Top 5 yako ya Romantic Movies

Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
6,629
10,707
IMG_3175.jpg


Hugh Grant amecheza kama Muingereza flani ndani ya London mchovu ana hangaika na duka lake la vitabu huko Notting Hill(mfano Manzese changanyikeni)

Siku moja akiwa dukani anaingia Muigizaji wa kike nguli na maarufu kutoka marekani, utamu unaanzia hapo, but baada ya tofauti zao kubwa za kipato mazingira na umaarufu wanakuja kuwa wapenzi. Kuna black comedy flani hivi amazing

IMG_3176.jpg


Demu na mshkaji walitongozana kwenye dating site wakapanga waonane wayajenge. Walipokutana kwenye dinner hawakupendana kabisaa, basi ikabidi jamaa ampe lift demu kumrudisha kwake. Njiani waka simamishwa na polisi mzungu akawadhalilisha na kumshuti demu, jamaa akaingilia na katika kunyang’anyana bunduki na polisi bahati mbaya risasi ikafyatuka na kumuu askari. Ikabidi wakubaliane kutoroka na katika harakati za kutotoka wakageuka wapenzi. Inakisa kizuri sana

IMG_3178.jpg


(Korean) Jamaa alikua mgumu flani hivi halafu mtata, mtoto wa boss wake akamzimia mshkaji lakini jamaa akakza. Baadaye na yeye akammpenda yule binti wakaanza kuishi maisha safi sana

Ghafla demu akaanza kupoteza network, kuja kupimwa akaoneka anaugonjwa wa kusahau na kadiri siku zinavyo kwenda atasahau kila kitu. Jamaa alihangaika sana kwajinsi alivyompenda halafu demu akaanza kusahau vitu hadi mshikaji akawa hamtambui kabisa
Inasikitisha pia

IMG_3180.jpg

Daktari anamuwahi mgonjwa na demu anawahi harusi yake siku inayofuata lakini wanakwama airport ndege zote zimesimamishwa. Kwa bahati wanakutana na kukodi ndege ndogo pamoja. Wakiwa angani rubani anapata stroke na ndege inaanguka kwenye milima ya barufu

Rubani anakufa palepale demu anaumia na kuzirai kwa siku kadhaa kabla hajapata fahamu. Walikaa wiki kadhaa kwa taabu sana kwenye milima ya mabarafu kabla ya kuokolewa

Walipitia mengi pamoja kuweza ku survive katika mazingira yale kulikopekea mwisho wake kuwa mzuri

IMG_3177.jpg


Ka bwana mdogo hivi katata sana high school akafall in love kwa mtoto wa mchungaji. Dogo akakolea kweli kweli lakini akawa anashangaa kama vile demu hajali na hana future

Baada ya kubana sana kumbe demu ana kansa na amebakisha miezi michache kansa immalize. Basi dogo hakukuba hiyo hali lakini baadae akakubaliana na hali halisi, lakini akafanya kitu fulani amazing sana akaamua kutimiza ndoto zote demu wake alizokua anaziwish kabla hajafa.

Soo good


Zipi ni top 5 zako?
 
The Great Gatsby
A star is born
Twilight
Friends with benefits
Ae Dil Hai Mushkil

Honorable Mentions
-Titanic
-Ugly truth
-La la Land

Zipo kibao binafsi huwa najiconsider sinaga favourite ila hapo Ae Dil Mushkil ndio naiangaliaga mara nyingi zaidi... nadhani sabab ya soundtracks.

Nimeanza The great gatsby kwa sababu love stories zinakuwaga na tragic endings, sio happy endings mara zote kama movie zinavyoonyesha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom