Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,925
- 30,273
DULLY SYKES
Hukaa nikarudi nyuma sana katika fikra.
Ilikuwa mwaka wa 1968 mimi na Ebby Sykes tumekaa kwenye kibaraza cha nyumba moja Mtaa wa Mchikichi na Livingstone.
Ebby alikuwa ndiyo kafiwa karibuni na baba yake.
Hapo si mbali sana na kwao nyumbani kwa bibi yake Bi. Mruguru bint Mussa.
Ebby kwa siku hizo namkumbuka kila akitoka amepiga suruali ambayo kiuno ni kikubwa anaikazia na mkanda kisha juu wakati mwingine amevaa koti zuri na shati la kuvutia.
Hizi zilikuwa nguo alizoacha marehemu baba yake Abdulwahid Sykes.
Siku ile Ebby alikuja pale barazani na guitar zuri la umeme akawa anafanya mazoezi kupiga nyimbo moja ya Sam and Dave, "Hold On I am Coming."
Guitar hili katoka nalo nyumbani kwao na lina historia ndefu...
Ni miaka mingi imepita.
Rafiki yangu Ebby katangulia mbele ya haki.
Nataka leo niandike kitu kuhusu mwanae Abdulwahid maarufu kwa jina la Dully.
Nilipanda basi la Tahmeed na Dully sote tunakwenda Mombasa.
Ilikuwa mwaka wa 2014.
Nikamuona Dully na team yake nzima wamefika lakini wamesimama nje ya ofisi ya Tahmeed.
Wanakwenda kutumbuiza Mombasa.
Hili ni basi la kwanza Alfajir saa 11.
Dully hanifahumu.
Mimi nikashuka kwenye basi nikamwendea pale aliposimama nikamtolea salaam.
Akaniitikia kwa adabu sana.
Hapo nikajitambulisha na kumtaja baba yake, Ebbie nikamwambia, "Mimi na baba yako Ebbie tumepishana kuzaliwa kwa siku moja yeye kanitangulia, siku ya pili nikazaliwa mimi na siku zote tumekuwa marafiki ndugu.
Mpe salamu zangu mwambie tumekutana."
Siku narudi kufika Likoni Ferry nikaona hiyo flyer ya jina la Dully Sykes inatangaza show yake.
Haraka nikapiga picha huku basi linakwenda na nashindwa kupata jina la Dully kwa ajili ya upepo uliokuwa ukipindua hiyo flyer.
Picha hii nilikuwa sijaiweka popote.
Nikakutana na Dully kwenye maziko ya baba yake.
Hatukukutana tena hadi kwenye Khitma nyumbani kwa Mama Ali aliyekuwa mke wa Aziz Ali.
Kumbe Dully alipozungumza na baba yake akamwambia Mohamed anatujua sisi sote kwani watu wa Gerezani wakijuana na kuishi kama ndugu miaka na miaka kabla hata sisi hatujazaliwa.
Dully akanifuata akaniambia, "Uncle Mohamed wewe umeandika kitabu cha babu yangu, hebu niambie babu yangu alikuwaje."
"Dully babu yako alikuwa akikata mitaa ya Dar es Salaam anaendesha Mercedes Benz yake na vijana wa Kariakoo waliokuwa na Mercedes alikuwa babu yako Abdulwahid Sykes na kijana mmoja wa Kiarabu Abbas Abdulwahab."
Dully aliruka akapiga kelele kashika kichwa akawageukia wenzake, "Mmesikia? Babu yangu akiendesha Mercedes."
Dully akanigeukia akasema, "Uncle mimi nilikuwa na Mercedes nikapatanayo ajali Sea View."
Dully akawa kafurahi sana.
Sikutaka kumwambia kuwa baba yake mkubwa Kleist na yeye akiendesha Mercedes mji huu huu wa Dar es Salaam katika miaka ya 1980s.

Picha ya tatu ni Mwandishi na Ebby Sykes picha hii tulipiga mwaka wa 2010.