Tiba mbadala ya chumvi: Sehemu ya tatu

Tiba mbadala ya chumvi: Sehemu ya tatu

Nipende kwanza kujivunia kwa mada ya tiba mbadala ya chumvi ... Sijivunii kwa wingi wa wachangiaji la hasha bali kwa mada husika kuwa msaada mkubwa kwa wengi mno... Tiba ile imewasaidia hasa kwenye
Kutopatwa na mauzauza tena
Kuota ndoto mbaya na za kuogofya
Kupata usingizi mororo
Kukingwa na nguvu hasi za kiroho
Kusafisha nyota zilizofifia
Kutakasa miili iliyokuwa imechafuliwa
Kuboost CD4 za kiroho
Kuleta mvuto
Kuondoa uchovu na kuleta uchangamfu, furaha na amani mioyoni

Baada ya hapo ilifuatia mada ya mrejesho : yatokanayo na tiba mbadala ya chumvi hii ilikuwa maalum kwa ajili ya ufafanuzi namna ya kuitumia chumvi vizuri kwa matokeo bora zaidi... Lakini vilevile kwa wale wenye shuhuda mbalimbali ambao wangependa kushare na wengine....

Hii ni sehemu ya tatu na ya mwisho kuhusiana na hii tiba mbadala ya chumvi... Kwa usahihi zaidi chumvi ya mabonge... Hivyo mwenye swali la ziada, hoja ama maoni bado anakaribishwa kuhusiana na kile nitakachoandika hapa ama kwenye mada zilizotangulia...

Wengi wetu wamekuwa wakidhani kuwa tiba mbadala ya chumvi ina dozi maalum hivyo kutamani kujua kwa hakika wanaweza kutumiaje, kwa kiasi gani na hata kwa muda gani....
Kwenye mada zilizotangulia nilishauri matumizi yawe kati ya wiki moja mpaka mwezi mmoja.... Lakini ningependa kusema hivi... IFANYE CHUMVI SEHEMU YAKO YA KUDUMU...
Kama hujawahi kuitumia chumvi basi kwa mara ya kwanza ni kiwiko kimoja cha mkono kwenye ndoo ya maji ya lita 20... Huhitaji kuikoroga bali utaoga na sabuni maji ya juu kisha yale ya mwisho yenye chumvi ndio utatumia kujisuuzia huku ukiyanenea na kunuia utakayo....
Kama ni nyumbani ama ofisini basi nyunyiza ama mwagia kuzunguka eneo husika.... Na kwa kuogea unaweza kufanya hivyo kwa mwezi mzima bila kukosa....

Baada ya hapo ifanye chumvi sehemu yako ya maisha kama ilivyo simu yako, sabuni yako, lotion yako nknk.. Hakikisha chumvi haikosekani na unapoitumia kuogea si lazima uweke kiwiko kizima la hasha bali hata punje mbili tatu zinatosha kabisa.. Usiache kuwa nayo nyumbani, chumbani, ofisini kwenye gari na hata kwenye mkoba...

Chumvi ya mabonge ni tiba rahisi isiyo na miiko, isiyo na maagano isiyo na masharti, nafuu ya bei na rahisi kuitumia.... Usiipuuze wala kuidharau... Imewafaa wengi na haina uhusiano na ushirikina wala uchawi...
ANGALIZO muhimu : ukiona kwako haijafanya kazi tarajiwa usiichukulie haifai bali nayo ni tiba kama tiba nyingine.... Inaweza kumsaidia mmoja na mwingine isimsaidie... Japo naamini asilimia 95 inafanya vizuri View attachment 1186647
Nimekucheki PM mkuu
 
CC : mnyililo

Jr[emoji769]

Ndugu nimekuwa nafatilia mada hii kwa muda
Wiki iliyopita nami nikaanza kutumia chumvi Nimekuwa napata Changamoto ya kuwashwa mwili mzima. Nimejaribu kusitisha kwa muda toka juzi laki bado nawashwa ... naomba usaidizi wa mawazo tafadhali


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndugu nimekuwa nafatilia mada hii kwa muda
Wiki iliyopita nami nikaanza kutumia chumvi Nimekuwa napata Changamoto ya kuwashwa mwili mzima. Nimejaribu kusitisha kwa muda toka juzi laki bado nawashwa ... naomba usaidizi wa mawazo tafadhali


Sent from my iPhone using JamiiForums
Unatumia chumvi ya aina gani?
Unatumia kiasi gani?
Una historia ya mzio?
Ukiachana na hilo la kuwashwa je umeona nini kingine?

Jr[emoji769]
 
Unatumia chumvi ya aina gani?
Unatumia kiasi gani?
Una historia ya mzio?
Ukiachana na hilo la kuwashwa je umeona nini kingine?

Jr[emoji769]

Natumia chumvi ya MAwe
Kiasi ni nusu ya kiganja cha mkono
Sina historia ya mzio kabisa
Matokeo nimeona tofauti nyingi sana
Kwanza nilikuwa nalala sana yaani mtu anaweza kuniamsha kwa tarumbeta lakini baada ya kuanza kutumia chumvi hii hali imeisha. Pili nilikuwa naota ndoto nyingi lakini halii hii pia imetoweka
Tatu katika kazi nilikuwa kama Nina Mkosi/nyota chafu maana hakuna nilikuwa nafanya nikafanikiwa lakini kwa sasa angalau kazi inaoneka namshukuru mwenye mungu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Natumia chumvi ya MAwe
Kiasi ni nusu ya kiganja cha mkono
Sina historia ya mzio kabisa
Matokeo nimeona tofauti nyingi sana
Kwanza nilikuwa nalala sana yaani mtu anaweza kuniamsha kwa tarumbeta lakini baada ya kuanza kutumia chumvi hii hali imeisha. Pili nilikuwa naota ndoto nyingi lakini halii hii pia imetoweka
Tatu katika kazi nilikuwa kama Nina Mkosi/nyota chafu maana hakuna nilikuwa nafanya nikafanikiwa lakini kwa sasa angalau kazi inaoneka namshukuru mwenye mungu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
Endelea na dozi usiache

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom