This is why all mama mean nothing to some people!

Jamani usaidiane kula watoto ilioenea waje kuwa watu arima wanawaza kuhimili stress. Sio mtu baba au mama ukipata shida kidogo tu unakimbia au ukiona greener pastures seems yoyote unasahau commitments zote unaondoka. Hio naita ni tendence ya uselfishness ambayo inakua. Mwanzo ilikuwa wakina baba siku hizi ni wote tu. Hawajali kabisa ahadi zao wala majukumu kwa wazazi au watoto mradi tu apate kitu roho nataka. Pole sana kaka, ilioenea usiige tabia ya ubinafsi ya mama yako pls tunza familia yako
 
Jambo hili hutokea kwa pande zote, ila kama utaweka kwenye mizani, wanaume ndio wanaoongoza kwa kutelekeza wake na watoto zao......
Nimewahi kufanya kazi na kijana mmoja kwa sasa hivi ni marehemu, (alijitioa roho kwa sumu miezi miwili iliyopita) Mungu amrehemu huko alipo. yeye alitelekezwa na mama baada ya mama yake kupata mzungu na kuolewa na kisha kuondoka nchini na kwenda ughaibuni. kibaya zaidi alikuwa hamjui baba yake, akaishia kulelewa ujombani......... ilikuwa kama mama yake akija nchini hataki hata kumuona mwanaye, na hata akienda kumuona hataki amwite mama bali amwite shangazi.............huyu kijana ameishi kwa sononi kwa karibu maisha yake yote, na hata kifo chake inawezekana hiyo ikawa ni moja ya sababu......... hapa ninapfanya kazi sasa yupo Binti, mama yake alimtelekeza na kuolewa na mzungu raia wa US, na kumuacha na baba yake akiwa na umri wa miaka miwili, huyu anaongea na mama yake kwa simu tu, lakini hajawaki kumuona. Baba yake hajaoa hadi leo, na ni mtu mzima sasa. alimlea na kumsomesha binti yake akiwa peke yake................
 
Ukweli kitendo alichokifanya mama yako hakina justification unless daktari atuthibitishie kuwa anamatatizo ya akili kama alivyosema Gaijin. Unasisitiza kuwa umemsamehe lakini kiuhalisia hujamsamehe kabisa. Pole sana sana sana but pls find it in ua heart to forgive ha. Msamehe tu bure kwa maana hiyo ndio njia pekee ya kukupa amani ya kweli na pia itakuondolea uchungu ulionao sasa. Najua sio rahisi but inawezekana, just do it as a sacrifice na Mungu atakusaidia.

Nimesikitika pamoja na wewe na wengine wote ambao walitelekezwa na wazazi wao kwa jinsi yako. Mi nimwanamke na wala sijazaa ila naishi na watoto ambao ninawalea ambao mama yao alifariki (ni ndugu yangu) na kuwaacha. Sijawaza hata sikumoja waishi na baba yao cos maisha ya mama wa kambo (wengi wao) singeweza hata kufikiria itakuwaje.
 
Kbd ubarikiwe sana kwa kuwalea hao watoto,Mungu akuzidishie baraka nyingi!
 
Unapomtelekeza mwanao unakua umelaaniwa siku zote mpaka utakapozungumza na mwanao,hili ni jambo la hatari sana!
 
pole sana eiyer
hii ipo pande zote....nakumbuka kuna thread ilianzishwa nani kama mama/baba....kila mtu anaona mzazi fulani ananafasi yake kuendana na nani alikuwa karibu katika maisha yake.
 
pole mkuu,,mim nimekuelewa kabisa..pia nimeguswa na ulichokiongea..ila nashindwa kuelewa huyo mama ameumbwa na roho gani..ila mradi baba alikupa mapenzi basi tuna kila sbb ya kumshukuru Mungu na kusonga mbele maana mambo mengine hapa dunian hadi tunakufa hatutapata majibu yake.
 
