Tiba za asili: Manufaa ya asali na mdalasini

EP PRO

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
7,593
2,000
hebu somo lianze basi
tuielew dunia yetu vizur, n plz kuna baadhi ya mimea hufahamika kwa majina tofauti tofaut
kutokan na jamii zilivyo so ingekuwa vema ungekuwa waweka na picha ya mmea ili ujumbe ufike vizuri kabisa
 

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,250
Hiyo namba mbili na namba kumi naijua hua inaota sana ovyo majumbani au shambani au porini ila sijui majina yake kwa lugha yoyote ile hata kiswahili.
 

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,250
Ivi unataka kuniambia hiyo mimea inatumika yenyewe tu bila uwepo wa nguvu yoyote ya kiza?
Karibia magonjwa yote yanatibika na mimea na mboga mboga za nyumbani bila ushirikina na ukapona.... kwani majani ya mpera unatambikia mpk unywe uzuie kuharisha..?
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,713
1,225
Karibia magonjwa yote yanatibika na mimea na mboga mboga za nyumbani bila ushirikina na ukapona.... kwani majani ya mpera unatambikia mpk unywe uzuie kuharisha..?
qn of sheba bhana!
Dawa zitumikazo kuponya watu usitake kulinganisha na hiyo mimea ya kuzuia mvua!

Kuna kitu kinaitwa 'connection', Ukiugua, hata kama unadawa millioni 100 hauwezi kupona unless unywe or ule hizo dawa! Kitendo cha wewe kula/kupakaa (hata kunusa) itapelekea unyonywaji wa dawa kwenda sehemu iliyokusudiwa! Hiyo connection baina ya wewe mgonjwa + dawa + eneo husika (unapoumwa)!

Embu nipe connection ya mimea utakayotengeneza huku chini na kuzuia mvua iliyoko juu.

Najua watu wanauwezo wa kuzuia mvua. Issue ni kwamba hawatumii mimea pekeyake ili kufanikisha hilo!
...
Sidhani kama tunaelewana hapa!
 

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,250
qn of sheba bhana!
Dawa zitumikazo kuponya watu usitake kulinganisha na hiyo mimea ya kuzuia mvua!

Kuna kitu kinaitwa 'connection', Ukiugua, hata kama unadawa millioni 100 hauwezi kupona unless unywe or ule hizo dawa! Kitendo cha wewe kula/kupakaa (hata kunusa) itapelekea unyonywaji wa dawa kwenda sehemu iliyokusudiwa! Hiyo connection baina ya wewe mgonjwa + dawa + eneo husika (unapoumwa)!

Embu nipe connection ya mimea utakayotengeneza huku chini na kuzuia mvua iliyoko juu.

Najua watu wanauwezo wa kuzuia mvua. Issue ni kwamba hawatumii mimea pekeyake ili kufanikisha hilo!
...
Sidhani kama tunaelewana hapa!
Ok hapo kwenye mvua nitaamini kunaushirikina ila kutibu magonjwa mengine kama ini.. tumbo... jipu n.k hayo magonjwa yanatibika tu kwa mitishamba au matunda na mboga bila hata matambiko yoyote
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,713
1,225
Ok hapo kwenye mvua nitaamini kunaushirikina ila kutibu magonjwa mengine kama ini.. tumbo... jipu n.k hayo magonjwa yanatibika tu kwa mitishamba au matunda na mboga bila hata matambiko yoyote
qn of sheba thanks kwa kunielewa!

Tuko amewamislead wengi ktk post yangu ya kwanza (post #2 ) alichokifanya ni kuondoa nilivyomreply with quote na kumuekea maandishi mekundu hapo kwenye mimea ya kuzuia mvua!

("..3. Jinsi ya kuzuia mvua
isinyeshe siku kuna tukia kama sherehe au mkutano..."
)

Na sjui kwanini ameamua kunifanyia hivyo! (amefanya post yangu isieleweke naongelea nini!)

Tuko you have prima facie case!
 

Maarko

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,158
2,000
Kuna mti mmoja mdogo kimo cha mbuzi inatibu kidonda kipya na kinapona kabisa kinaitwa "Kibaranungu"kichagga.
 

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
14,927
2,000
Lengo kubwa la Uzi huu tutakuwa tunaulizana maswali yanayohusu magongwa na tiba zake za asili.

Napenda kufafanua kuwa maelezo yangu kuhusu dawa asilia hayana uhusiano wowote na masuala ya tiba yanayoshughulikiwa na waganga wa kienyeji wanaotumia mazingaombwe, ushirikina, mizimu, mashetani na mambo kama hayo.

Hapa nina maana ya tiba inayotumia dawa za asili kutokana na majani, magome ya miti, mizizi, matunda kwa ajili ya kunywa, kupaka, kuchua na hata kunusa.

Tiba ya kutumia dawa asilia ilikuwapo kabla ya ujio wa wakoloni. Wakoloni walipoingia nchini walileta dawa za vigonge, vimiminika na pia matumizi ya sindano. Baada ya dawa za kigeni kuingia nchini kwa tiba kwa magonjwa mbalimbali, umeibuka mtindo hivi sasa wa ama kudharau au kupuuza tiba asilia.

Vilevile ulaji wa vyakula vya asili ulipungua na sehemu nyingine uliachwa kabisa. Kutokula vyakula vya asili umeshika kasi hasa kwa wasomi na wenye hali nzuri kiuchumi. Maana yangu ni kuwa makundi haya yameacha kutumia dawa zinazotengenezwa kiasili kutokana wakiamini kuwa hazifai kwani zimepitwa na wakati.

Mawazo ya aina hii yamepandikizwa katika akili zetu na wageni waliokuwa na dhana kuwa kitu chochote cha kiasili ni dhaifu au hakifai. Nakumbuka tulikuwa na dawa ya kulisafisha tumbo ambayo ikinywewa inaondoa uchafu ulioganda katika ukuta wa tumbo na pia utumbo mpana. Dawa hii ilitokana na mbegu za mmea uliojulikana kama ‘ngetsi'. Baada ya siku moja mtu hujisikia mwepesi na kuwa na hamu ya kula. Walipokuja Wazungu walituletea dawa ya ‘Epsom Salt'.

Dawa hii ilifanya kazi kama ‘ngetsi' lakini ilikuwa na madhara hasa kwa utumbo mwembamba. Kwenye utumbo mwembembe kuna vimelea vinavyosaidia kufyonza virutubisho na kuviingiza katika mfumo a damu mwilini kwa lugha ya kigeni vinaitwa ‘villi' (umoja ni villius).

Kama mtu akitumia ‘Epsom Salt', vimelea hivi hukwanguka na hivyo mwili kushindwa kupata virutubisho kwenye chakula na kuviingiza mwilini. Mwili hudhoofika kwa kukosa virutubisho muhimu kwa afya.

Mawazo finyu tuliyopata ni kwamba tiba asilia ni mbaya. Imetufanya tujenge dhana ya kutothamini kilicho chetu kwa kuthamini kila kinachotoka nje.

Na ni vzr kama kuna mtu alishawai kuumwa ugonjwa wowote akatumia dawa Fran za mitishamba akapoana atuambie ili na sie tupate elimika

Nawasilisha kwa wazee wa JF
Mzizi Mkavu, mshana jr, Pasco, king kong The Boss @Nyan Ngabu

Na wadau wengine wengi tu mnakaribishwa
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,772
2,000
Nahusika sana hapa na asante kwa mada nzuri nitakuwepo sana hapa[MENTION][/MENTION]
 

Step by step

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
1,053
2,000
Shukrani sana kwa uzi wenye manufaa. Naomba kuwa wa kwanza kuleta tatizo langu.
Mimi ni jinsia ME,
1. Ishu ni kuwa nakosa kabisa hamu ya kula hasa breakfast. Nikiamka asubuhi siwezi kula kitu na nikijilazimisha najiskia kutapika ila nikikaa cjaa mpaka mchana hamu ya kula inakuja napiga msosi vizuri tu.
2. nikiwa safarini siwezi kula tumbo linachafuka mpaka nifike nikae hata siku mbili ndo narudia hamu ya kula ya kawaida.
3. Naweza kuwa vizuri tu ila mtu akiniletea taarifa yeyote ya kushtua tumbo linavurugika naweza tapika na hali inabadilika kabisa.
Wataalam wa tiba mbadala hebu tieni neno hapo yaweza kuwa nini
 

Kisima

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
3,825
2,000
Asante mleta mada.
Ni kweli kabisa umagharibi mwingi umewafanya Waafrika wengi kudharau tiba za asili.
Wamesahau kwamba kuna magonjwa nengine wazungu mpaka hivi leo wamefeli kupata ufumbuzi wa tiba halisi.

Moja ya ugonjwa ambao hautibiki kwa dawa za kizungu ni PUMU ugonjwa ambao ulinitesa sana mimi ila nikatafuta dawa ikaniponya kabisa kabisa na ninaendelea kusaidia na wengine.

Kwa wewe mwenye tatizo hilo wala usiwaze mara mbili nitafte 0785018611 upate kupona.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom