesha, lakini amemuumbua kwa kuwa Mtikila alimgeuka na hao CUF wajue wakithubutu kumgeuka atawaumbua na kumtaja huyo mwanasiasa aneyemfadhili pale hotelini Dar.

   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Safi sana RA. Mimi nazimia mafanikio yako, unawafanya hata ma profesa wakusujudu! Duh!!

  Mi nikiwaambia kuwa upinzani bongo hamna bali NJAA tu zinawasumbua mnakataa!!!

  CCM Hoyeeeeee!
   
 17. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ndio maana lipumba alikuwa mkali sana kwa mengi nini kuhusu kutaja mafisadi papa?
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Fumbo la vyama vya upinzani bado, mbona mnaitaja CUF wakati taarifa zinasema anafadhiri vyama? msione aibu semeni hicho chama kingine basi.
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwani kuna siri gani katika hili? ThisDay wameshindwa vipi kumtaja kwa jina? Mbona mwenyewe alisema hata Mtikali alimpa sh. milion Tatu. Sidhani kama kuna siri juu ya hili kwakweli.
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tina,
  Hivi anayekaa hotelini ni Prof. Lipumba nini?
  Kama ni huyo, basi nabadili URAIA na UKABILA. Au itabidi nianze kutafuta kithibitisho kuwa Lipumba SI MNYAMWEZI. Kama Mirambo akifufuka leo, basi huyu Lipumba atachukuliwa ISELAMAGAZI na Walugaluga, na akifika huko basi watapiga hadi mifupa ionekane.

  LIPUMBA UNATUTIA AIBU KAKA YETU. Kama mambo magumu, nenda tu UDSM ukafundishe na uachane na haya MATAPISHI. SHAME ON YOU.

  BURN: Huyu kaka yetu, vijana wa CCM Tabora, CCM Tabora, kwa kweli itatufanya milele tubaki na umasikini wetu, Wanyamwezi siye. Sijui tumelaaniwa nini?

  "LIPUMBA veve, lekaga ikuluye kulya vya vantu, vilakufumile mu-nyindo."
   
Loading...