Pole sana na umenikumbusha machungu
Hata mimi yalinikuta,mama aliona ndoa yake ni vyema zaidi kuliko mimi aliyenizaa nje ya ndoa.....Hakuthamini kuwa nilimwitaji wala hakujali uchungu aliyonipa kwa vitendo vyake.Nilipata upendo kutoka kwa baba wa kambo kuliko hata kwake.Alitugawa kwenye mafungu nami nilibaki pekeyangu coz ckuwa mtoto wa ndoa ile.kupokea vichapo na matusi ya hapa na pale hata yaliyo juu ya umri wangu.Ilibidi ndugu zake wanichukue na kunilea.
Hakutaka kunieleza baba yangu ni nani akidai kuwa amefariki na hafahamu ndugu zake.
Mimi ni mdada lakini for sure miaka michache iliyopita nilikuwa namchukia sana mama yangu....But baada ya kugundua kuwa atleast saffering alizonipa zimenifanya niwe mchakalikaji wa kujitafutia life{not dependat} nikapata nafasi ya kumpatia nafasi yake tena maishani mwangu.
For the life she is in she real needs me now more than ever and I am glad to help her.
Think twice na umsamehe Mama yako

mmh! Pole inawezekana mamaako alikuwa raped ndio maana alikuchukia! Nilishuhudia mdada hospital baada ya kujifungua alikataa mtoto kabisa kuhojiwa kumbe she was gang raped! So let us forgive our mama but we shd always love our fathers and appreciate wat they ve done in our life. Role ya baba huwa inasahaulika kabisa kwa watoto tukishakuwa wakubwa tunakumbuka mama zetu na kusahau baba zetu! Plse tuwapende baba zetu kama una uwezo mpigie hata simu mwambie nakupenda usisubiri afe ndio uanze kummwagia sifa!
 
Pole sana kaka,watu wengi wanasumbuka na maumivu,ya namnambali mbali,hilo kwako pia ni umivu,ulilo umizwa na mama yako,kusamehe na kusahau ni jambo muhimu zaidi,kwani litakusaidia kukuondolea hayo maumivu uliyo nayo kaka yangu,usipo samehe utabaki katika hiyo hali ,ni ngumu lakini Muombe Mungu akusaidie umsamehe,ili usiendelee katika hayo maumivu uliyonayo.
 
Wakina mama wakiamua kufanya ukatili utajiuliza sana hivi ni huyu ndio anafanya hivi kweli?!!! unaweza kuta mwanamke anagombana na mumewe anakimbia akidhani anamkomoa kumbe anakomoa watoto wake mwenyewe!! sasa unabaki unashangaa.la msingi ni kwamba sisi wote kama wanadamu tuna mapungufu,mimi mwenyewe naona nisipokuwepo nyumbani watoto wangu wanapata shida sana manake mama yao yupo lakini hajitumi kuangalia watoto hata kidogo...sasa hapo mtu utasema nani kama mama?!! jiulize pia nani kama baba, kusingiziwa mtoto inategemea kweli ushindwe kuangalia hata mguu ujue hapa sina kitu!!!
 
