Tiba za asili: Manufaa ya asali na mdalasini

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,808
2,000
Wakuu nimekutana na makala hii nikaona nianzishe mada hapa ili tuweze kujadiliana na wataalam wetu na watufahamishe ukweli wake na uwongo wake au kutupa ushauri zaidi ya huu niuonao katika mada hii. Nimejaribu kwa kadiri ya uwezo wangu kuirekebisha kiswahili chake lakini nahisi hakiko sawa bado lakini naamini ujumbe unafika.

Leo naanza na manufaa ya asali na mdarasini:

MDALASINI NA ASALI

Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.

Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

Kama ifuatayo:
1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja 'cha chai' cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. Kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.

Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER

SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.

7. Helemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.

Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann.

Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.

8. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.

9. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa angalau vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}.

Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.

Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,808
2,000
11. Esidi/Gesi-Co2. HCO3. HCl.
Kula asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi/asidi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko India na Japan.

12.Ugonjwa wa Moyo {HEART DISEASE}
Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa.

Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko kimoja {cha mezani} cha mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa 74% ya wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja ulionyesha.

13. Shinikizo la damu {HIGH BLOOD PRESSURE}
Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali ilyochanganywa na mdalasini.

Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha ukawaida na wote 137 waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya wiki chache za tiba hii ya ajabu.

14.Kinga ya mwili {IMMUNE SYSTEM}
Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja - wataalamu wanasema.

Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya vitamini{vivurutubisho}na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea {virus} na {bacteria}.

15.Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}
Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.

Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia ya kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao za kufanya mapenzi.

16.Kutokuchaguliwa kwa chakula {INDIGESTION}
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo{kula chakula} huondoa kiungulia na wataalamu wanasema kwamba asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula tumboni na mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.

17.Flu {INFLUENZA}
Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vairasi {vimelea} waletayo Flu.

18.Umri wa kuishi {LONGERVITY}
Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vine{vikubwa} vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.

19.Chunusi {PIMPLES}
Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.

Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.

20.Kuumwa na wadudu {kwa washawasha} wenye sumu
Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe vinatoweka.

21.Madhara ya ngozi {INFECTIONS}
Fanya kama ilivyoelekezwa hapo juu. Rudia kufanya hivyo hadi hali itakapokwisha.

22.Kupungua kwa uzito
Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu. Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala.

Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.

23.Sarakani {CANCER}
Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu sarakani.

Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa sarakani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu kupata nafuu kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi".anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na milo ya kawaida".

24.Uchovu {FATIGUE}
Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu, wataalamu wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji, nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri wakati nishati {nguvu}inapoanza kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa. "katika wiki moja hii itajionyesha".

25.Kuvimba Nyayo {SORE FEET}
Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu}


 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,482
2,000
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat Sawdaa-1 (haba Soda - Chembe Nyeusi)

Al-Bukhaariy anasimulia kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema.

((Habbat-Sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti)).

Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.

Kwa faida ya Afya kwa ujumla:
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.

Vipele (chunusi) Na Ngozi:
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.

Upara (Alopeshia):
Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.

Pumu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):
Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Mwiba Wa Nyuki Na Nyigu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kibofu cha Mkojo/Figo:
Kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya Habbat-Sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi. Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko unaweza kukaa kwa siku 15 na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.

Jiwe La Figo:
Kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyochanganwa pamoja na gilasi (bilauri) moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Changanya vitunguu saumu pamoja na asali na Habbat-Sawdaa. Kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo kula limau (bila ya kumenywa). Rudia haya kwa wiki moja Insha-Allah jiwe litaondoka.

Maathiriko Ya Figo:
Changanya baadhi ya Habbat-Sawdaa pamoja na mafuta ya alizeti. Chukua mchanganyiko na weka katika sehemu ambapo figo limeathirika. Kunywa kijiko cha Habbat-Sawdaa asubuhi. Rudia haya kwa muda wa wiki moja Insha-Allah maathiriko yatatibika.

Mafua:
Chukua mbegu za Habbat-Sawdaa 21, ziweke katika kitambaa na roweka usiku. Tumia kama matone kwenye pua siku ya pili nusa poda ya Habbat-Sawdaa iliyomo katika kitambaa.

Kikohozi:
Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya Habbat-Sawdaa kwenye kahawa au chai.

Bawasiri:
Kula unga wa Habbat-Sawdaa pamoja na maji.

Shinikizo la damu (high blood pressure):
Changanya kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, kijiko kimoja cha asali safi na kitunguu kiasi kidogo. Chukua mchanganyo kabla ya kufungua kinywa kwa siku ishirini.

Uwasho Na Maumivu Ya Jino Na Ufizi:
Chemsha Habbat-Sawdaa katika siki na itumie kwa kusukutulia meno na ufizi. Na jikinge kutumia dawa za msuwaki za kibiashara na tumia dawa za msuwaki ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye nyuzi za mboga za mti wa siwak ambao kwa karne ulikuwa unatumiwa na Wahindi, Waafrika na Waarabu, ni msuwaki wa kiasili.

Kumbukumbu (memory):
Kunywa kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa na changanya na asali mara mbili kwa siku.

Utaratibu Wa Ulinzi Wa Mwili:
Kula kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa na asali mchana na usiku Kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu.

Jaundice:
Tumia Habbat-Sawdaa pamoja na maziwa.

Maumivu Sugu ya kichwa (Maumivu ya kichwa ya upande mmoja, maumivu ya kichwa):
Kaanga Habbat-Sawdaa na iweke katika kitambaa cha pamba, funga au weka tu kitambaa katika kikomo (kipaji cha uso). Roweka Habbat-Sawdaa ndani ya siki wakati wa usiku, siku ya pili ivuruge kufanya unga. Ingiza katika pua halafu vuta pumzi.

Ngozi kavu:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Upepo:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Minyoo:
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,482
2,000
Asidi (Acidness)
Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.

Uvimbe Wa Tumbo
Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.

Maradhi Ya Macho
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope, atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti.

Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Kichocho (Bilharziasis)
Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na nishati.

Kutoa Wadudu Tumboni
Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.

Utasa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah itakuwa kheri.

Tezikibofu (Prostate gland)
Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na atajipaka chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.

Pumu (Asthma)
Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.

Kidonda
Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.

Saratani (Cancer)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.

Nguvu Za Kiume
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja achanganye (apige) ndani ya mayai saba ya kienyeji; atafanya hivyo siku baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi hata kama ana miaka 120 atapata nguvu za barobaro!

Udhaifu kwa Ujumla
Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.

Kuleta Hamu Ya Kula
Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.

Kutibu Ulegevu Na Uvivu
Atakunywa- kabla ya kula – juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo kwa muda wa siku kumi. Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.

Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi
Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi.
 

KANUYA

New Member
Apr 5, 2009
4
0
Ahsanteni sana kwa taarifa na elimu nzuri kuhusu Habbat Sawdaa! Je hapa Tanzania inapatikana wapi?
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,182
1,500
Naomba tutumie huu uzi kutaja tiba za asili tunazozijua kwani ni wazi kuwa yapo magonjwa yasiyo na tiba muafaka hospitalini lakini kuna watu wanajua tiba za asili.

Lengo ni kuweka kumbukumbu kwani maandishi uliyoweka hapa yanaweza kuja kuwa na manufaa miaka hata 50 ijayo, huwezi kujua.

Najua wengi hatujui majina kwa lugha ya kiswahili, au kisayansi ya mimea mingi tunayoijua ni tiba. Naomba tu uitaje kwa jina la lugha unayoifahamu, inawezekana akatokea mdau anajua jina la mmea huo kwa lugha nyingine tunayoweza kuielewa wengi. Kama unaweza weka picha kabisa ya mmea au tiba unayoongelea.

Binafsi nitaanza na kutaja mimea ya tiba zifuatazo katika posts zitakazofuata, na nitajitahidi kuweka picha pale ninapoweza. Pia nitaandika "tiba" au "tambiko" kwa mujibu wa wazee wangu niliobahatika kukua nao (ingawa kwa sasa sifanyi hizo), kwa lengo tu la kuweka kumbukumbu kwani inawezekana miaka mingi ijayo watoto au wajukuu zetu wakaja kusoma huu uzi katika kujifunza mila na desturi zao.
Baadhi ya tiba nitakazotaja hapa ni zile ambazo niliwahi kuona wazee wangu wakizitumia, zile nilizowahi kutumia mwenyewe, zile nilizowahi kuhadithiwa, na hata zile nilizosoma sehemu mbali mbali ikiwemo humu JF...

Baadhi ya nitakazoweka kwenye posts zinazofuata ni;

1. Mimea inayotibu maumivu ya tumbo (la kuharisha)
2. Mimea inayotibu maumivu ya tumbo (sio la kuharisha)
3. Mimea inayotibu vidonda
4. Mimea inayotibu kiungulia
5. Mmea unaotibu athma (mara moja tu)
6. Mimea inayoongeza nguvu za kiume
7. Mmea unaotibu maumivu ya meno (pamoja na kutoboka)
8. Tiba ya maumivu ya sikio (sio mmea)
9. Mimea inayofunga kizazi kwa wanawake
10. Mmea unaotibu jipu (bila kupasuliwa)
11. Dawa ya kusaidia kutoa kondo la nyuma la ng'ombe
12. Mmea unaotibu minyoo (kwa binadamu na mifugo)
13. Mmea unaotibu mastitis kwa ng'ombe
14. Kadhalika

Pia zipo tiba vyingine ambazo zinahusiana na imani ambazo nitazitaja baade kwa mfano
1. Jinsi ya kumkinga au kumtibu mtoto mchanga dhidi ya "kijicho"
2. Jinsi ya kujizuia "kufanyiwa mchezo" kwa chakula unachokula hadharani au kwenye sherehe
3. Jinsi ya kuzuia mvua isinyeshe siku kuna tukia kama sherehe au mkutano
4. Tambiko ya kuomba mvua
5. Kadhalika

Nawaombeni wanaJF mposti kwenye huu uzi tiba zozote za asili mnazozijua au mlizowahi kusikia. Huwezi jua miaka mingi ijayo akatokea kijana wetu mtafiti akasoma bandiko lako, akafanya utafiti akaibuka na dawa matata ambapo utakuwa umesaidia vizazi na vizazi...
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,713
1,225
Baadhi ya tambiko kweli unaweza kuzichukulia kuwa ni ushirikina hasa kwa wale tunaoamini katika hizi dini za kigeni. But ndiyo historia yetu. Kwa hiyo mimea sio ushirikina...
Ivi unataka kuniambia hiyo mimea inatumika yenyewe tu bila uwepo wa nguvu yoyote ya kiza?
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,182
1,500
Embu tupe somo basi ili tuende sambamba na lengo la sired!

1 ni mimea gani inatumika ili kuzuia mvua?

2 unafanyaje (procedures) kwa hiyo mimea na kuweza kuizuia mvua?
Hahaha. .. mkuu hizo za kuzuia mvua nimesema ni imani, na hizo ndio tambiko. Nitaziongelea baadae sana kwenye huu uzi. Kwa sasa najiandaa kuongelea mimea ya kawaida inayotibu magonjwa kwenye miili ya binadamu/wanyama...
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,713
1,225
Hahaha. .. mkuu hizo za kuzuia mvua nimesema ni imani, na hizo ndio tambiko. Nitaziongelea baadae sana kwenye huu uzi. Kwa sasa najiandaa kuongelea mimea ya kawaida inayotibu magonjwa kwenye miili ya binadamu/wanyama...
Wakati unaelezea namna ya kuzuia mvua, usiache kunitag!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom