Tido Mhando atemwa TBC

Tido Mhando atemwa TBC

look at his friend jeff koinange..... Na vipindi vyake have you seen capital talk, three sides of the coin the big story....... Now thats what i call creativity...... This is results business kulingana na package anayopata, experience aliyonayo, na kule alikotoka he should have done better.... hata messi akimaliza msimu amefunga magoli mawili tu nadhani barcelona watamfukuza (still kwenye mfano ukimnunua messi hutegemei performance ya peter crouch) ukinunua ferrari hutegemei speed ya baiskeli.. thanks mkuu.

Even if ameitoa tbc from a to b he should have taken it to d....... Lets be optimistic and shoot for the stars....... Unajua tatizo sio kwamba we dont aim high but its because we dont aim high enough...... we are happy with mediocraty

mkuu kumbuka kuwa tbc is a state owned media and not private like itv and others where by you can decided to do what you feel its right.
 
..Utakumbuka hata Salva alikuwa safi kifikra na kiakili kabla hawaja m sandwich. Pia hata ukiangalia approach waliyoitumia kuwaficha Mwakyembe na Sitta.
Salva na kabila yake ndivyo walivyo!
 
Sidhani kama ni uchanguzi umemuondoa kama maoni ya wengi nafikiri naye alifanya ufisadi na wachina kwenye mkataba wa startimes na hii ndio imefanya aondolewe

Unajitahidi kuwa mbunifu!
 
What Tido did with TBC is just 1/5 of what was support to be done. Hatujazoea kuona vitu vyenye viwango ndo maana sifa kemkemu. Hope the next director work hard to compete with other East African News corp.

Brother that what I was trying to tell my fellow wanajamvi we are so happy with mediocracy... thats why hatuishi kupongezana.. hata mtu anapofanya kazi yake tunaona ametufanyia favour..... Wakuu hebu nipeni package ya huyu mtu ili kweli tuone kama alideliver kulingana na what he achieved..... Na hapa mtu hatuangalii ni pesa ngapi ameeingizia TBC because thats not what TBC is for (to make money)
 
mkuu kumbuka kuwa tbc is a state owned media and not private like itv and others where by you can decided to do what you feel its right.

Unajua as a good Director... inabidi uwe na msimamo sio kuendeshwa..... kuanzia mwanzo unawapa terms kwamba mimi nitaendesha kipindi as i see fit within reasonable limits... na wasikuendeshe endeshe... Sasa kama wanakwambia jinsi ya kufanya na wewe unafata orders EVEN I CAN FOLLOW ORDERS..... BUT IT DOES NOT MEAN AM FIT TO MANAGE TBC....
 
What Tido did with TBC is just 1/5 of what was support to be done. Hatujazoea kuona vitu vyenye viwango ndo maana sifa kemkemu. Hope the next director work hard to compete with other East African News corp.

Mkuu, you saying he achieved only 20% of what was support to be done. Mmmh...., what was he supposed to do for you to rate him that low - it doesnt ring the bell, frankly. I reckon he deserves a credit.

Pamoja na kwamba kuna mambo amefanya vibaya lakini kuna mambo mengi sana amefanya vizuri. Miaka minne ni kipindi kifupi kufanya mabadiliko kama aliyoyafanya pale TBC kuiwezesha kuwa kituo bora cha runinga kulinganisha na vituo vingine. Tukiacha kubezana mimi namuona jamaa ni CEO mwenye mafanikio.
 
BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.

Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.

“Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia," alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. "Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka.... ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.

“Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.’’

Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.

"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.

Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu.

"Tangazo linasema kuwa amefanya kazi na sisi kwa miaka minne na sasa mktaba wake umeisha na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Rugarabamu," alisema mmoja wa wafanyakazi wa TBC.
"Baadaye alitushukuru kwa ushirikiano wetu kazini na akatuambia tusubiri hadi hapo mkurugenzi mpya atakapotangazwa."

