Time travel na ufunuo wa ufufuko

Kama imeshindikana kabisa kuficha kuwa asili ya mwanadamu ni Afrika. Basi huyu mwafrika kabeba siri kubwa kwenye uumbaji na kikomo cha kuwa... Sasa kuko wapi kushindwa kwake?
Unaposema asili ya Mwanadamu ni Afrika una maanisha nini ? Yaani unamzungumzia Adamu au nani ?

Na kipi kimekujulisha kwamba asili ya mwanadamu ni Afrika. ?
 
Hii definition kuhusu sayansi siyo kutoka kwa mzungu kweli?!!🤣🤣
mpk utafuniwe na mzungu ndo ufahamu wako ujazwe sivyo..? Mengine ukiyaona Kama mafumbo ukiyashindwa lala
 
mpk utafuniwe na mzungu ndo ufahamu wako ujazwe sivyo..? Mengine ukiyaona Kama mafumbo ukiyashindwa lala

Mkuu, Wazungu ndiyo elimu zao hizo, Hebu nitajie Mwana fizikia, mwana hisabati, mwana kemia Mswahili hata mmoja!!?--- a world recognisable one, labda kinjekitile ngwale aliyebadilisha risasi kuwa maji,🤣🤣🤣
 
Mzungu ndo anaubongo peke yake..?
 
Muda ninini? Linaweza kuwa swali gumu kujibika lakini unaweza kuelewa kupitia maelezo yafuatayo

Ni lazima kutambua ya kwamba kuna aina mbili za muda
1. Muda halisi unaosomeka na kuandikika kwa tarakimu
2. Muda usiosomeka wala kupimika... Muda was kufikirika ndani ya fikra

Muda unaosomeka na kuandikika kwa tarakimu hatuna muamana nao.... Upo hatuwezi kuubadili wala kuudhibiti... Muda huo upo tangu uumbaji.. Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuurekebisha, kuubadili wala kuutawala vyovyote vile.... Sisi ndio tunaufuta utakavyo hatuna milki nao.. Ulikuwepo... Upo na utakuwepo...

Muda usiosomeka wala kuandikika kwa tarakimu... Muda wa mawazoni na ndani ya fikra zetu.... Huu ni muda ndani yetu... Muda huu si wa wingi kwa maana ya wote bali ni muda wa umoja, muda wa kipekee unaotofautiana na kila mmoja wetu hapa...

Muda huu hujaribu tu kupimika kwa kumbukumbu ya mawazo na matendo yaliyopita, na mawazo ama matendo yajayo yasiyojulikana bado...
Tunakumbuka nyakati za furaha ama huzuni zilizopita huku tukitaraji mema ama mabaya ya nyakati zijazo.. Unaweza kuangalia nyuma ulikotoka kifikra na ukatamani kurudi huko.... Mawazo na fikra zako vikakubeba na kukupeleka huko mazima.... Yaani kimwili unaishi sasa katika wakati huu halisi lakini kifikra uko nyuma kabisa ya wakati mwaka juzi ama jana ama mwezi uliopita

Ukiwa katika hali hii unakuta muda halisi unakuwa na muingiliano na muda wa kufikirika... Muda uliokwisha kufa... Muingiliano wa muda na uumbaji... Dhana ya kuwa na kukoma kuwa....!

Nimeeleweka?
Daah,kaka mimi sijakuelewa kabisa labda ukinijibu hili swali naweza kuelewa.

Muda ili utambulike kunahitajika vitu gani ?
 
mkuu tunaongelea races mbili huyo nyani kafikaje lkn hata Hivyo ni unafahamu dhahiri kuwa nyani hawezi Kisha unauliza!!!

Sasa si ndio ujiulize kama suala ni Ubongo hata kuku anao, sasa vipi ashindwe kufanya mambo anayofanya binadamu??, hiyo ni hoja fikirishi kwako.

Yaani Mzungu anao ubongo Mwafrika naye anao ubongo, sasa inakuaje linapokuja suala la tafakuri tutafakari tofauti??, na mbaya wenzetu "in General" wanatafakari positively na sisi negatively!!, why is it so ??! 🤣🤣

Genetic make up za bongo zetu ni tofauti.
 
Unaposema asili ya Mwanadamu ni Afrika una maanisha nini ? Yaani unamzungumzia Adamu au nani ?

Na kipi kimekujulisha kwamba asili ya mwanadamu ni Afrika. ?

Zurri achana na uwongo wa watu wa mashariki ya kati kuwa Adam ni mtu kwanza

Quran yenyewe inatambua kuwa mtu wa kwanza ni mweusi na watu weusi wanatoka africa hivyo mshana yupo right
 
Zurri achana na uwongo wa watu wa mashariki ya kati kuwa Adam ni mtu kwanza

Quran yenyewe inatambua kuwa mtu wa kwanza ni mweusi na watu weusi wanatoka africa hivyo mshana yupo right

Unaweza kunionyesha kwenye Qur'aan inamtambua mtu gani wa kwanza nje ya Adamu ?
 
Unaposema asili ya Mwanadamu ni Afrika una maanisha nini ? Yaani unamzungumzia Adamu au nani ?

Na kipi kimekujulisha kwamba asili ya mwanadamu ni Afrika. ?
Nimerudi Zurri
Nisome tena kwa utulivu nilichoandika... Nimezungumzia asili mbili....
Asili ya kwanza ni kihistoria kwamba 'binadamu wa kwanza' (kwa tafsiri ya historia) mabaki yake yalipatikana Afrika tena Tanzania... Na hili halijawahi kukanushwa popote pale... Namaanisha kanusho rasmi la kimaandishi na ithibati
Asili ya pili ni ya kiimani.. Kuumbwa kwa ulimwengu na mwanadamu wa kwanza yaani Adam na hii iko mashariki ya kati
 
Hivi hili tamko "TAHAJUDI" ni tamko rasmi la Kiswahili au ? Msaada tafadhali,kama ni tamko rasmi ukinipa marejeo utakuwa umenisaidia sana.
Kwangu mimi na naamini na kwa wengine pia tahajudi ni tafsiri ya meditation (tafakuri jadidi)
 
Daah,kaka mimi sijakuelewa kabisa labda ukinijibu hili swali naweza kuelewa.

Muda ili utambulike kunahitajika vitu gani ?
Hili ni swali gumu kwakuwa hata ukiniuliza muda nini nitashindwa kukujibu... Lakini naweza kusema tu ya kwamba muda ni saa (sio ya kuvaa mkononi) muda ni dakika muda ni sekunde muda ni wakati na muda ni nyakati
 
Zurri achana na uwongo wa watu wa mashariki ya kati kuwa Adam ni mtu kwanza

Quran yenyewe inatambua kuwa mtu wa kwanza ni mweusi na watu weusi wanatoka africa hivyo mshana yupo right
Quran yenyewe inatambua kuwa mtu wa kwanza ni mweusi na watu weusi wanatoka africa
 
Nimerudi Zurri
Nisome tena kwa utulivu nilichoandika... Nimezungumzia asili mbili....
Asili ya kwanza ni kihistoria kwamba 'binadamu wa kwanza' (kwa tafsiri ya historia) mabaki yake yalipatikana Afrika tena Tanzania... Na hili halijawahi kukanushwa popote pale... Namaanisha kanusho rasmi la kimaandishi na ithibati
Asili ya pili ni ya kiimani.. Kuumbwa kwa ulimwengu na mwanadamu wa kwanza yaani Adam na hii iko mashariki ya kati
Una kubali kwamba hizi asili mbili zinakinzana japokuwa zote zina maana moja ?

Je kwanini zipingane ? Bila shaka kati ya hizi mbiki moja ni kweli.

Nataka tukae katika meza ya uchunguzi katika kauli yako ya kwanza ili tuone ukweli juu ya kauli hiyo ya kwanza. Pili,nakukumbusha tu,kutokuwepo kwa andiko rasmi kupinga jambo fulani haimaanishi yakuwa jambo hilo ni la kweli,yawezekana kutokana na uongo wake kuwa wazi zaidi watu wamelipuuza kwani kuwepo kwake kuna sawa na kutokuwepo kwake kwa hizo habari.

Nipo katika hiyo hiyo kauli ya kwanza,je ni nani wa kwanza kusema habari ya kuwa mwanadamu wa kwanza aliishi Tanzania ? Je walikuwa na uhakika gani kama kweli huyo ndio wa kwanza ? Je wana ripoti yoyote kutuonyesha ya kuwa walitembea dunia nzima na hawakufanikiwa kuona fuvu lolote zaidi ya hilo ? Au je walitembea dunia nzima na kukusanya mafuvu na kuyapima na kufika hitimisho ya kuwa fuvu liliopatikana Tanzania ndio la kweli ?

Pia,nina maswali kadhaa kuhusu kipimo chenyewe,hapa maswali haya nayaweka akiba,nitayauliza baada ya kujibiwa maswali hayo.
 
Back
Top Bottom