KWELI Tofauti na tamaduni iliyozoeleka ya Rastafarians, Lucky Dube hakuwahi kuvuta bangi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kama ilivyozoeleka kwenye jamii nyingi kuwa ukiwa Rastafarian basi kwa asilimia kubwa utakuwa unatumia bangi/marijuana na majina mengine lukuki kama inavyojulikana.

Leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa kuna meme inasambaa ikiwa na ujumbe "Wakati Lucky Dube anaimba "Born to Suffer" me nilidhani ni sababu anavuta bangi"

Meme hii ikanikumbusha article niliyowahi kusoma kuwa Lucky Dube alijiepusha na matumizi ya bangi, pombe na sigara ili kuwa mfano mzuri kwenye jamii.

IMG-20240119-WA0029.jpg
 
Tunachokijua
Lucky Philip Dube alizaliwa 3 Agosti 1964 huko Ermelo Afrika ya Kusini. Alikuwa mwanamuziki wa reggae na Alirekodi albamu 22 katika lugha ya Kizulu, Kiingereza na Kiafrikaans katika kipindi cha miaka 25 na alikuwa mwanamuziki wa Reggae kutoka Afrika Kusini ambaye aliuza albamu nyingi sana.

Wazazi wake walitalikiana kabla ya yeye kuzaliwa na alilelewa na mama yake, Sarah, ambaye alimpa jina hilo kwa sababu alichukulia kuzaliwa kwake kama bahati baada ya mimba nyingi kutoka/kuharibika. Pamoja na ndugu zake wawili, Thandi na Patrick, kwa kipindi cha muda mrefu utotoni mwake Dube aliishi na bibi yake, baada ya mama yake kuhamishwa kufanyia kazi sehemu nyingine. Kwenye mahojiano ya mwaka 1999 alimsimulia bibi yake kama "mpenzi wake wa dhati" ambaye "alisaidia vitu vingi kumkuza kuwa mtu wa kuwajibika aliye sasa."

Dube aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliokuwa wanataka kumpora gari lake, wakati wa tukio hilo alikuwa na watoto wake wawili. Kifo chake kilitokea katika kitongoji cha Rosettenville huko Johannesburg jioni ya 18 Oktoba, mwaka 2007.
1705748476093-png.2877276

Lucky Dube aliwahi kuvuta bangi kwenye historia ya maisha yake?
Thokozani Dube, mtoto wa marehemu nguli wa muziki wa Reggae Lucky Dube aliwahi kujibu katika mahojiano na kipindi maarufu cha dunia cha Reggae cha Rasmoral Katika KALEAWO FM katika eneo la Volta nchini Ghana na alieleza kuwa baba yake hakuwahi kuvuta Bangi wala sigara enzi za uhai wake.

Blog ya Opera News Imemuandika Lucky Dube kama miongoni mwa watu wenye imani ya Rastafarians na muimbaji wa muziki rege ambaye hakuwahi kuvuta bangi, sigara wala kuywa pombe kama wengi wanavyoweza kudhani, limeandika alifanya hivyo ili kuwa mfano bora kwa watoto wake.

Pia Lucky Dube kupitia Album yake ya Trinity kwenye wimbo alioupa jina la "Rastaman's Prayer" Alizungumzia makundi matatu ya watu ambao wanataka kumshukuru Mungu, moja ya kundi hilo ni wavuta bangi, alisema: Watu wanaovuta banngi wanataka kukushukuru Mungu kwa kuotesha bangi kimataifa, japo Polisi wamekuwa wakikata na wakati mwingie kuichoma ila bado inastawi, wavuta bangi wanataka kukushukuru. Katika tungo hiyo amewaongelea wanaovuta bangi na yeye kajitoa ikiwa na maana si mtu anayetumia kitu hicho.
1705744047238-png.2877214
Pia kwenye wimbo wake uitwao Up with hope ameimba kuhusu kukataza madhara ya kutumia madawa ya kulevya, kuywa pombe na kuvuta vilevi akiwaasa kuwa wasikilizaji wake kuwa si vitu vizuri kwao, hiyo inaonesha jinsi alivyokuwa kinyume na matumizi ya vilevi.
1705747490653-png.2877265
JamiiCheck, imefuatilia machapisho mbalimbali na mahojiano ya mwanaye ikiwemo baadhi ya nyimbo za Lucky Dube ambazo alionesha kukiri matumizi ya vileo kutokuwa mazuri, hivyo ni ukweli uliowazi Kuwa Lucky Dube hakuwahi kunywa pombe, kuvuta bangi wala sigara kwenye uhai wake.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom