Kuna jamaa kipindi cha nyuma alitaka kunidhulumu kiwanja fln hiv makusudi tu. Nikamtuma kijana mmoja akaniletee udongo wa kile kiwanja niufanyie kazi!
Nilichokifanya sasa; nilichukua chumvi ya asili nilitoa kateshi, nikachanganya na huo udongo, nikaandika na jina la huyo bwana na rafiki zake ili umoja usiwepo, nikasali sana ile usiku..sana..asubh nikampigia yule kijana aje achukue hlf akamwage ule udongo +chumvi pale kwenye kiwanja!
Nikamwambia sasa tutulie huyu jamaa hatafatilia tena hiki kiwanja na atakisahau mana nia yake si nzuri! Ooooh alinitafuta mwenyewe, akanambia hiki kiwanja ni chako sina mda wa kubishania haki ya mtu!
Tunapeana hi tu tukikutana!
Kuna ofisi moja nilikua nataka mkopo, sasa kila siku usumbufu, hawataki kunipa hela....nikahakikisha napata majina yao wote wale afisa mkopo na meneja wao...nikafanya juu chini nikabeba udongo kidogo sana wa pale, kwasababu sipeleki kwa mganga naweza shika udongo kwa mkono tu haina shida, ni tofauti na kwa mganga...sasa sababu namwamini Mungu katika Kristo Yesu, nilifanyia kazi navyojua mimi, nikarudi pale kwa kuhangaikiwa nipate hela haraka, wakajilaumu kwann wamenicheleweshea kunipa mkopo mapema, niliwanyamazia tuu!
Haya mambo yanafanya kazi kwa kupitia imani ambapo lazima kuwepo na ufahamu fln utakaoungana na hiyo imani na imani lazima iungane na supernatural being...hakuna mtu duniani anayeishi nje ya kuamini kwake, hayupo na hatatokea.