Leo ni siku ya Kimataifa ya Ugonjwa wa Kisukari, hauna tiba zaidi ya Insulin for life. Je, tiba asili na tiba mbadala ni Effective?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Ugonjwa wa Kisukari, huu ugonjwa uko kwenye kundi la magonjwa yasiyo ambukiza, ugonjwa huu hauna tiba za kihospitali zaidi ya kudungwa sindano ya Insulin for Life! kwa maisha yako yote.

Kuna wanganga wa kienyeji wa tiba asili na riba mbadala ambao wanajinasibu kuwa na uwezo wa kutibu kabisa Kisukari kwa kutumia tiba asili na tiba mbadala, na kudai mgonjwa ana pona kabisa!.

Ugonjwa huu unatesa sana haswa wanaume maana unaathiri performance, hivyo ukiwa na mwenza very demanding, there is no way out lazima tuu utasaidiwa!.

Na kwa baadhi ya wagonjwa akipata kidonda, hakiponi hivyo anakatwa kiungo!, hivyo mtu unageuka kilema!

Waganga na matabibu hawa, mimi huwa ninakutana nao kwenye maonesho mbalimbali.

Je ni kweli tiba asili na tiba mbadala zinasaidia? How effective tiba hizo?

Hawa ni baadhi ya wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala.

View: https://youtu.be/7xIm2y22fGE?si=p2GzQ-Ixe_tYTifR

Je, kuna watu wana ushuhuda wa ndugu zao, jamaa zao na marafiki ambao wamepona kabisa Kisukari kwa kutumia tiba asili na tiba mbadala?

Nawatakia maadhimisho mema ya Siku ya Kisukari Duniani.

Paskali
 
Ukiachana insulin hospital Wana vidonge pia,mgonjwa wa kisukari niliyekaa nae Karibu amekuwa akipewa hizo kila akienda clinic, lkn akinywa hizo zinamchosha sana anakuwa anasinzia muda mwingi.

Kuhusu za kienyeji Kuna mtu alimletea magamba ya mti ambao siujui kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania, akitumia hiyo dawa Sukari inafika mpaka 5 na kushuka zaidi.

Tatizo ni kwamba haiponi Kuna muda ataanza kusikia vibaya akipima anakuta imepanda. Sasa ninachofikiri ni kwamba hii miti ingepata wataalam kabisa ingeweza kuleta manufaa Fulani kwenye kutibia kisukari.
 
Mkuu mimi Herbalist Dr.MziziMkavu ninayo dawa ya kutibu maradhi ya Kisukari na Mgonjwa atapona kabisa kwa muda maalumu. Kwa mtu mwenye Ugonjwa wakisukari anitafute kwa wakati wake ili nipate kumtibia maradhi yake na apate kupona.
 
Kuna aina mbili za kisukari
Type 1 diabetes kongosho/pancrease imeakufa kabisa kwa hiyo anategemea insulin ya kujichoma
Type 2 diabetes hii ni ya kawaida na ndo wengi wanayo
 
Hii type one inasabibishwa na Nini?ni lifestyle au Kuna la ziada?
Hii inatokana na autoimmune, kwa maana mfumo wa kinga ya mwili ulishambulia kongosho kwa tafsiri kwamba ni adui ktk mwili na hivyo huaribu uwezo wa kongosho kufanyakazi. Kumbuka kazi ya kongosho mojawapo ni kuzalisha hormone zinazosawazisha sukari na ya mwili.
 
Kuna mtu alipona kisukari kwa miti shamba.
Sasa bahati mbaya hiyo miti haijulikani na mtaalamu amefariki.
 
Mkuu mimi Herbalist Dr.MziziMkavu ninayo dawa ya kutibu maradhi ya Kisukari na Mgonjwa atapona kabisa kwa muda maalumu. Kwa mtu mwenye Ugonjwa wakisukari anitafute kwa wakati wake ili nipate kumtibia maradhi yake na apate kupona.
Toa mawasiliano yako na utakuwa umewasaidia wengi kama utaweka hapa ni kiasi gani cha pesa kwa ' dose'
 
Hii inatokana na autoimmune, kwa maana mfumo wa kinga ya mwili ulishambulia kongosho kwa tafsiri kwamba ni adui ktk mwili na hivyo huaribu uwezo wa kongosho kufanyakazi. Kumbuka kazi ya kongosho mojawapo ni kuzalisha hormone zinazosawazisha sukari na ya mwili.
Okay, Asante
 
hii miti ingepata wataalam kabisa ingeweza kuleta manufaa Fulani kwenye kutibia kisukari.
Sahihi kabisa,nimekuwa nikieaza sana hichi kitu.

Kuna tiba za asili zinatibu kama vidongr,mimi nahisi wataalamu wangeifanyia tafiti zaidi wangejua vipi wafix ili iweze kutibu moja kwa moja tatizo
 
Ndio hivyo Tanzania bado changamoto
 
Ndio hivyo Tanzania bado changamoto
Ni fani gani ambayo mtu akisoma anakuwa anaruhusiwa kisheria kufanya tafiti za mitishamba na kutengeneza madawa ?

Kuna fursa naiona ila watu wanaipotezea
 
Tatizo vitu vyetu vizuri vya kiasili Wafrika hatuviweki kwenye vitabu, pili tuna ulimbukeni wa kuvidharau vitu vyetu vizuri. Ila tukae tukijua kizazi cha wazee wetu kimetibiwa na mitishamba.
 
Haturuhusiwi kuweka Mawasiliano hapa Jamii forums Mtu akihitaji atanitafuta PM nitazungumza nae juu ya matibabu yake huo ugonjwa wa Kisukari.
Dr. Weka mawasiliano hapa. Mbona wanaoisifia ccm kama Lucas Mwashambwa wanaruhusiwa kuweka mawasiliano na wanaweka kila siku iweje wewe jf wasikuruhusu?
 
Baadhi ya Ma-Moderator wa JF wananipiga Vita mimi Si unajuwa ukiwa Maarufu lazima utapigwa Vita. Waswahili wanasema Mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe. Ukinitaka mimi nifuate PM aka inbox tupate kuzungumza nitakupa mawasiliano yangu lakini hapa ninaogopa kupigwa BAN. Au kanitafute Faceboo kwa kuandika jina langu Herbalist MziziMkavu utanipata huko kiurahisi sana.
 
Back
Top Bottom