orangutan
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 757
- 773
Dini ya urasta ilianzishwa miaka ya 1920 na 1930 huko maeneo ya visiwa vya Caribbean. Mwanzilishi wa imani hii ni Marcus Garvey aliezaliwa mwaka 1887 na kufariki dunia mwaka 1940. Marasta huamini kwamba huyu jamaa ni Yohanna mbatizaji wa pili kwasababu alitoa unabii wa kutokea mfalme Afrika ambae ndie atakuwa mkombozi wa waafrika wote dhidi ya udhalimu wa mtu mweupe (Babylon).
Marcus Garvey alihubiri kwamba waafrika ndio Waisrael wa Kweli waliopelekwa utumwani kama adhabu ya dhambi zao. Mnamo mwaka 1927 Marcus Garvey alitoa unabii kwamba atatokea mfalme barani Afrika ambae atakuja kuikomesha hiyo adhabu ya utumwa na kuwarudisha waafrika wote Afrika (Zion/Sayuni). Alitamka 'Look to Africa, for a king shall be crowned'.
Dini ya urasta ina wafuasi zaidi ya milioni moja duniani kote. Marasta huamini katika Mungu wa kikristo anaeitwa Judeo au Jah. Marasta huyatumia maandiko ya biblia agano la kale na kitabu cha ufunuo huku wakiwatukuza sana manabii Musa na Eliya. Wanaimani kwamba Yesu Kristo alikuwa ni mtu mweusi na pia wana biblia yao inayoitwa 'The Piby' ambayo wameondoa baadhi ya vitabu na mistari wanayodai imeandikwa na watu weupe ili kupotosha maana iliyokusudiwa kuandikwa hapo awali.
Licha ya kuwa urasta ni dini iliyosambaa duniani kote, dini hii haina uongozi maalumu kama zilivyo dini nyingine. Hii imepelekea dini hii kuwa na vimatawi vingivingi na kutofautiana kwa baadhi ya misingi kulingana utofauti wa kijiografia. Kuna baadhi wanaichukulia Rastafarianism kama dini huku wengine wakiona ni kama njia ya maisha tu. Licha ya tofauti hizi, marasta wote huamini kwamba Haille Selassie I ndiye mfalme wa kweli aliyekuja kama kristo mpya (Jesus reincarnation).
EMPEROR HAILLE SELASSIE I.
Mwaka 1930 Ras Tafari Makonnen alichaguliwa kuwa mfalme wa Ethiopia. Huu ulikuwa ni ukamilisho wa unabii alioutoa Marcus Garvey kwamba 'tazama mfalme atavikwa taji Afrika'.
Na pia ulikuwa ni ukamilisho wa maandiko ya kibiblia kutoka verses zifuatazo.
Ufunuo 5:5 'Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, chipukizi wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu.”
Ezekiel 28:25 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya na kuwaleta Waisraeli kutoka katika mataifa yote ambamo walitawanywa. Hivyo nitawafanya watu wa mataifa waone kuwa mimi ni mtakatifu. Watu wa Israeli wataishi katika nchi yao ambayo mimi nilimpa mtumishi wangu Yakobo".
Ras Tafari Makonnen akajiita Emperor Haille Selassie I, Mfalme wa wafalme, Simba mshinda vita wa Yuda, Mteule wa Mungu.
Na marasta wote duniani wakaamini kwamba unabii umetimia na kwamba adhabu waliyopewa na Mungu (divine punishment) imefikia ukomo na kwamba umetimia muda wa kurudi Zion (Afrika).
Haille Selassie I alikuwa ni muumini wa dhehebu la kikristo la Orthodox. Waumini wote wa Rastafarianism wakaamini kwamba Haille Selassie I ndiye Mungu katika umbo la mwanadamu na ndio ule ujio aliouhaidi Yesu kwamba atarudi tena.
