TITUS AMIGU: NI MTEGO MBAYA SANA

EP cosmetics

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
2,469
3,844
Kutoka kwa Pd. Titus Amigu:

NI MTEGO MBAYA MNO

Katika suala la baraka mgogoro ni kwamba mashoga na wasagaji ni WANAHARAKATI (ACTIVISTS). Ndiyo maana watakuja kanisani kuomba baraka wakijitambulisha. Wanapigania kutambuliwa kisheria, kijamii na kikanisa (kidini). Kwao kuwapa baraka maana yake ni KUTAMBULIWA NA KUKUBALIWA NA KANISA. Kwao huo ni mwanzo wa USHINDI. USHINDI kamili utakuwa kufungishwa ndoa katika Kanisa Katoliki. Wadhambi wengine hawafanyi uanaharakati ndiyo maana hawajitambulishi. Walevi, wazinzi, waasherati, wambea, mafisadi, waongo, majambazi, wevi, wauaji n.k. hawajitokezi kuomba baraka wakaendelee kuishi katika dhambi zao kwa baraka ya Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mashoga na wasagaji hawaji kuomba baraka kusudi waongoke bali washinde katika itikadi na chaguo lao. Kinyume chao, wadhambi wengine ni wanyonge wanaopambana wabadilike (metanoia). Kwa kisa hicho wanakuja wakiwa wanyonge mbele ya Mungu huku dhamiri zao zikiwauma. Kinyume chake mashoga na wasagaji ni WABABE wanaojitokeza wakijisikia ni mashujaa wa kutangaza hali zao kadamnasi pasipo kuumwa na dhamiri. Mashoga na wasagaji (na LGBTQ+ kwa ujumla) WAMEPANIA kulishinda Kanisa washerehekee uhuru wa mapenzi, mtego ambao Papa ananasa pasipo kuutambua au kama anautambua basi ameamua kusaidia utunase Wakatoliki. Mashoga na wasagaji hawaombi baraka kusudi wakaache mwenendo wao mbaya. Hawaji kuomba baraka eti wakapate nguvu ya kuachana. SIVYO! Na hili ndilo jambo ambalo watu wanataka kumwelewesha Papa. Kuacha dhambi hakuhitaji kwanza kubarikiwa rasmi. Ni uamuzi wa dhati tu. Mwanampotevu hakuja kwanza kwa baba yake kuomba baraka kusudi akaache upotevu wake kisha arudi kuomba radhi. Anayetubu hapitii mzunguko mrefu hivi. Mimi nitakuja na andiko langu refu katika msimamo huu.
Mzee wenu Pd. Titus Amigu.
 
Back
Top Bottom