Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

JamiiForums

Official Robot
Nov 9, 2006
6,064
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
8,829
2,000
Ni wanufaika wa vyeo tenda mbalimbali kwenye kampuni zake binafsi na Serikalini hao kutwa kumsifia bila Aibu
April 11, 2020

ZITTO KABWE AICHAMBUA RIPOTI YA CAG 2018/19
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe (Mbunge Kigoma Mjini), akichambua ripoti ya CAG kwa mwaka 2018-19 na Ripoti za CAG kwa miaka 5 ya serikali ya awamu ya tano .
Hivyo uchambuzi huo unalenga ktk maeneo makubwa kumi muhimu :


Source: Mwanahalisi TV
  1. Kuporomoka kwa makusanyo ya kodi : hivyo serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya bajeti na hivyo bajeti kukosa maana inayo kusudiwa ya uwiano wa makusanyo dhidi ya matumizi pia ufanisi wa kukusanya kodi.
  2. Deni la Taifa ktk awamu ya tano ya serikali ya CCM linakuwa kwa kasi kubwa yaani asilimia 12% kuliko kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi ulio ktk wastani wa asilimia. Serikali imeanza kushindwa kulipa madeni ya ndani mfano kulipia Hati Fungani yaani Government Bonds jambo lililo hatari maana yake wananchi na wanunuzi wengine wa hati fungani kukosa imani ya serikali kuweza kulipwa amana zao. Serikali inadaiwa kiwango kikubwa na watoa huduma ikiwemo wakandarasi, makampuni na watu binafsi. Wakala wa Barabara yaani TANROADS ni mdaiwa sugu mwenye deni kubwa yaani Bilioni 900. Serikali pia inaficha kipande cha madeni ya Hifadhi za Jamii yanayofikia trilioni 3 shilingi za kiTanzania na wastaafu kuwa ktk hatihati ya kushindwa kulipwa malipo yao.
  3. Ufisadi umerudi nchini kupitia transit goods kwenda nchi jirani umeongezeka sana kufuatana na taarifa ya CAG. Kiasi cha bilioni 300 ni kimepotea ktk awamu ya 5 huku awamu ya Jakaya Kikwete upotevu ulikuwa bilioni 45 tu.
  4. Kesi dhidi ya serikali yaani contingent liability kimefikia trilioni 1.8 za shilingi za kiTanzania kutokana na kutotii mikataba na wadai kukosa imani ya kulipwa.
  5. Manunuzi yasiyofuata sheria yafikia Shilingi Trilioni moja kwa unapproved suppliers.
  6. Serikali inaendelea kutumia fedha za umma bila kufuata katiba ibara ya 135 yaani kupitia mfuko Mkuu wa serikali yaani Consolidated fund bila idhini ya Controller and Auditor General.
  7. Ukaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania umefanywa na GAG bila kutumia kampuni za Ukaguzi za binafsi Dillotte, KPMG n.k hivyo kukosa uwazi na uhuru wa kufanya ukaguzi huru unaoaminiwa na IMF, WORLD BANK na wabia wengine.
  8. Korosho zanunuliwa na fedha kutoka Benki Kuu na fedha hizi hazijarejeshwa Benki Kuu
  9. Ndege kununuliwa bila taratibu za kifedha zilizo wazi.
 

Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
5,266
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Tunahitaji katiba mpya ambayo hizo sauti zitapewa uzito
 

emfmpm

New Member
Jul 18, 2014
4
20
unyanyasaji wa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda umekithiri sana nchini kote, kila kituo cha polisi utakuta kimejaza pikipiki nje utadhani ni mojawapo ya mapambo ya vituo vya polisi.
 
Top Bottom