MKANGANYIKO
Licha ya Emperor Haille Selassie I kutukuzwa kama Mungu mtu na waumini dini ya urasta kutoka Jamaica, yeye mwenyew alikuwa anakana kwamba yeye sie huyo waliemdhania kuwa ndie! Kwenye mojawapo ya mahohiano aliyowahi kufanyiwa na BBC Sellasie alieleza kwamba yeye ni mwanadamu wa kawaida tu wala sio huyo aliyeahidiwa kwenye maandiko matakatifu.
Mnamo mwaka 1937 Marcus Garvey aliandika kitabu alichokiita 'Kufeli kwa Haille Selassie I kama mfalme'. Garvey alionyeshwa kukatishwa tamaa na namna Haille Selassie alivyokuwa anauendesha ufalme wake hasa pale alipopigwa na Waitalia na akakubali kusaidiwa na Waingereza ili aweze kulikomboa taifa lake kutoka utawala wa Italy. Garvey alimuona kwamba Selassie kuwa ni kiongozi mwenye mapungufu mengi sana.
Mwaka 1950 mfalme Haille Selassie I alikutana na viongozi wa marasta nchini Ethiopia na wakajadili namna ya kuweza kuwakomboa waafrika walioko nchi za utumwa ili waweze kurudi Afrika (Zion). Mwaka 1955 Haille Selassie alitoa ekari 500 za ardhi yake mwenyewe binafsi maeneo ya Shashemene na kuwakabidhi marasta ambao watakuwa wako tayari kurudi Afrika. Mpaka mwaka 1960 marasta zaidi ya 2,200 walifanikiwa kwenda kuishi huko Ethiopia lakini kutokana na kutokukubalika kwao na jamii ya wazawa wa Ethiopia pamoja na umasikini uliokithiri wengi wao walifariki na inakadiriwa mpaka leo hii wamesalia kama 250 tu.
SIKU YA KIHISTORIA
Mnamo tarehe 21 April 1966 Haille Selassie I aliitembelea Jamaica kwa mara ya kwanza.
Hii ilikuwa ni siku kubwa sana na ya kihistoria kwa marastafari wote (Kumuona Mungu mtu na baadhi yao kufanikiwa kupeana mikono). Kuanzia siku hiyo hadi leo tarehe 21 mwezi April ni sikukuu ya marasta duniani kote.
Akiwa Jamaica Haille Selassie I aliwashauri marasta wote kwamba kabla hawajafikiria kuja Afrika lazima wajikomboe kwanza kutoka kwa minyororo ya mtu mweupe.
ANGUKO LA HAILLE SELASSIE I
Mwaka 1974 serikali ya mfalme Haille Selassie I ilipinduliwa kijeshi na yeye mwenyewe akapewa kifungo cha ndani (house arrest). Inasemekana mwaka 1975 aliuawa na watekaji wote.
Lakini mpaka leo hii marasta hawaamini kwamba Haille Selassie I aliuawa. Wanaamini kwamba yupo hai na anaendelea kuishi. Hii ni kutokana na imani ya marasta ya kutokuamini maisha baada ya kifo. Marasta huamini kwamba wao hawataonja umauti bali wataendelea kuishi milele na milele katika mifumo na sura zingine (True rastas are immortal and everliving).
MATAWI YA MARASTA DUNIANI
Rastafarianism imegawanyika katika makundi makubwa matatu ambayo ni Nyahbinghi, Bobo Shanti na makabila 12 ya Israeli.
1. Nyahbinghi
Hili ni kundi la marasta wanaomuamini Emperor Haille Selassie I kama Mungu aliyekuja duniani katika umbo la kibinadamu. Jina la Nyahbinghi limetokana na Queen Nyahbinghi wa Uganda aliepigana na wakoloni karne ya 19.
2. Bobo Shanti
Hili tawi lilianzishwa na Prince Emmanuel Charles Edward miaka ya 1950. Bobo maana yake ni weusi na Shanti ni kwa ajili ya kabila la Waashanti wa Ghana. Waamini wa hili tawi wanaitwa 'Bobo dreads'.
Bobo dreads wanamuabudu prince Emmanuel Edward (wakiamini kwamba ni ujio wa Yesu Kristo kwa mara ya pili), wanamuabudu na Emperor Haille Selassie I. Pia wanaamini kuwa ipo siku watalipwa fidia kutokana na kutumikishwa utumwani. Bobo dreads huvaa nguo ndefu pamoja na kuvaa vishungi kuzunguka vichwa vyao vyenye rasta. Bobo dreads wanaziamini sheria za kiyahudi na sabato. Hupenda sana usafi wa mwili na mara nyingine hutembea na mifagio kuashiria hulka yao ya usafi na unadhifu.
3. Makabila 12 ya Israeli
Hili tawi lilianzishwa na Dr. Vernon 'mtume wa Mungu' Carrington mwaka 1968.
Wafuasi wa hili tawi wanaruhusiwa kuabudu kwenye kanisa lolote watakalopenda.
TAMADUNI NA IBADA ZA MARASTA
Ibada za marasta hufanyika katika namna mbili: Tafakari (reasoning) na Nyabinghi (Dansi ya marasta).
1. Tafakari.
Hapa marasta huwasha ganja (bangi) na kisha huanza kuvuta kwa kuizungusha kwenye hilo duara huku wakijadili na kuitafakari maandiko ya biblia yao (The Piby). Tafakari hii huisha pale marasta wanavyoanza kuondoka mmojammoja mpaka wanavyoisha.
2. Nyabinghi
Hii ni dansi maalumu inayofanyika nyakati za usiku na inaweza ikaendelea mpaka asubuhi. Hii mara nyingi hutanguliwa na kuvuta ganja. Muda wa mchana marasta hupumzika na kufanya tafakari halafu jioni dansi inaendelea tena. Hii inaweza ikafanyika kwa siku kadhaa na marasta kutoka sehemu mbalimbali hukutana kwa ajili ya hii ibada.
TAMADUNI
Marasta wana lifestyle yao ya kipekee kabisa. Marasta huamini katika kufuga dreadlocks kutokana na maandiko ya biblia kutoka kitabu cha Walawi 21:5 "Wazawa wa Aroni kamwe wasijinyoe upara kuomboleza wala wasikate pembe za ndevu zao wala kujichanja chale mwilini".
Pia nywele nyingi huwafanya wawe na muonekano wa mnyama simba (Simba wa Yuda), nywele pia huashiria uasili, nguvu na kuonyesha kuwa mizizi ya urasta iko Afrika.
Uvutaji wa bangi (Ganja).
Marasta hutumia bangi katika ibada (tafakari) na pia kwa ajili ya sababu za kitabibu. Wanaamini hilo limeruhusiwa kutoka kwenye biblia Zaburi 104:14
"Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo,
na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini". Pia Mwanzo 3:18, Kutoka 10:12 na Mithali 15:17.
Marasta hawapendi kutumia vilevi vya pombe kwasababu vinampumbaza mtu na kumpa nafasi Babylon kufanya maovu juu ya rasta. Wao huamini kwamba bangi humfanya mtu kuwa conscious (muelewa) na kumsogeza mtu karibu na utukufu wa Bwana. Bangi ni mmea mtakatifu kwa marasta.
Ulaji wa nyama
Marasta hawaruhusiwi kula nyama. Hawali mayai wala maziwa. Badala yake wao hula vyakula vya asili ya mbogamboga vikiwa katika uasili wake (Vegetarians) . Hawapendi vyakula vya viwandani wala vya supermarket. Wana utaratibu wao wa chakula wanaouita 'ital' ambao ni kula vyakula vya asili tu.
Marasta hawaamini maisha baada ya kifo (afterlife). Wao huamini kwamba rasta wa kweli hawezi kufa bali ataishi milele (everliving) katika nchi aliyoahidiwa ambayo ni Afrika (Zion).
Kwa leo inatosha wakuu, unaweza ukakosoa au ukaongezea sehemu penye mapungufu. Naamini kuwa kama umesoma mpaka hapa utakuwa umepata elimu fulani kuhusu urastafari.
Jah Rastafari! PEACE.