Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

JamiiForums

Official Robot
Nov 9, 2006
6,092
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
 

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,485
2,000
Watanzania wamechoka kuendelea kusikiliza kauli chafu zitokazo kwa baadhi ya Wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Tunaonba serikali ifanye kazi yake. Hatuwezi kuvumilia lugha chafu zinazoashiria uvunjifu wa Amani.
 

Atlantis Voyager

Senior Member
Jan 19, 2018
168
250
Keri kubwa ni hivi vibali vya ujenzi. Mtu unaongeza chumba chako kimoja . Mtendaji anakuja anataka rushes ukikataa anakupiga faini na barua limetoka manispaa na muhuri ameligonga. Huu ni utapeli maeneo yetu hayajapimwa iweje ulazimishe kibali na hizi hela wanakuja mgambo wa kata na Mtendaji.

Ikiwezekana futa kabisa Mambo ya watendaji wa kata hawana Cha maana wanachofanya zaidi ya fitina na kukamua wananachi pesa. Misharahara yenyewe haipandi bado Kila mtu anageuka zakayo mtoza ushuru
 

Forforty

Member
Nov 13, 2019
84
125
Watanzania wamechoka kuendelea kusikiliza kauli chafu zitokazo kwa baadhi ya Wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Tunaonba serikali ifanye kazi yake. Hatuwezi kuvumilia lugha chafu zinazoashiria uvunjifu wa Amani.
Hizo lugha chafu ni zipi? Na ni mgombea gani kazitoa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom