SIRI NZITO ZA KAMPENI CCM ZAFICHUKA.
Hakuna siri ya watu wawili au zaidi, hili limethibitika ndani ya CCM baada ya mambo mazito kuibuka hivi karibuni kwenye kampeni za chama cha mapinduzi CCM.
Mnajua ni kwanini Magufuli na Samia wamebaki wapweke kwenye kampeni?
Mnajua kwanini Janauary Makamba anahangaika kuleta propaganda kwa kasi kubwa kuliko wana CCM wengine?
Najua wengi hatujui ni kwanini? Lakini kupitia mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ndani ya CCM ukweli umejulikan, umewekwa wazi.
Mh Mwigulu, Mh Mkapa,na viongozi wengine mashuhuri wa CCM wamemsusia Mgombea urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli kwasababu nyingi sana, mojawapo ya sababu hizo ni kwamba mgombea huyo hashauriki kabisa, habebeki ,anasema John Pombe magufuli anaona yeye anajua kila kitu zaidi ya wenye chama, pia ameonekana kuwa hakipaishi chama hata kidogo zaidi ameamua kujipaisha yeye peke yake.
Hali hii imewapelekea viongozi hawa kususia kabisa kampeni za mgombea urais huyo, lakinj pia mnyetishaji wetu kasema kuwa Mkapa toka alipozomewa Kagera kutokana na kauli yake ya kuwadharau wa Tz Basi kaamua kukaa mbali kabisa ili kulinga heshima yake kwa mataifa ya nje.
Lakini pia inasemekana kuwa mgombea uraisi huyo kawagomea baadhi ya waliotakiwa kuwa naye kwenye kampeni kwa sababu zake binafsi ambazo hazijawekwa wazi lakini mnyetishaji huyo alisema pia tabia za baadhi yao kutumia lugha chafu kwenye mkutano ni kikwazo kikubwa kwa mgombea huyo.
Lakini pia mnyetishaji wetu katueleza kuwa hadi sasa wapo hovyo kifedha japo inasemekana kuwa walichukua 40% ya bajeti kila wizara ili kusaidia kampeni. Amedai kuwa wameishiwa fedha kutokana na matumizi mabovu ya fedha hizo. Inasemekana kuwa kuna wengine wanaiba fedha za kampeni na kufanyia mambo yao na kumpa wakati mgumu mgombea wa ccm na msaidizi wake katika kufanikisha adhima yao.
Alidai kuwa mmoja wa wana team ya kampeni anayeungwa mkono na katibu wa CCM na Familia ya Jk kwa nguvu zote amekuwa akizitumia pesa nje ya makubaliano ya team hii imetokana na lengo lake la kujiimarisha yeye kisiasa.Na hii ndio sababu kuu za mmoja huyo kutumia nguvu kubwa kwenye kampeni hizi kupitia media na mitandao ya kijamii.
Mnyetishaji huyo alimtaja January Makamba kuwa anatengeneza mazingira ya kuwa waziri Mkuu endapo Magufuli atashinda na pia mazingira ya urais 2025,ametajwa kuwa mmoja wa wanaotengeza genge dogo ndani ya chama hicho.
Anatumia pesa nyingi kwenye wizara yake kwa ajili ya kuhakikisha umma unapotoshwa, kama alivyofanya kupitia kwa watafiti kama vile Taasisi ya Twaweza na nyinginezo na wasanii mbalimbali.
Hali hii mbaya imemfanya mkuu wa kaya kukimbilia nchi za nje.
Katika mazingira haya ya utata ambapo hadi sasa Mgombea urais amekuwa akiongozana na Bulembo ambaye ameonekana pia kuvuruga kampeni kwa kufanya siasa za 1995 kipindi hiki cha watu wenye uelewa, anapelekea kuzomewa kwa mikutano yao.
Mtoa taarifa kasema hali imakua mbaya kila siku, hali inayomkatisha tamaa Magufuli, alisema hali hii ikiendelea kuna uwezekano mkubwa sana Dr. JOHN POMBE MAGUFULI anaweza kujiengua na kusubili huruma ya Lowassa ateuliwe tu kuwa Waziri Mkuu au waziri wa wizara aliyopo hadi sasa.
Nitaendelea kuwapa taarifa kadri nitakavyozipata toka kwa mmoja wa waliopo kwenye team ya kampeni za magufuli.