Mfanyakazi mwingine alisema kuwa walitarajia kuwa Mhando angetimuliwa mapema kabla ya uchaguzi kwa kuwa wanadai kuja kwake nchini kulitokana na uhusiano wake na kigogo mmoja wa CCM ambaye kwa sasa hayuko madarakani.

"Angetimuliwa hata kabla ya Desemba 15, lakini ikaonekana kuwa isingekuwa sahihi," alisema mfanyakazi huyo ambaye alieleza kuwa Mhando aliwasiliana pia kwa simu na mfanyakazi mmoja mmoja kumuelezea uamuzi huo wa serikali.

Habari za Tido kuondoka TBC zilianza kuvuma wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wakati iliposemekana kuwa alikuwa akipigana vijembe vya chinichini na vigogo wa CCM kutokana na vyombo hivyo vya umma kutangaza habari bila ya upendeleo.

Baadhi ya mambo yaliyoibua hisia kuwa mtendaji huyo wa shirika la umma angeondolewa ni msimamo wake wa kuendelea kurusha hewani kipindi cha "Jimbo kwa Jimbo" ambacho kilikutanisha wagombea ubunge wa vyama mbalimbali vya siasa kwenye mdahalo kuhusu maendeleo ya eneo lao.

Kipindi hicho kilichorushwa kwa wakati mmoja na vituo vya televisheni na redio kilianza kwa kushirikisha wagombea wote wa ubunge kwenye jimbo, lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akaandika waraka wa kuzuia wagombea wa CCM kushiriki kwenye mdahalo huo akidai kuwa chama hicho tawala kina njia zake za kufanya kampeni.

Pamoja na CCM kujitoa, TBC iliendelea kurusha vipindi hivyo hadi kumalizika kwa uchaguzi ambao uliisha kwa CCM kupoteza viti vingi Tanzania Bara, ikiwa ni mara ya kwanza tangu serikali iruhusu mfumo wa vyama vingi.

"Ilikuwa aondoke kabla kampeni hazijaanza ingawa mkataba wake ulikuwa umalizike Desemba 15. Lakini serikali ilikuwa inarekebisha mambo yake na kumtafuta mtu anayeweza kurithi nafasi yake," chanzo cha habari cha ndani serikalini kilidokeza.

Chanzo kingine alisema: "Kuna watu wanaajiriwa pale TBC ambao malipo yao yanayotokana na Saccos ya shirika hilo, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za serikali zinazotaka mwajiriwa alipwe na Hazina."
Jitihada za gazeti hili kumpata katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Seti Kamhanda hazikuzaa matunda.

Alipoulizwa endapo atakubali kurejee kwenye wadhifa huo ikitokea serikali ikamwita tena, Mhando alijibu: "Nitalazimika kuchukua muda zaidi kutafakari hilo kwa kina.

“Nitafanya maamuzi ya kazi ya kufanya kulingana na wakati utakavyokuwa, lakini itanichukua muda kidogo kutafakari hilo kwa kuwa nimefanya kazi mfululizo.’

Kuhusu utendaji wa shirika hilo, Tido alisema amefarijika kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya kiutendaji yaliyofikiwa.
“Nilikuwa na mipango mikakati mingi ya kuendeleza shirika hili hususani kulifanya lijiendeshe kwa kujitegemea bila ya kuhitaji ruzuku serikalini," alisema na kuendelea:

“Lakini nimefarijika vya kutosha na utendaji wangu na mafanikio yaliyofikiwa na TBC hadi wananchi kukiamini chombo hiki na ‘reaction’ imekuwa nzuri kutoka kwao na kwa vyama vya siasa.’’

Mbali na kurusha taarifa za kampeni katika njia iliyoonekana kuwa si ya upendeleo hata kwa chama tawala, TBC ilifanikiwa sana katika urushaji wa moja kwa moja wa matangazo ya mechi za mpira wa miguu na matukio makubwa ya kisiasa na kijamii.

