Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Hi natumai mu wazima!Hey plz woman don't get angry with me!Natumia mimi mwenyewe kama mfano;Nilizaliwa pamoja na ndugu zangu wawili hivyo tukawa wa3,wakati tukio linatokea mimi ndo nilikuwa mdogo kuliko wengine,mama yetu alitutelekeza jioni na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine,wakati huo my Late father(may his soul rest in peace)alikua amesafiri kikazi,toka siku hiyo sikumwona mama mpaka nilipotimiza umri wa miaka 13,tuliishi na baba bila ya baba kuoa coz hakutaka mapema tuteseke,mama alipokuja alituona kwa dakika chache tena kwa kulazimishwa na baba,Alipoondoka sikumwona mpaka nilipotimiza miaka 25 alipolazimishwa na marehem babu(apumzike kwa amani)ambae ni baba yake,tulikuja kuonana tena hosptl wakati babu anaumwa na hapo ni baada ya miaka mi3,mara ya mwisho nilimuona mwaka jana nilipoamua kwenda kumwona,kumbuka kwenye msiba wa baba hakuja,to be hornest with u,i don't feel anything for her!Pia sijui umuhimu wake,wala sijui mapenzi ya mama.Napenda nieleweke kua simchukii,najua yeye ni mama yangu,alinizaa na alininyoshesha,lakini haza ni majukumu yake!Hajawahi kunishawishi kwa njia yoyote kuwa yeye ni mama!Sasa kama huyu aliesikia uchungu kwaajili yangu yupo hivi,nitaona vipi umuhimu wa akina mama?Je kama mimi tupo wangapi?JE NI NANI KAMA BABA,I LOVE HIM MUCH,I WISH HE COULD BE HERE!