Ni kazi kwelikweli mimi nashukuru nililelewa na mama yangu jamani japo baba alianza kusongea baada ya kumaliza shule ya msingi.. bado huwa inakuwa ngumu kusahau. Na kibaya zaidi nilipomaliza from six miaka hiyo, nilipata tempo moja.. ikawa inalipa vizuri miaka ya 1997. Mama alikuwa na nyumba nzuri ya kulala lkn hana jiko la kupikia. Mnajua mambo ya vijijini basi nilaamua kumjengea jiko dogo la bati kama kumi tuu.. ila apike kwa amani, Baba alikuwa anaishi mjini, alipojua hivyo alikasirika bila ya mm kujua. Ila nilikuwa nawatunza watoto wa mama mkubwa yaani wakambo aliyenipokea kutambulishwa kama mmoja wa familia. Sasa ile tempo iliisha nilisota nyumbani kwa muda. Nikapata bahati ya kazi nyingine lakini ilinihitaji kusafiri na ilitakiwa nauli. Nilipomuomba aliniahidi kwenda kuchukua kwa mama mdogo bahati nzuri shangazi alikuwepo. Nilipofika niliambiwa kuwa hela hawezi kunipa wakati mm nilianza kumjengea mama badala ya kumpa yy hela. Kumbukeni mama amenilea as a single mother for good 14 yrs. Nimeenda secondary kwa support ya dada zangu. Iliniuma sana tena sana... nilimwambia shangazi point blank anifikishie ujumbe kuwa... nitenda hiyo kazi kwa nguvu za Mungu na nitaipata.. na wala hakuna shida yeyote ile. Niliondoka nilikaa almost miaka miwili bila kuonana naye. KWa kuwa mama yangu wa kambo amabye ndiye alikuwa mke mkubwa alikuwa maefariki na alinipokea vizuri sana.. jukumu langu ilikuwa kuwalea waliobaka pale nitakapoweza. Wadogo zangu waliniambia baba analalamika kuwa sitaki hata kuwasiliana naye. Ukweli nilimtafuta niakamsalimia akaomba msamaha. But damage ilikuwa tayari imefanyika tena kubwa sasa. watoto wa marehemu mama yangu wa kambo bado nawasidia na wa mwisho yupo form six private school na namuombea Mungu afanikiwe, namshukuru Mungu. Ila imekuwa vigumu sana, najitahidi kusamehe lkn ile flash back inaludi tuu. Katika haya maisha kila mmoja analo la kusimulia kwa kweli. Ila Mungu atutie nguvu siku zote.
 
Thats why nikimkuta mzazi katelekezwa na wanae huwa sishangai sana japo huwa inanisikitisha!! Pole sana Eiyer!
 
Hi natumai mu wazima!Hey plz woman don't get angry with me!Natumia mimi mwenyewe kama mfano;Nilizaliwa pamoja na ndugu zangu wawili hivyo tukawa wa3,wakati tukio linatokea mimi ndo nilikuwa mdogo kuliko wengine,mama yetu alitutelekeza jioni na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine,wakati huo my Late father(may his soul rest in peace)alikua amesafiri kikazi,toka siku hiyo sikumwona mama mpaka nilipotimiza umri wa miaka 13,tuliishi na baba bila ya baba kuoa coz hakutaka mapema tuteseke,mama alipokuja alituona kwa dakika chache tena kwa kulazimishwa na baba,Alipoondoka sikumwona mpaka nilipotimiza miaka 25 alipolazimishwa na marehem babu(apumzike kwa amani)ambae ni baba yake,tulikuja kuonana tena hosptl wakati babu anaumwa na hapo ni baada ya miaka mi3,mara ya mwisho nilimuona mwaka jana nilipoamua kwenda kumwona,kumbuka kwenye msiba wa baba hakuja,to be hornest with u,i don't feel anything for her!Pia sijui umuhimu wake,wala sijui mapenzi ya mama.Napenda nieleweke kua simchukii,najua yeye ni mama yangu,alinizaa na alininyoshesha,lakini haza ni majukumu yake!Hajawahi kunishawishi kwa njia yoyote kuwa yeye ni mama!Sasa kama huyu aliesikia uchungu kwaajili yangu yupo hivi,nitaona vipi umuhimu wa akina mama?Je kama mimi tupo wangapi?JE NI NANI KAMA BABA,I LOVE HIM MUCH,I WISH HE COULD BE HERE!
Mh... hii mbona inanihuzunisha?
 
Mwenzio nilimpotema Mama yangu nilipokuwa na miaka 2, simjui, siiui sauti yake naziona picha zake tu! natamani angekuwepo around me! nimemiss kitu kikubwa sana ktk maisha yangu MAMA! yote namwachia MUNGU yeye ajuae yote!
 
Blaki Woman,asante,lakini kiukweli kati ya wazazi wote hakuna alie bora zaidi ya mwingine,unaweza kuhisi mmoja ni bora lakini atakapokosekana huyo unaesema sio bora ndipo utauona ubora wake!
 
Ni kweli cheusmangala,mambo mengine majibu yake ni kazi sana kuyapata!Wakati mwingine maisha yanakosa maana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom