mussa.lumala
Senior Member
- May 12, 2015
- 116
- 27
Wameoza hao, kazi yao kununua wasanii ndo iliobaki
Na hii ndio picha kwamba wananchi wamechoshwa na watawala.Mtoa mada una bahati sana kwamba habari yako itakuwa ni ya kuwafurahisha wengi hapa jamvini hasa wale wanaopenda
kutukana. Kwa mfano ungeandika Lowassa njiapanda timu ya kampeni imesambaratika ungetukanwa ungeitwa mnafiki,
Magamba, msaliti, Yuda yaani kila jina. Ila angalau ubunifu wako mzuri hapa utapewa hongera na kuonekana mpenda
mabadiliko.
Nimeambiwa kuwa ile ya kampeni ya CCM iliyoundwa kwa kumsaidia Dr. Magufuli na Mama Samia imesambaratika jana usiku baada ya kikao cha kimkakati. Nimearifiwa na mmoja wa wajumbe wa timu hiyo kuwa kusambaratika kwa timu hiyo kunatokana na sababu mbalimbali. Wapo wajumbe waliosusa baada ya kuona wananchi hawaelewi somo la CCM na kuielewa Ilani. Wananchi wamekuwa hawaelewi wanachoambiwa na sasa wajumbe wanaishiwa cha kusema.
Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa wanatuhumiana, na hata na Dr. Magufuli mwenyewe, kuwa ni popo wa kisiasa. Wanaunga mkono harakati za wapinzani kwa kificho na kumharibia Dr. Magufuli majukwaani kwa kutamka maneno ya kukwaza na kukera yanayochochea hasira za wananchi dhidi ya wagombea wa CCM wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani.
Wapo wajumbe waliosusa kutokana na kutotimiziwa matakwa yao hasa ya malipo kwa kila siku wanayoifanyia kazi. Wajumbe hao wamesema kuwa hawana muda wa kusubiri kulipwa baadaye kwakuwa uchaguzi ni bahati nasibu na lolote laweza kutokea. Wanasisitiza kulipwa marupurupu yao sasa kwa mujibu wa makubaliano ya kichama na kutoahidiwa kulipwa baada ya uchaguzi.
Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa hawapewi uzito na umaarufu kama ilivyotarajiwa. Wanamlaumu Dr. Magufuli na viongozi waandamizi chamani, kwa mfano, kumuamini sana Abdallah Bulembo ambaye hana hadhi kichama, kisera na kihela kupewa nafasi ya kutawala majukwaa kama afanyavyo sasa. Wanalalama kuwa watu maarufu wamewekwa kando na sasa wanaanza kuota utando.
Sasa timu imesambaratika. Dr. Magufuli yuko njiapanda kikampeni. Itambidi kupambana kiume ili kuendelea kujieleza mbele ya wananchi. Apambane kivyake sasa na watakaobaki naye!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
huo ndio ukweli,Ni hatari sana mtu kuwa maarufu na nguvu zaidi ya chama. Sina hakika ume-type ukiwa na mihemko au ndiyo ukweli wenyewe. Ila sishangai as kwenye kampeni, JPM anajinadi yeye mwenyewe badala ya chama, hata mabango yake say all.
Mheshimiwa umeandika kitu cha maana sana, lakini kumbuka siyo wewe tu ambaye unayetaka mabadiliko na maendeleoKuandika habari sio kuandika tu. Lazima ujue unaandika kuhusu jambo gani na kwa wakati gani. Unatukanwa kutokana na kuandika udaku, uzushi, kashfa zisizo na ukweli na mambo kama hayo sehemu ya siasa ambayo watu wanatumia akili nyingi, muda na mali zao kujadili mambo ya maendeleo. Ni mbaya sana kufikiria kwamba wenye kupenda mageuzi ya kimaendeleo hapa Jamii Forum kazi yao ni kutukana. Kumbuka JF wengi ni Great thinkers na nina amini hivyo nikijua hata wewe ni mmoja wapo, Sasa unapoleta habari za mzaha mzaha na habari zisizo na tija yoyote katika kulisukuma kurudumu hili na maendeleo sioni ni kwanini usitukanwe. Tujifunze kukubaliana na hali tuliyo nayo japo wakati mwingine itikadi zetu zina tofautiana.
Na hii ndio picha kwamba wananchi wamechoshwa na watawala.
wanakula nchi wanabakiza mtaji wa kutumia kulaghai wananchi pindi uchaguzi ukikaribia.
safari hii,hizo fedha wale watafiti,sisi msimamo wetu ni mmoja tu LOWASA for presidency.
endeleeni kula upepo. Kuna kila dalili mmeshindwa na ukawa yenu, mikutano inajielezaKauli mbiu yenu Hapa ni kazi tu, kweli mwaka huu kazi mnayo.
Ndio sababu kutwa kucha CCM inajaribu kufanya kampeni kwa kutumia lugha chafu, na hata kupika matokeo kwa kutumia TWAWEZA na REDET.
Ukweli ni kwamba Magufuli na CCM haiuziki, watu tumewachoka, na siyo siri.
Na hizo njama zinazotumiwa kutaka kulazimisha kukubalika ndizo zinazokwenda kuwamaliza!
Wananchi ningewaelewa sana kama wangekuwa wanataka mabadiliko chanya, na siyo haya tunayoyashabikia sasa.
Kulikuwa na watu ambao walianzisha UKAWA na walikuwa wana movements za ukweli na zenye maana na siyo hivi vituko
tunavyoviona sasa.
Wala siyo ubunifu, ni taarifa zilizothibitishwa toka ndani ya "kamati" Na ni kweli kamati imebomoka jana usiku. Na ajabu kuna ya ghafla imeundwa ikiongozwa na naibu waziri fulani Kijana kuliko wengine.
VUTA-NKUVUTE
Umeamua kuwapunguza nguvu wapinzani wa CCM kisayansi zaidi kuliko hata Twaweza walivyofanya.