Home remedy ilivyonitibu Viral Infection!!

Beige

Senior Member
Dec 7, 2022
173
364
Amani kwenu wote.

Naomba kushare na ninyi hii dawa ambayo imenitibu kabisa viral infection. Msimu huu na tunaouelekea wa baridi, ukikoswa koswa na seasonal flu ni bahati. Nlialikwa iftar mahali kukawa na katoto kana homa kali basi baada ya pale wote tulivyoondoka kila mmoja wetu ni mafua, kifua, homa, tonsillitis zimevimba na uchovu wa hatari hata kula tabu.

Basi nikachukua nikatengeneza dawa hii na leo wiki imeisha jamani nimepona namshukuru Mungu.

Dawa ni kama ifuatavyo:

Chemsha maji moto plain.Yakiendelea kuchemka kisha chukua manjano mbichiile unaisaga kwenye kile kidude cha carrot pale padogo kabisa alafu unaiweka kwenye kichujio. Saga na tangawizihivyo hivyo. Alafu weka chujio juu ya kikombe alafu mimina yale maji moto.

Unaacha kale kachujio pale kwa kama 12mins maji yawe infused na ule mchanganyiko. Kamua na limaojuu. Baada ya hizo dk12 ukitoa kichujio tia asali ya kalonjikwenye hiyo chai alafu jitahidi kunywa ikiwa ya moto bado. Asbh na jioni. Yaani utasahau stress za viral infection. (Kachujio kawe na kakitako kanakodumbukia ndani ya kikombe ili maji yawe infused vizuri na mchanganyiko)

Kama huna asali ya kalonji, basi zitwange kalonji kwenye kiuri kijiko kimoja kidogo uweke kwenye chai na asali kijiko kimoja kidogo (Asali usiweke maji yakiwa ya moto sana inapoteza nutrients)

Pia ukipona, uwe unaunywa huu mchanganyiko every other day maana unaboost sana immunity.Mara 3 kwa wiki au nne!

Ni hayo tu. Sharing is caring!
 
Chai yangu haikosi mchaichai,tangawizi,mdarasani,karafuu,pilipili manga,hiriki bila kusahau limao,hakika mafua nayasikia kwa jirani tu.


Kuna hii pia,chukua kitunguu swaumu, limao yachemshe weka na manjano kunywa kila siku asbh glass moja.
 
Back
Top Bottom