Ufanisi wa manjano na asali katika kutuliza kikohozi

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
291
Manjano na asali imekuwa tiba iliyokuwa ikinisaidia sana katika makuzi yangu endapo nilikuwa nasumbuliwa na kikohozi.

Unachanganya manjano kwenye asali, pia siku zingine unakamulia maji maji ya Tangawizi bila kuweka na machicha yake kwa sababu inaweza kusabibisha karahaa kwenye koo.

Mara zingine nilitengeneza kwa size ya kijiko kikubwa cha kula au kwenye kicontainer na kuhifadhi kwenye fridge ili isiharibike.

Inasaidia kulainisha koo na kutuliza kikohozi pia.
 
Back
Top Bottom