This is Rostam I know... The Story Behind the Man

yani mtu mmoja kama huyo anaweza kuwa brainwash mijitu mizima ya ccm na wakaona hela za rushwa ni bora kuliko mali za nchi yao.hii inasabibishwa kuwa na viongozi malimbukeni na waoga wa maisha ya uraia kwani hawana elimu ya kuweza kujitafutia mali kwa jasho lao.
 
Kwani Mababu zetu walipoingia mikataba na wageni wa Kiarabu na kizungu ili watawaliwe mambo siyalikuwa hivihivi tu??

Unakatiwa kipande cha nguo kufunga kiunoni na mkeo anapewa shanga za kuvaa kiunoni mnauza nchi yenu kwa wageni.

Tunaambiwa walowezi walikuwa na bunduki na kuwalazimisha babu zetu, hiyo si kweli hata kidogo. Watawala wetu wa zamani walilainishwa kwa zawadi za kipuuzi na kuamua kuuza nchi kuliko uongo kwamba bunduki ziliwatisha.

Kuna Risasi iuayo zaidi ya risasi ya udhaifu na uroho??

Ukiweka nchi makalioni na uchoyo mdomoni, hakika utakuwa radhi kuuza nchi kwa thamin ya ada ya vijana wako wawili kusoma UK.
Thamani ya nchi uiuzayo ni Shilingi ngapi? Hata hujiulizi kwa vile akili yako imezibwa na kiwi ya Uchoyo na ubinafsi.

Pande la nchi lililo jaa dhahabu kwetu si mali hata kidogo, mali ni Fedha taslimu ndani ya mfuko wa Khaki kutoka kwa Fisadi bila hata kujiuliza kazitoa wapi.

MH R Aziz naye ni sawa na Wale walowezi wa mwanzo, leo viongozi wa CCM wanakatiwa tambala la kujifunga kiunoni(vijisenti) na wake zao wananunuliwa shanga na Rostam ili aruhusiwe kuunajisi uchumi wetu.

Akili za viongozi wetu ni sawa na akili za jogoo. Punje ya almasi si mali wala si chochote mbele ya jogoo mwenye njaa atafutaye punje ya mtama.

Mawazo ya jogoo huyu yako juu ya punje ya nafaka ishibishayo leo na si thamani ya almasi iwezayo leta shibe kubwa baadaye. Viongozi wetu wameidharau nchi na mali yake kwa kutafuta fedha taslimu za kutatua matatizo ya udhaifu wao.

Ardhi na watu wa Tanzania ni bugdha kubwa mbele ya viongozi wetu, si vibaya wakiwa utumwani ndani ya nchi yao wenyewe kama tendo hilo litawapa viongozi wetu shibe ya leo.

Watanzania wengi hatuamki na kutumia uwezo wetu kuondoa tabaka hili la wahuni kuongoza nchi kwa sababu kwa ujinga tunaamini zamu yetu ya kuinajisi nchi itafika nasi tutakula tupendavyo. Au tunafaidika na vidondokavyo kutoka katika meza itumiwayo na viongozi wa CCM kunajisi nchi. Hivyo tunaamini kwa dhati kwamba tukikomesha unajisi wa nchi huo utakuwa mwisho wetu wa kufaidi makombo ya unajisi. Kwa lugha nyingine sisi wananchi tunashiriki katika karamu chafu ya kujinajisi na kudumisha laana katika nchi yetu kwa kujua kwetu na kwa kuto kujua kwetu.

Siku ghadhabu ya kuwapatiliza wote walionajisi nchi yetu itakaposhuka, hata wale wanukao makombo ya unajisi nao watagubikwa na ghadhabu hiyo.
 
Inabidi kumshawishi RA awekeze vitegauchumi vyake nchini hususan kwao Igunga pengine itakuwa ni ukombozi kwa wana Igunga
 
Mkuu,
Hakuna anayemtetea RA.Tunachoongea hapa na uoga wetu wenyewe.Kama mtu anavielelezo na hayo mambo, basi nikwenda mahakamani.

Mkuu hapo kwenye nyekundu,
Umewauliza Shy, Uwiano Maalum, Yessir, Dar es Salaam, FisadiMtoto et al wakakukubalia kwamba hawamtetei RA?
 
Nafikiri wahisani wafanye kama vile walivyofanya kwenye EPA. Waligoma kutoa pesa mpaka waone hatua zinachukuliwa dhidi ya wahusika. Sasa tena inabidi wagome kutoa pesa washinikize hatua zichukuliwe dhidi ya RA huku nasi wananchi tukiongeza presha juu ya serikali ya JK bila kusahau wazo la mwenzetu alilotoa hapa la kumwomba MUNGU aingilie kati juu ya huyu RA. Tumwambie MUNGU sasa yatosha tulivyonyonywa, atukumbuke watoto wake tunavyoteseka na umaskini ili hali kuna mtu mmoja anachuma na kupeleka nje ya nchi.
 
