Tibaijuka akataa kupokea shilingi 200 millioni

Tibaijuka akataa kupokea shilingi 200 millioni

Mbona ile "pesa ya mboga" toka kwa Escrow aliipokea? ...... Mwepesi kweli kusahau!!!!!
 
By Raymond Kaminyoge, Mwananchi

Dar es Salaam. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka amesema amepata tuzo nchini Marekani ikiwa ni kuthamini mchango wake akiwa Umoja wa Mataifa lakini akakataa kuchukua fedha dola 100,000( zaidi ya Sh 200 milioni) ambazo huambatana na tuzo hiyo.

Alisema alikataa kupokea fedha hizo kwa sababu maadili ya nchi yetu hayaruhusu kupokea zawadi kama hiyo.

Alisema lakini aliwaeleza kwamba katika mkoa anakotoka kumetokea tetemeko la ardhi na kuna maafa.

Alisema wao wataamua cha kufanya lakini yeye binafsi amekataa kupokea fedha hizo.

Proof atakuwa na uelewa mdogo wa nini maana ya zawadi halali na zawadi zisizo halali kama escrow...
 
Ningekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu CDM ningeamuru mamluki wote waliohamia wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015 waondolewe kwenye Chama sababu walikuja kwenye Chama kwa masilahi yao binafsi tu na hawana msaada wowote!
 
Fedha halali za Tuzo anakataa, Fedha za Wizi anapokea!!! Huyu ni teja wa Ufisadi hata Mshahara wake halali huenda akaiba ndio afurahi
 
Mwenyekiti hana Mamlaka ya kumvua uanachama, msifananishe CCM na magenge yenu ya Kisiasa!
 
Angempa mama Lwakatale alipie faini wasiojiweza ili kupunguza msongamno magerezani.
 
Kwa maadili ya utumishi asingekataa - ila angepokea kisha zawadi hiyo angeikabidhi serikalini na kukatiwa ERV kisha fedha zingeingizwa kwenye hazina ya serikali.
Huo ndio ukweli.
 
Hawa Ma Prof wa inji hii ni tatizo ,huyu mama haiba yake kimataifa imeshuka sana baada ya ile mambo ya ESCROW.
HUYU WA KIMATAIFA ANA UZOEFU ANAJUA NDEGE ZA MAREKANI HAZIRUHUSU SANDARUSI ANGEKWENDA HUKO BAADA YA NDEGE ZA MAGBOMBIER KUANZA TRIP ZA USA
 
Amezoea vya kunyonga,kama ESCROW,hivyo vya kuchinja huwatoa busara viongozi wetu wengi.
 
Baada ya Mama Tibaijuka kutwaa tuzo na kukataa kuubeba mpunga uliokuwa umeandamana na tuzo hiyo (zaidi ya mil 200) kutokana na uwoga wake wa kwamba yatatokea kama yale ya Escrow(Ubinafsi)..ningekuwa mm ndo yeye ningefanya yafuatayo...
1. Ningezichukua hizo ela na kuwapelekea waathirika wa tetemeko.
2. Ningezichukua na kuwapa vijana wakiwemo wahitimu ambao wanahangaika kutokana na either kukosa ajira or kukosa mitaji.
3. Ningezichukua hzo ela na kujenga madarasa au kununua madawati ili wanafunzi wanaokaa chini au kukosa madarasa wapate ahueni
Nashauri watu jamani tuache ubinafsi...unakataa mil 200 wakat watu ata 1000 ya chai hawana....inauma kwa kweli
 
Kitendo cha Serikali kutafuta pesa kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko wa mkoa wa Kagera huku jimbo la Buleba likiwa ni sehemu ya mkoa wa Kagera Mbunge wake akiwa ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya kimataifa ya maswala ya uongozi na KUKATAA TAKRIBANI T..SH 200 MIL KAMA KIAMBATA CHA TUZO.NI JAMBO LA KUSTAJABISHA KWA KIONGOZI MKUU KAMA HUYU ANAYETOKA KATIKA ENEO LILILOATHIRIKA NA JANGA HILI AMBAPO BADO JUHUDI ZA KUKUSANYA MICHANGO ZINAENDELEA FANYIKA. LAITI KAMA NINGEKUWA NI MWENYEKITI WA CCM NINGEMVUA UANACHAMA KAMA HATUA MUHIMU YA KUELEKEA MVUA UBUNGE WAKE
sorry unaweza kusema sababu za kukataa hizi pesa?!
 
Mi ninashangazwa na hatua aliyochukua kukataa hiyo pesa,maelezo aliyotoa na kiwango cha kuelimika kwake na majanga yaliyo tusibu kwa kweli sijamuelewa jamani.
 
Back
Top Bottom