Habari Mkuu
Mshana Jr . Kwanza natanguliza shukrani [emoji120], Mimi ni mtu ninayesumbuliwa sana na kusisimkwa sana ubavu wangu wa upande wa kushoto hadi kichwani, midomo kucheza, nimeshahangaika sana kwenye swala la tiba bila mafanikio. Mganga anatibu baada ya wiki au siku 4 tatizo linarudi. Nimefatilia kuogea chumvi ya mawe nimeona imerudisha mvuto, kusisimkwa kunaenda kunapungua japo kwa taratibu, inabakia tu kama nimebandikwa kitu kizito kwenye kifua.
Nahisi hii niliyopigwa ni zongo. Nimeona hapo umezungumzia tena kuhusu dawa ya makata. Pengine hiyo inaweza kunitatulia tatizo langu. Samahani, naomba formula jinsi ya kuitumia hii makata na utaratibu wake.