greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 779
- 1,209
MAKALA YA 4
Karibuni katika Makala yetu ya Ujenzi,Ambapo dhana na lugha ngumu ya Kitaalam inageuzwa kuwa nyepesi na kueleweka.Leo japo kwa ufupi tutajadili kuhusu suala la "Chumvi kwenye Jengo"
1.CHUMVI KATIKA JENGO : Hii ni moja ya athari na matokeo ya Dampness/unyevu katika sehemu za Jengo.
Katika kila Majengo 15 uyaonayo ukiwa mizunguko kuna ma4 ambayo yanakumbwa na kadhia hii ya Chumvi Chumvi kwenye Kuta,Slab au Msingi wa jengo.
Aina za element za chumvi ni Sodiam,Potashiam,Kalshiam,Magneshiam,Kloraid,Salfeti,Kaboneti na Naitreti.
2.CHANZO : vyanzo vikuu vya Chumvi katika jengo.
I) Ujenzi katika eneo lenye Udongo wa maji chumvi au maji chumvi.
Ii) Shughuli za kibinadamu mf. Ufugaji,
III) Bahari
IV) Matilio
3.USAMBAAJI : Chumvi Kwenye jengo usambaa kwa njia kuu tatu.
i) Unyevu unaopanda:hapa unyevu upanda kutoka kwenye Ardhi kwenda kwenye Jengo kupitia Msingi au Sakafu.
Ambapo maji hayo huwa na Chumvi ndani yake
-Hii hutokea pale unapojenga kwenye eneo ambalo udongo wake una chumvichumvi
-Namna ya kuyajua maeneo yenye chumvi:
a.maeneo yenye mikoko namatoresheo ya maji ya bahari. mf.Kunduchi Kilongawima na Ununio,Somangira na Geza.
b.Maeneo yenye Udongo mweusi ambapo kipindi kirefu cha mwaka utaona umelowa
Mfano;Mikocheni A,Bonde la Mpunga (Msasani),Bwawani(Mwananyamala).
c.Maeneo ambayo kuna Visima vifupi ,vyenye maji chumvi
-Kuangalia mimea, Kuna mimea kuota kwenye udongo wa chumvi mf.upupu,4.USAMBAAJI
ii.Unyevu Unaopenya: Hapa Hupenya kwenye Ukuta moja kwa moja.
-mvua ikinyesha na matone yake, yanarusha udongo wa chumvi ukutani
-Chumvi inayopeperushwa kutoka baharini kwenda kwenye majengo
-watu,Viumbe hai kukojolea ukutani.
- maji kutoka mazizi ya wanyama kugusa ukuta.
Nyumba za ukanda wa pwani huathiriwa sana na chumvi ya baharini.5.USAMBAAJI
(iii)Matilio zenye Chumvi : kwenye njia hii ya tatu, Hapa watu hujenga kwa kutumia
-matofali yenye chumvi.
Utajuaje
Unapoenda kununua,haya. matofal katikati ya nyuso yana weupe.
- Mchanga wenye Chumvi Utakuta mchanga una rangi. kama ya kahawia(Dar)
- Maji ya chumvi Maji yanakuwa na radha ya magadi
6.VICHOCHEZI : Ongezeko la Chumvi kwenye jengo lako,huchochewa na
i) Kiwango cha maji :
chumvi ili ipenye kuwa katika sehemu za jengo na kupenya huitaji uwepo wa unyevu/maji
ii) Joto :
uwepo wa joto, huvukiza maji yaliyo kwenye kuta na kubakisha chumvi.
-ndiyo mana mikoa pwani huathiriwa sana na chumvi kwasabu ya joto la pwani
iii) Upenyeshaji wa matilio :
matilio huwa na vitundu vidogo sana, ndipo maji hupenya na chumvi zake
Mf.Matofali ya BamBam ,vitundu huwa vingi kuliko tofali za Umeme.
7.Athari : chumvi ina athari nyingi sana kwenye jengo,hii ndiyo hufanya majengo ya ukanda wa Pwani na joto ,yasidumu kuliko majengo ya Mikoa yenye ubaridi.
-Chumvi humeng'enyua matofali
-Huaribu rangi
-Huaribu matilio za metali I.e Kopa, Aluminium
-Huarakisha kutu katika nondo
-Huaribu kwanza kuondoa ung'avu wake kisha uweka kutu.
-Huaribu mbao.
-Huaribu zege
-Upunguza maradufu uhai wa jengo.