Mshana Jr, nilipitia ule uzi wako wa Tiba mbadala ya chumvi sehemu ya kwanza, nikapitia tena ule wa mrejesho na nikamalizia na huu,.
Kwanza nikiri ule uzi wako wa kwanza wa mwaka 2017 nilishauona kitambo ila sikuwahi kufuatilia kusoma.
Sasa juzi kuna mtu alileta chumvi ya mawe hapa home, sasa nilipoiona ndio nikakumbuka uzi wako ule,nikaanza kuusoma pamoja na comment zote nikamalizia na ukifuatilia utaona nimelike comment zako mle na za wadau wengine kwenye nyuzi zako hizo tangu jana.
Chumvi ya mawe nilikua naijua kazi yake hasa upande wa tiba kiafya ni nzuri sana, ila kwa upande wa kiroho nilikua sina ufahamu.
Jana nikaamua nianze kutumia kama ulivyoelekeza,kwa siku 1 tu ya jana asubuhi ndio niliogea.
Matokeo yake usiku ule nimelala usingizi mzito sana nakuja kushtuka karibia na muda wangu wa kuamka kabisa maana mimi mara nyingi naamka saa 11:30 alfajiri kitu ambacho sio kawaida maana wakati mwingine usingizi hua unakata usiku kabisa.
Halafu hata usingizi niliopata ni ule wa kupumzika hauna usumbufu yaani quality sleep, unajua ukilala usingizi mzuri hata akili na mwili vinajua kabisa na hata ukiamka una nguvu mpya na unakua mwepesi.
Kweli nimeamini Chumvi ina nguvu ya asili sio mchezo.
Asante sana mkuu kwa uzi huu, Na baada ya kusoma shuhuda za watu humu, hii chumvi nitaendelea kuithamini na kuitumia katika afya ya mwili na rohoni.
Leo naendelea siku ya Pili.
Ubarikiwe Kaka