THT inaweza kuwa chanzo na sababu kubwa ya Ruge kutofautiana na Wasanii wengi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,669
2,000
Ukweli ni kwamba kila kazi na fursa zake, palipo na fursa hapakosi changamoto na kila mtu na mazuri yake na mapungufu yake.

Ruge Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

THT, Tanzania House of Talent, ni kituo kilichoanzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe kwenye sekta ya sanaa hapa nchini.

Mwaka 2005, baada ya Rais Jakaya Kikwete kufurahishwa na ushiriki wa wasanii kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, aliwaahidi THT kuwajengea studio kubwa ya kisasa ili iweze kuwasaidia vijana wengi zaidi.

Baada ya serikali kutimiza ahadi yake na studio kukabidhiwa kwa THT, aliyekuwa Mkurugenzi mwanzilishi Ruge Mutahaba alianza kulalamikiwa na wasanii wenzake kuwa amejimilikisha studio hiyo kwa manufaa yake na rafiki zake, na ameifanya studio hiyo kama mali ya kampuni ya CMG inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV, na kuwa anawabagua, kuwanyonya na kuwadhulumu wasanii wengine.

Baadhi ya wasanii ambao hawakukubaliana na Ruge ni Lady JD, Joseph Mbilinyi SUGU, Dudu Baya, Q Chief, Joseph Haule na wengine, walianzisha umoja wa kupinga unyonyaji huo uliopewa jina la Anti Virus.

Sugu na Ruge waliingia kwenye ugomvi baada ya Sugu kumtuhumu Ruge kujimilikisha Project ya Malaria iliyofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia THT.

Lady JD aliwahi kumtuhumu Ruge na Kusaga kuwa ndio wanaonyonya jasho la wasanii, hadi kufikishana mahakamani kiasi kwamba waliapizana kutozikana, ugomvi uliopelekea Clouds kutopiga nyimbo za Lady JD na yeye kukimbilia EATV.

Q Chief naye alikwaruzana na Ruge kwa tuhuma za Ruge akishirikiana na BASATA kuzuia kibali cha mwimbaji wa Nigeria Davido.

Si hao tu, Ruge ameshawahi kukwaruzana na kundi zima la WCB linaloongozwa na Diamond Plutnamuz, ilifikia hatua wasanii walio chini ya WCB nyimbo zao kutopigwa na Clouds FM wala Clouds TV na hata kutoalikwa kwenye matamasha ya Fiesta yaliyokuwa yanaandaliwa na CMG. Leo WCB wameanzisha tamasha lao linalojulikana kama WASAFI Festival na TV yao ya Wasafi TV.

Karibu tujadili.
 
Born2xhine

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
798
1,000
THT hiyohiyo ndio imefanya wasanii wengi kutambulika katika tasnia hii ya Muziki mfano: barnaba anaetamba na wimbo uitwao washa pia msanii kama linah,amini na msami n.k hivyo kutofautiana kupo chamsingi ni kusameheana na pale ambapo mambo hayakwenda sawa
 
Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,713
2,000
Huyu Marehamu kazidiwa na lawama... haya maisha kamalizia kwa kuteseka na gharama kubwa I see. .. sifa nzuri nazisikia kwa Ccm tu wenzake masikini na kina barnaba....

Inanikumbusha sinema ya Yesu kuna mtu alisema hakika Huyu mtu hana kosa...

Na kwa Ruge mmh! Mwenyezi Mungu amuweke pahali panapomstahili...
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,416
2,000
It seems Ruge hakuwa na mahusiano mazuri na wenzake. Lakini ndiyo strugle for survival, au survival for the fittest....unatumia nguvu, mbinu zipi uweze kufanya biashara upate profit! uweze kuwa na eneo la "kujidai".. sphere of influence kubwa.. unaweza kufanya , kama huna roho ya Mungu uchafu wowote. Mshana Jr naomba comment yako , nimesoma andiko lako 40 min before
 
kibugumo

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
1,428
1,500
Mambo mengi tunayofanya na kuyapigania katika ulimwengu huu ni ubatili mtup!Mwanadamu aliezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi sana nazo zimejaa tabu na mateso!rip Ruge,mbele yako nyuma yetu!
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,799
2,000
ila ruge amelaumiwa sana enzi zake..

sugu kamtukana sana matusi ya nguoni... kwenye nyimbo zake
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,669
2,000
Ukweli ni kwamba kila kazi na fursa zake, palipo na fursa hapakosi changamoto na kila mtu na mazuri yake na mapungufu yake.

Ruge Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

THT, Tanzania House of Talent, ni kituo kilichoanzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe kwenye sekta ya sanaa hapa nchini.

Mwaka 2005, baada ya Rais Jakaya Kikwete kufurahishwa na ushiriki wa wasanii kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, aliwaahidi THT kuwajengea studio kubwa ya kisasa ili iweze kuwasaidia vijana wengi zaidi.

Baada ya serikali kutimiza ahadi yake na studio kukabidhiwa kwa THT, aliyekuwa Mkurugenzi mwanzilishi Ruge Mutahaba alianza kulalamikiwa na wasanii wenzake kuwa amejimilikisha studio hiyo kwa manufaa yake na rafiki zake, na ameifanya studio hiyo kama mali ya kampuni ya CMG inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV, na kuwa anawabagua, kuwanyonya na kuwadhulumu wasanii wengine.

Baadhi ya wasanii ambao hawakukubaliana na Ruge ni Lady JD, Joseph Mbilinyi SUGU, Dudu Baya, Q Chief, Joseph Haule na wengine, walianzisha umoja wa kupinga unyonyaji huo uliopewa jina la Anti Virus.

Sugu na Ruge waliingia kwenye ugomvi baada ya Sugu kumtuhumu Ruge kujimilikisha Project ya Malaria iliyofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia THT.

Lady JD aliwahi kumtuhumu Ruge na Kusaga kuwa ndio wanaonyonya jasho la wasanii, hadi kufikishana mahakamani kiasi kwamba waliapizana kutozikana, ugomvi uliopelekea Clouds kutopiga nyimbo za Lady JD na yeye kukimbilia EATV.

Q Chief naye alikwaruzana na Ruge kwa tuhuma za Ruge akishirikiana na BASATA kuzuia kibali cha mwimbaji wa Nigeria Davido.

Si hao tu, Ruge ameshawahi kukwaruzana na kundi zima la WCB linaloongozwa na Diamond Plutnamuz, ilifikia hatua wasanii walio chini ya WCB nyimbo zao kutopigwa na Clouds FM wala Clouds TV na hata kutoalikwa kwenye matamasha ya Fiesta yaliyokuwa yanaandaliwa na CMG. Leo WCB wameanzisha tamasha lao linalojulikana kama WASAFI Festival na TV yao ya Wasafi TV.

Karibu tujadili.
 
BILLY ISISWE

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,384

Clouds wakaanzisha team Kiba Hili kumkandamiza Diamond na watu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
2,358
2,000
P Funk, Mika Mwamba, Sugu, Lady Jay Dee na wasanii wengi ni miongoni mwa wasanii ambao bila ya sababu yoyote ya msingi Ruge aliamua redio yake isipige nyimbo zao.
Pia Ruge ndiye aliyeua muziki wa hiphop Tanzania akisema hiphop haiuzi na watu wanaoimba mapenzi ndio nyimbo zao zipigwe huku wakiimba wakiwa wamebana pua.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom