Salamu mbele!
Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimesema maoni na mitazamo yanayotolewa na wanachama au viongozi wa TLS kwenye akaunti zao binafsi siyo mtazamo wa chama hicho.
Kauli hii ya TLS inakuja ikiwa ni siku mbili toka Rais wa chama hicho cha wanasheria wasomi kutangaza kupitia akaunti yake ya twitter kuwa anaunga mkono na kusapoti haki za wapenzi wa jinsia moja nchini au mashoga. Swala hilo lilizua mkanganyiko na mtanziko huku wengine wakiuhusisha mtazamo huo na mtazamo wa TLS.
Hata hivyo kumekuwepo na mkanganyiko juu ya iwapo maoni ya Rais wa chama hicho yanaweza kutenganishwa na mtazamo wa chama ikiwa msemaji anayetambulika kisheria ni Rais wa chama.
View attachment 920352