Wakuu.
Poleni na ugonjwa huu wa #covid19.Hili nalo litapita tu.Tuzidi kumuomba Mungu na kuchukua tahadhari.
Hawa watu wa intelijensia Tanzania,TISS,wanapataje watu wao? Sababu sijui kama kuna utaratibu wa kujiunga nao moja kwa moja.Kuna mtu aliniambia kuwa wenyewe ndo wanafuata watu na sio watu kuwafuata wao.Kama hiyo nadharia ni ya kweli,wanaangalia vitu au vigezo gani kuwapata watu wanaowahitaji?
Na pia ningependa kufahamu kama wana watu wao nchi zilizoendelea za dunia ya kwanza kama US,UK,Japan n.k.
Tusaidiane ujuzi,Asanteni.
#ChukuaTahadhari.
#StaySafe.