THT inaweza kuwa chanzo na sababu kubwa ya Ruge kutofautiana na Wasanii wengi

Umeunganisha unganisha vihabari...yaani umechanganya madawa tu.
Jaribu kufuatilia mambo Kwahi kina ndo uje uandike hapa...kinyume na hapo huu tunauita upotoshaji
 
WANAFIKI UKIWAAMBIA WANAKUPOOONDA!!!
Ukweli ni kwamba kila kazi na fursa zake, palipo na fursa hapakosi changamoto na kila mtu na mazuri yake na mapungufu yake.

Ruge Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

THT, Tanzania House of Talent, ni kituo kilichoanzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe kwenye sekta ya sanaa hapa nchini.

Mwaka 2005, baada ya Rais Jakaya Kikwete kufurahishwa na ushiriki wa wasanii kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, aliwaahidi THT kuwajengea studio kubwa ya kisasa ili iweze kuwasaidia vijana wengi zaidi.

Baada ya serikali kutimiza ahadi yake na studio kukabidhiwa kwa THT, aliyekuwa Mkurugenzi mwanzilishi Ruge Mutahaba alianza kulalamikiwa na wasanii wenzake kuwa amejimilikisha studio hiyo kwa manufaa yake na rafiki zake, na ameifanya studio hiyo kama mali ya kampuni ya CMG inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV, na kuwa anawabagua, kuwanyonya na kuwadhulumu wasanii wengine.

Baadhi ya wasanii ambao hawakukubaliana na Ruge ni Lady JD, Joseph Mbilinyi SUGU, Dudu Baya, Q Chief, Joseph Haule na wengine, walianzisha umoja wa kupinga unyonyaji huo uliopewa jina la Anti Virus.

Sugu na Ruge waliingia kwenye ugomvi baada ya Sugu kumtuhumu Ruge kujimilikisha Project ya Malaria iliyofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia THT.

Lady JD aliwahi kumtuhumu Ruge na Kusaga kuwa ndio wanaonyonya jasho la wasanii, hadi kufikishana mahakamani kiasi kwamba waliapizana kutozikana, ugomvi uliopelekea Clouds kutopiga nyimbo za Lady JD na yeye kukimbilia EATV.

Q Chief naye alikwaruzana na Ruge kwa tuhuma za Ruge akishirikiana na BASATA kuzuia kibali cha mwimbaji wa Nigeria Davido.

Si hao tu, Ruge ameshawahi kukwaruzana na kundi zima la WCB linaloongozwa na Diamond Plutnamuz, ilifikia hatua wasanii walio chini ya WCB nyimbo zao kutopigwa na Clouds FM wala Clouds TV na hata kutoalikwa kwenye matamasha ya Fiesta yaliyokuwa yanaandaliwa na CMG. Leo WCB wameanzisha tamasha lao linalojulikana kama WASAFI Festival na TV yao ya Wasafi TV.

Karibu tujadili.
 
Amegusa watu wengi, wengi wanaomlalamikia ukiangalia vizuri, utagundua kuwa marehemu ana mchango kwenye kuwainua! Na kwa kuwa mabaya huwa yanavuma zaidi!

Naomba niungane na chid benzi kwa hili!
Tumuombee apumzike kwa amani!
Nasi tujiandae kwani njia yetu in moja!

R I P RUGE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu wengi sana inaonekana ni wakuja au haya mambo wameanza kuyasikia majuzi juzi kuhusu Mawingu chini ya marehemu.

Mawingu walichofanya cha kwanza ni kuwajengea fikra wasanii bila mawingu huwezi ku' hit na kwa hilo walifanikiwa. Wasanii wao kwa vile wengi wao muziki ni maisha yao wakawa hawana jinsi, wakawa wanakubali kufanya kazi na mawingu kwa unyonyaji.

Na hata hawa wasanii wa kike nao wamebamizwa sana.
 
Amegusa watu wengi, wengi wanaomlalamikia ukiangalia vizuri, utagundua kuwa marehemu ana mchango kwenye kuwainua! Na kwa kuwa mabaya huwa yanavuma zaidi!