Mechi za michuano mbalimbali ya kimataifa na ya ndani, urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, urushaji wa moja kwa moja wa matukio makubwa na staili ya utangazaji ulilifanya shirika hilo kuwa na mvuto mpya na hivyo kuweza kupambana na vituo vingine vya redio na televisheni vya kampuni binafsi.
 
Tena ana bahati kwa kupewa barua baada ya mkataba wake kwisha, kwani viongozi wa nchi hii hufukuzwa kazi kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku.

INAONYESHA HAKUMTUMIKIA VIZURI KAISARI.

Karibu Mtaani Bro kazi za utaalam wako siku hizi ni za kumwaga.LAKINI bora ungeanzisha na kusimamia REDIO Anglican Dar es salaam.
 
Wakati mwingine nawashangaa wana JF, mpaka jana tu bwana huyu alikuwa akielezwa kuwa ni kibaraka, lakini leo kwa kupotoshwa kidogo tu na gazeti la Mtanzamia, ambalo mmiliki wake ndiye kinara wa ufisadi hapa nchini,kila mtu anamtaja Tido kuwa shujaa. Ukweli ulivyo ni kwamba katika uhai wake kama Mkugenzi mkuu wa TBC Tindo alikuwa amelemewa na mvuto toka pande mbili; upande wa kwanza ni kutoka kwa watawala walikuwa wanataka kutumia chombo hicho kwa maslahi yao wenyewe, na kwa upande mwingineTindo alikuwa akisutwa na dhamira yake; kuligana na taaluma yake, alijua fika anaeajibika kuendesha chombo hicho siyo kwa maslahi ya kikundi bali kwa umma wote wa watanzania. Katika utendaji wake Tindo hakuweza kukidhi matakwa ya upande wowote katika pande zote mbili hasimu. Hivyo wakati huu ambao Tindo anaondoka TBC ameandamwa na lawama nyingi kutoka pande hizo mbili.
 
Mkuu, you saying he achieved only 20% of what was support to be done. Mmmh...., what was he supposed to do for you to rate him that low - it doesnt ring the bell, frankly. I reckon he deserves a credit.

tatizo ni comparison....... kutokana na uzoefu wake mkubwa.... na kutokana na kwamba TBC ni kituo cha taifa ingebidi tufanye comparison sio na ITV na Channel 10..... (Hapana) inabidi tufanye comparizon na the likes of KBC, CNN etc.... Si kwamba hana uwezo am sure he has got it in Him.. Kweli uenda akawa better kulingana na wengine tulionao lakini inabidi kama nchi tuongeze kipimo cha hawa watu
 
nimesoma kwenye gazeti la Mtanzania la leo limenitia kichefuchefu ati Tido ameondolewa kwakuwa alikuwa anakipendelea chama cha Chadema!!! ni uzushi mkubwa huu
 
Tido uliboresha sana sekta ya utangazaji pale TBC 1 hususani kwenye mambo ya luninga nakupa pole sana lakini ulipotufikisha hapa tulipo kwenye sekta ya habari kweli umefanya mengi na ya kuigwa, wewe ni mfano sijui kwahuyo atakaye vaa viatu vyako ulivyoacha! sintapenda kuingilia na wala kujua ni nini kilichowasibu kukuandikia barua ya kukuachisha japokua unadai kuachishwa kwako kuna utata! Nakuomba kaa chini utafakari kama kweli kulikua na zengwe au mkono wa mtu. sisi tuliokua tunafuatilia vipindi pale TBC 1 hakika popote pale utakapokwenda tunaomba utupe taarifa zako ili tuweze kukufuatilia tena! Mbona pale CNN kulikua na mtu kama JEFF KOINANGE lakini naye pia alipata kama yaliyokupata? Pole sana kaka Tido ndio ukubwa huo.
 
Jamani naomba tuelewe kuwa TIDO alikuwa na Mkataba umeisha december 13,kwaiyo basi serkali imeamua kutoengezea mkataba , kwan amukumbuki Pro. BAREGU pale mlimani walimwambiaje Ndo hivyo acha aje mwingine
 
Back
Top Bottom