Prof. Tibaijuka akanusha kupokea Bilion 1.6 kutoka kwa James Rugemarila

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,203
12,904
Prof Anna Tibaijuka Amesema Tetesi za Kupokea kiasi cha Pesa Bilioni 1.6 Kutoka kwa Mfanyabiashara James Rugemarila ilikuwa Uongo na ndio maana kesi imeshindwa kusogea mbele kwa kuwa hakuna Mashahidi wa kwenda kuzungumza Mahakamani

Tibaijuka, Waziri wa zamani wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwenye mahojiano ambayo yamefanywa na @charles_william 2 pamoja na @officialzungu_ katika kituo cha Wasafi Tv.

Prof Anna Tibaijuka amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuachia huru mfanyabiashara James Rugemalila.

======
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.

Profesa Tibaijuka amesema hayo leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 kupitia Kituo cha televisheni cha Azam UTV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha fedha hizo walizopokea ili kumsaidia mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

“Suala hili sio langu binafsi maana fedha hizi ni za shule, mwenyekiti wangu (wenyekiti wa bodi), Salmon Odunga na mwenyekiti wa wazazi, Dk Kiharuzi wamekaa kwenye kikao wakaamua fedha zirudi."

"Nashukuru kwa msimamo huo kwa kuwa ndio msimamo wangu pia kwamba kama itasaidia, tunashukuru Mungu," amesema Profesa Tibaijuka.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa, Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

“Fedha zenyewe zilikwenda kulipa deni la mkopo ambao tulijenga bweni lakini taasisi kama hii inapoamua kurejesha fedha zitatafutwa na kurejeshwa” amesema.

Amesema kutokana na Rais wa Tanzania, John Magufuli kushauri watuhumiwa wa uhujumi uchumi waandike barua kukiri na kurejesha fedha na mali, wao watarejesha kiasi walichopewa na Rugemarila.

“Msamaha wa Rais unapotoka ni fursa adimu, sasa fursa ukiichezea utabaki kujuta mwenyewe, kwa upande wangu na shule, sisi tunashughulika na ule mchango tulioupokea tunaurudisha mezani” amesema profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka alipokea mchango wa Sh1.617 bilioni kutoka kwa Rugemarila ambazo amesema zilitumika kwa ajili kulipa mkopo waliokuwa wakidaiwa katika Bank M.

Rugemarila anakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
Mbunge wa Muleba mkoani Kagera Prof Tibaijuka amerudisha fedha alizopewa na mzee Rugemalira ili kuondoa sintofahamu iliyokuwepo kwamba fedha zile zilitoka katika account ya Escrow.

Prof Tibaijuka ameitikia wito wa Rais Magufuli kuwataka waliofisadi fedha za umma kukiri na kuzirejesha.

-------
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.

Profesa Tibaijuka amesema hayo leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 kupitia Kituo cha televisheni cha Azam UTV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha fedha hizo walizopokea ili kumsaidia mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

“Suala hili sio langu binafsi maana fedha hizi ni za shule, mwenyekiti wangu (wenyekiti wa bodi), Salmon Odunga na mwenyekiti wa wazazi, Dk Kiharuzi wamekaa kwenye kikao wakaamua fedha zirudi."

"Nashukuru kwa msimamo huo kwa kuwa ndio msimamo wangu pia kwamba kama itasaidia, tunashukuru Mungu," amesema Profesa Tibaijuka.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa, Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

“Fedha zenyewe zilikwenda kulipa deni la mkopo ambao tulijenga bweni lakini taasisi kama hii inapoamua kurejesha fedha zitatafutwa na kurejeshwa” amesema.

Amesema kutokana na Rais wa Tanzania, John Magufuli kushauri watuhumiwa wa uhujumi uchumi waandike barua kukiri na kurejesha fedha na mali, wao watarejesha kiasi walichopewa na Rugemarila.

“Msamaha wa Rais unapotoka ni fursa adimu, sasa fursa ukiichezea utabaki kujuta mwenyewe, kwa upande wangu na shule, sisi tunashughulika na ule mchango tulioupokea tunaurudisha mezani” amesema profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka alipokea mchango wa Sh1.617 bilioni kutoka kwa Rugemarila ambazo amesema zilitumika kwa ajili kulipa mkopo waliokuwa wakidaiwa katika Bank M.

Rugemarila anakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

-Mwananchi-
 
Ushenzi mtupu yaani wewe muhaya upo hapa kumsafisha huyo fisadi?
Uhaya wangu sio wa unafiki, mi ninereport kilicho zungumzwa na Tibaijuka, sijaongeza wala kupunguza kile kilichoreport kwenye page wa Wasafi tv kuoitia account yao ya Insta na wajati mwingine ujue tu mtu anaweza kureport kutokana kuona hiyo ya habari kwake ni mshangao! Sio lazima aipende.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ufisadi mtupu na huyo mama hakuna tena mtu wa kumuamini kabisa.

Kwa kujua hilo ndiyo maana amesoma alama za nyakati kutogombea tena ubunge maana wasinge penda kusikia hata kampeini zake.
 
Angalau huyo ni Mwanamke inaeleweka kibaologia hata socially hivyo anasameheka, shida ni Wanaume ambao wanajipendekeza na hata kuuza utu wao , mambo yanaweza geuka kesho Madame hayupo anakuja mwingine huwezi jua, Mwanaume simamia unachokiamini usiwekeze kwa binadamu, …
 
Back
Top Bottom