amour msellem
Senior Member
- Aug 16, 2015
- 106
- 20
Tatizo si magufuli ila tatizo ni Sisiem
Mwizi kukataa kujengwa kituo cha polisi hapo hakuna la ajabu.Kwa mtazamo wako upo sahihi, ila kwa mtazamo wangu mimi naona watanzania kwa kuichoka kwetu CCM tunataka kuipa
nchi kwa kundi fulani la watu ambao hata hao CCM waliwakataa.
Kama lowasa ameshindwa kukontrol kinyesi chake kitoke wakati gan na wakati gan kisitoke ataweza kweli kuzuia gesi yetu isitoke
Hahaha
Ni Kama Ambavyo Sumaye Yeye Mwenyewe Tu Alishindwa Kutusua Kama Siyo Kutoboa Kwenda IKULU Pamoja Na Kujaribu Kwake Mara Mbili Bila Mafanikio Leo Na Yeye Ndiyo Kampeni Meneja Wa Muhanga Mwenzie Lowassa. Hivi Tangia Lini Maiti Akamsaidia Marehemu KUZINDUKA?
Ukiitwa uthibitishe hili unaweza fanya hivyo au unatiririka tu??????
Na bado mwaka huu lazima tukingoe chama cha kijani
Na hii ni gud niuz...
Hawezi fungua mahakama ya mafisadi bila kujitenga na mafisadi...
Hilo ndio jeshi la mtu mmoja....
Subirini mabadiliko toka ndani...
Kila mnavyomuandika huyu JPM mnafanya tuso na vyama tuzidi kumuamini...
Tunataka rais independent ...asiyefungamana na matajiri wala mfumo...
Nimeambiwa kuwa ile ya kampeni ya CCM iliyoundwa kwa kumsaidia Dr. Magufuli na Mama Samia imesambaratika jana usiku baada ya kikao cha kimkakati. Nimearifiwa na mmoja wa wajumbe wa timu hiyo kuwa kusambaratika kwa timu hiyo kunatokana na sababu mbalimbali. Wapo wajumbe waliosusa baada ya kuona wananchi hawaelewi somo la CCM na kuielewa Ilani. Wananchi wamekuwa hawaelewi wanachoambiwa na sasa wajumbe wanaishiwa cha kusema.
Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa wanatuhumiana, na hata na Dr. Magufuli mwenyewe, kuwa ni popo wa kisiasa. Wanaunga mkono harakati za wapinzani kwa kificho na kumharibia Dr. Magufuli majukwaani kwa kutamka maneno ya kukwaza na kukera yanayochochea hasira za wananchi dhidi ya wagombea wa CCM wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani.
Wapo wajumbe waliosusa kutokana na kutotimiziwa matakwa yao hasa ya malipo kwa kila siku wanayoifanyia kazi. Wajumbe hao wamesema kuwa hawana muda wa kusubiri kulipwa baadaye kwakuwa uchaguzi ni bahati nasibu na lolote laweza kutokea. Wanasisitiza kulipwa marupurupu yao sasa kwa mujibu wa makubaliano ya kichama na kutoahidiwa kulipwa baada ya uchaguzi.
Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa hawapewi uzito na umaarufu kama ilivyotarajiwa. Wanamlaumu Dr. Magufuli na viongozi waandamizi chamani, kwa mfano, kumuamini sana Abdallah Bulembo ambaye hana hadhi kichama, kisera na kihela kupewa nafasi ya kutawala majukwaa kama afanyavyo sasa. Wanalalama kuwa watu maarufu wamewekwa kando na sasa wanaanza kuota utando.
Sasa timu imesambaratika. Dr. Magufuli yuko njiapanda kikampeni. Itambidi kupambana kiume ili kuendelea kujieleza mbele ya wananchi. Apambane kivyake sasa na watakaobaki naye!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Nachojua UKAWA inakaribia kusambaratika, inakwisha. Mbatia hoi......
Mwizi kukataa kujengwa kituo cha polisi hapo hakuna la ajabu.
fisim wanapoona mwenzao anataka kubadilika wanamzushia mengi
ili asiaminiwe na umma asije akavujisha siri.
Binafsi mtu akichukiwa na fisim mimi huyo naona ni mkombozi.
Ni sawa na majambazi,mwenzao akiwaaga kwamba anaenda kuokoka wapo
tayari kumuua maana wanaona atawaumbua.
Fikiria watu kama msukuma walivyokuwa wanamuunga mkono EL
kitendo cha EL kuama unaona wanamtukana matusi ya nguoni,
Je hao ndo wana nia ya kweli kuwatumikia watanzania?