Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imethibitisha kuwa haijapokea barua yoyote ya malalamiko kutoka kwa klabu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC wala NBC Championship hadi sasa. Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Habari wa Bodi hiyo, Karim Boimanda, ambaye amesema kuwa hata klabu ya Singida Black Stars, licha ya msemaji wao kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu malalamiko, bado hawajawasilisha barua rasmi kwa TPLB.
"Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) haijapokea barua yoyote kutoka kwa timu yoyote ile ya Ligi Kuu ya NBC wala NBC Championship na hata hao Singida Black Stars licha ya msemaji wao amezungumza na vyombo vya habari ila hatujapokea barua ya malalamiko kutoka kwao."
Kauli hiyo inakuja wakati ambapo kumekuwa na mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu baadhi ya Vilabu kutaka kususia mechi zilizosalia kwenye Ligi ya NBC kufuatia maamuzi na matukio yanayohusiana na mechi za ligi.