Timu ya wananchi kujenga uwanja kwa michango sio sawa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Bila kuwa Na makubaliano kuhusu namna ya kugawana mapato yatakayotokana Na uwanja uliojengwa Na wanachama Na mashabiki kwa michango yao ya mifukoni itakuja kutokea vurugu kubwa sana huko mbele ya safari.

Lazima mgawanyo wa faida itakayotokana Na uwanja kwa wanahisa ifahamike kabla watu hawajaanza kuchangia ujenzi wa uwanja. Iko siku mapato ya uwanja huo italiwa na MTU, familia, au kikundi kimoja tu cha watu. Ikitokea hivyo malalamiko yatazuka kwa wale wote waliochangia ujenzi wa uwanja huo.

Kulinda haki za watanzania serikali ihakikishe kuwa wananchi hawachangishwi ovyo bila kuwepo kwa andiko litakaloanzisha hiyo asset ya uwanja linaloonyesha umiliki Na mapato yatakwenda wapi.
 
Watu walikuwa wanaendesha timu kwa makapu sembuse kiwanja

Ndio tumuulize mleta mada kipindi kile Young Africans wanatembeza bakuli mbona watu hawakuhoji kuhusu michango na mgawanyo wa faida, au Uwanja wa Simba unataka kuwatoa roho kwa kuwa hata ninyi hamjapta akili ya kujenga!?

Unataka Serikali iingilie kati fedha mtu anazotoa kwa mapenzi yake binafsi!?
 
Yaani unataka wanachama wakubaliane kwanza jinsi watakavyokuwa wanagawana mapato? Nchi hii ngumu sana 😁😁😁
MTU kwenye maono anajiandaa mapema Na yajayo. Watu wasitumie mihemko kujenga uwanja (kitega uchumi) kwa hela za watu mifukoni bila kuwa Na andiko kuhusu uwanja, matumizi, mapato Na matumizi Na ziada itakavyogawanywa. Je, waliochanga watakuwa Na haki gani?
 
Kama viwanja kibao vimejengwa kwa nguvu ya wananchi lakini vipo chini ya umiliki wa CCM na maisha yanaendelea, itakuwa kwa umiliki wa klabu yao?
 
Kiongozi mchango wa hiari siku zote huwa hauna return, mtu anachanga alichonacho kama ameguswa, sio lazima.

Hakuna atakayekushikia panga uchangie.
Hilo unalosema linawezekana kwenye kuchangia harusi Na perishables, sio kwenye asset kama uwanja ambao utaingiza pesa. Unataka kusema wanachama na wachangiaji watakubali mapato yooooote ya uwanja wao yaende kwa Barbara Na familia yake bila kuhoji?
 
Uo mchakato lazima utakuwepo mambo yatawekwa wazi.
Lazima kuwe Na hisa, ili wachangiaji wanunue hisa ambazo zitakuja kurahisisha kwenye gawio kama faida itakujakuwepo huko mbele ya safari, vinginevyo uwanja utakujatiwa kiberiti Na waliochanga Leo.
 
Kwa sasa huu ni mchango wa kishabiki ila huko baadae unaweza kuwekewa mtazamo wa kitaalam.

Jambo la kwanza lilikua ni kujua uwanja unahitajika wa aina gani na thamani yake ni kiasi na kila upande uchangie shs ngapi, yaani muwekezaji na wanachama.
 
Ndio tumuulize mleta mada kipindi kile Young Africans wanatembeza bakuli mbona watu hawakuhoji kuhusu michango na mgawanyo wa faida, au Uwanja wa Simba unataka kuwatoa roho kwa kuwa hata ninyi hamjapta akili ya kujenga...
Zile ni fedha ambazo zililipa mishahara, nauli, chakula Na posho (utilities) Na kwisaha kabisa. Hii ni tofauti Na kujenga uwanja utakaodumu miaka 100 ukiingiza pesa.

Haiwezekani ni change Mimi lakini pesa ule we we? Je, kama timu ikifa uwanja unabaki kwa nani? Je kama uwanja utafanya faida pesa zitamnufaisha nani Na nani?
 
Ndio tumuulize mleta mada kipindi kile Young Africans wanatembeza bakuli mbona watu hawakuhoji kuhusu michango na mgawanyo wa faida, au Uwanja wa Simba unataka kuwatoa roho kwa kuwa hata ninyi hamjapta akili ya kujenga!?

Unataka Serikali iingilie kati fedha mtu anazotoa kwa mapenzi yake binafsi!?
Iyo haina tofauti Na upatu, deci. Chamlevi kuliwa Na mgema. Huu sio mchango wa kusoma hitima au communion ya mtoto, hiki ni kitega uchumi, wacheni uzuzu Na mihemko.
 
Kama viwanja kibao vimejengwa kwa nguvu ya wananchi lakini vipo chini ya umiliki wa CCM na maisha yanaendelea, itakuwa kwa umiliki wa klabu yao?
Si umeona hapo, siku ccm ikishindwa uchaguzi viwanja vyooote hivi vitarudi kwa wananchi, maana vilijengwa Na wananchi. Lakini kama ccm itajenga kiwanja kipya sasa hicho kitakuwa ni cha ccm hata kama kitashindwa uchaguzi
 
Haya sasa, kwa mfano huo, ikitokea siku kama hiyo kiwanja cha klabu kitatoka kwa nani kwenda kwa nani?
 
Zile ni fedha ambazo zililipa mishahara, nauli, chakula Na posho (utilities) Na kwisaha kabisa. Hii ni tofauti Na kujenga uwanja utakaodumu miaka 100 ukiingiza pesa. Haiwezekani ni change Mimi lakini pesa ule we we? Je, kama timu ikifa uwanja unabaki kwa nani? Je kama uwanja utafanya faida pesa zitamnufaisha nani Na nani?

Kwa hiyo mmeanza kuhoji kabla hata fedha hazijachangwa na wala uwanja bado haujajengwa, ni wapi Simba/Mo pamoja na wanahisa wengine wametoa tamko kwamba mapato yatakayotokana uwanja yatawanufaisha wao wao pekee!?

Unapompa ndugu yako mtaji wa biashara kama msaada kisha akafanikiwa huko mbeleni kwa msaada uliompa utataka mgawane kila faida atakayopata!?

Mimi naomba niishie hapa maana mitazamo yetu imetofautiana tu na haimaanishi kwamba uko sahihi au umekosea, ndivyo hivyo na kwangu ilivyo.

Kama unaweza kuchanga, changa.
Kama hauwezi kuchanga kaa kimya hakuna atakekushitaki mahakamani kwamba hujachanga.

Ahsante.
 
Haya sasa, kwa mfano huo, ikitokea siku kama hiyo kiwanja cha klabu kitatoka kwa nani kwenda kwa nani?
Shida hapo sio kiwanja, bali hela za kiwanja nilichochanga kujenga anakula nani? Maguli Na Bashiru walipowanyang'anya watu ulaji wa mali za ccm si uliona mwenyewe malalamiko?
 
Back
Top Bottom