Naomba niungane na chid benzi kwa hili!
Tumuombee apumzike kwa amani!
Nasi tujiandae kwani njia yetu in moja!

R I P RUGE

Sent using Jamii Forums mobile app
Kawanyanyua wapi! Wasanii walinyonywa tu. Au kwa vile unaona nyimbo zao kupigwa sana kwenye radio yake? Au kujulikana kwa msanii kwa promo zao!

Mawingu hawakuwa kibiashara wapo kiunyonyaji. Uliza wasanii wanaozunguka mikoani Fiesta wanalipwa shilingi ngapi. Ukienda nao kibiz hawakubali. Kusikika utasikika na show chini yao utapata lakini hautokipata kile unachostahili.
 
Ukweli ni kwamba kila kazi na fursa zake, palipo na fursa hapakosi changamoto na kila mtu na mazuri yake na mapungufu yake.

Ruge Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

THT, Tanzania House of Talent, ni kituo kilichoanzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe kwenye sekta ya sanaa hapa nchini.

Mwaka 2005, baada ya Rais Jakaya Kikwete kufurahishwa na ushiriki wa wasanii kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, aliwaahidi THT kuwajengea studio kubwa ya kisasa ili iweze kuwasaidia vijana wengi zaidi.

Baada ya serikali kutimiza ahadi yake na studio kukabidhiwa kwa THT, aliyekuwa Mkurugenzi mwanzilishi Ruge Mutahaba alianza kulalamikiwa na wasanii wenzake kuwa amejimilikisha studio hiyo kwa manufaa yake na rafiki zake, na ameifanya studio hiyo kama mali ya kampuni ya CMG inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV, na kuwa anawabagua, kuwanyonya na kuwadhulumu wasanii wengine.

Baadhi ya wasanii ambao hawakukubaliana na Ruge ni Lady JD, Joseph Mbilinyi SUGU, Dudu Baya, Q Chief, Joseph Haule na wengine, walianzisha umoja wa kupinga unyonyaji huo uliopewa jina la Anti Virus.

Sugu na Ruge waliingia kwenye ugomvi baada ya Sugu kumtuhumu Ruge kujimilikisha Project ya Malaria iliyofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia THT.

Lady JD aliwahi kumtuhumu Ruge na Kusaga kuwa ndio wanaonyonya jasho la wasanii, hadi kufikishana mahakamani kiasi kwamba waliapizana kutozikana, ugomvi uliopelekea Clouds kutopiga nyimbo za Lady JD na yeye kukimbilia EATV.

Q Chief naye alikwaruzana na Ruge kwa tuhuma za Ruge akishirikiana na BASATA kuzuia kibali cha mwimbaji wa Nigeria Davido.

Si hao tu, Ruge ameshawahi kukwaruzana na kundi zima la WCB linaloongozwa na Diamond Plutnamuz, ilifikia hatua wasanii walio chini ya WCB nyimbo zao kutopigwa na Clouds FM wala Clouds TV na hata kutoalikwa kwenye matamasha ya Fiesta yaliyokuwa yanaandaliwa na CMG. Leo WCB wameanzisha tamasha lao linalojulikana kama WASAFI Festival na TV yao ya Wasafi TV.

Karibu tujadili.
Sasa Qchief na Davido wapi na wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na kwamba huwa inasemwa kwamba marehemu hasemwi kwa mabaya,lakini ukweli ni kwamba Ruge na station yao ya clouds tangu kipindi kile wakiwa ni radio station tu pale kwenye jengo la kitega uchumi,wamehusika sana kwenye kuharibu sanaa ya bongo fleva,kuvunja ama kugombanisha makundi mengi ya wasanii wa bongo fleva,na vile vile kuwanyonya sana wasanii wa hiyo fani.
Ni ukweli ulio wazi kuwa,jamaa amefanya kazi moja kubwa sana kuifikisha mawingu hapo ilipo leo hii,hilo halina mjadala kabisa,lakini vile vile amahusika sana kwenye kuwafanyia wasanii fitina na kuwalostisha ama kuwapoteza kisanaa.na kwa hili mimi simkubali kabisaaa pamoja na kwamba naona mapambio mengi tu humu ndani juu yake!!!
 
Back
Top Bottom