BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha wadau kujadili kuhusu adhabu ya Kifo, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia amesema mifumo ya haki haipo madhubuti na kuweza kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa aliyetiwa hatiani ana kosa
Ameongeza kubwa “Adhabu hii ni hatarishi kwa uhai wa watu ambao hawana hatia, pia ni adhabu ambayo imepitwa na wakati kwa kuwa imejengwa katika mfumo wa kisasi kwamba anayeua na yeye auwawe. Ukitengeneza mfumo wa Haki kwa utaratibu huu hauwezi kubadili makosa ya mkosaji
Sungusia amependekeza kuwepo adhabu mbadala, mtu akitiwa hatiani kwa kosa la kuua apewe kifungo maalumu na ikiwezekana akae kwenye Gereza maalumu la kuzalisha mali na Serikali isitumie fedha zake kuwahudumia ili Wafungwa wafanye shughuli za uzalishaji.
=========