Haya watetezi wa RA vipi article ya African Intelligence kuhusiana utata wa biashara zake?

TANZANIA
A truly mysterious businessman

The former treasurer of the government party, Rostam Aziz, cultivates an air of mystery. His name often does not even appear in the companies he owns.

The businessman Rostam Aziz, an MP for the Chama cha Mapinduzi (CCM, governing party), under suspicion by Parliament of being involved in several recent scandals, is also a fervent company creator. When he forms new companies, he gives the impression of juggling with the names. Although he owns around a dozen companies, some of which have the same address and/or phone number, his name only appears clearly on one of them, African Trade Development (T) Ltd (ATDL). Even then, in the Business Registration and Licensing Agency (Brela) document concerning this company, he is listed as a director of ATDL but under the name Rostam Sakarri. All of the company’s other directors have fairly similar sounding names that are more or less derived from his: Rostom A. Sakarr, Rustom Aziz Sakarr, Rustam Sakarri and Rustam Sakaari. On the shareholder lists of other companies, the Tanzanian businessman appears to hide behind Iranian sounding names like Chakaar and Mehrab.

Nor is the name Rostam Aziz listed on Brela documents of at least half a dozen other companies which are supposed to belong to him, such as Africa Tanneries Ltd, Tanzania Leather Industries Ltd, Wembere Hunting Safari Ltd, Tanzania Packages Manufacturer Ltd and even the most well-known of them, Caspian Construction Ltd. Rostam Aziz has publicly stated that he has acquired Habari Corporation Ltd (HCL), a company publishing several newspapers and the proprietor of the media training institute Mamet. However, his name does not appear on the list of shareholders of Isenegeja Ltd which effected this purchase, nor on that of New Habari (2006) Ltd which was created to run this press company and which he nevertheless claims to own. A mystery indeed!
 
Last edited:
Yote hii haina maana yoyote kwa nchi kama Tanzania.. Mimi mwenyewe jina langu hukosewa mara kibao na kuandikwa kama Mukandara. Mukandala, Mkandala Mkadala na kadhalika tena sehemu nyeti inabidi mimi mwenyewe nifuatilie kuhakikisha makosa hayo yanarekebishwa..Lakini sii wote wanafanya hivyo kwa sababu hakuna msisitizo wowote..
Makosa mengi hutokana na uchapishaji au kutokuwa makini kwa hao makarani wetu.. kisha hakuna sheria imayosisitiza jina moja la cheti cha kuzaliwa ndilo pekee litumike kwa kila nyaraka....Trust me kuna watu wameitwa Rashad jina ktk cheti cha kuzaliwa kimetoka kama Richard na akaweza kwenda kusoma hadi chuo kikuu kwa jina la Rashad lakini cheti kikaandikwa Rashard..Passport ikawa na jina la Rashad..

Ili mradi tu miaka hii ya karibuni watu hawa wamepata taabu sana ktk kuchukua fedha zao benki, Western Union na sehemu nyingi zenye kuchunguza majina kwa uangalifu..
 
All of the company’s other directors have fairly similar sounding names that are more or less derived from his: Rostom A. Sakarr, Rustom Aziz Sakarr, Rustam Sakarri and Rustam Sakaari.

Mkuu, hapana! hii haiwezi kuwa ni kukosea. Kumbuka kuwa hayo majina yote yapo kwenye hati moja ya usajili wa kampuni moja. so, kama ni makosa si lingeandikwa moja? au unamaanisha nini mkuu? (huenda sijakupata). I am sure kuwa majina huwa yanakosewa kama ulivyosema, lakini haiwezekani ktk usajili wa kampuni moja, hati moja majina yakakosewa yakawa Mkandara, Mkandala, Mukandara na Mukandala. Haiwezekani Mkuu.

Rostam anacheza mchezo wa kuficha majina, kama tulivyofanya hapa JF kujiita nick names, kwa lengo la kukwepa responsibility.
 
Tatizo si Rostam bali ni sisi wenyewe, anayolifanyia taifa wabongo Rostam kama tunavyoelekea kuelezwa na mwanzilishi wa hoja hii, tutakuwa tumeyataka wenyewe. Huyo msajili wa hayo makampuni si mtanzania mwenzetu? au katoka Irani. Na mwenye kauli ya kiungu (akisema panda unapanda, akisema zama unazama) si mtanzania pia? au ana damu ya Iran?. Sasa wote hao wameshindwa kumthibiti Ropstam kweli? Pamoja na Mengi kumtaja hivi akina Siwema wamekosa misuli ya kumshughulikia kabia kabisa? na anaachwa aendelee hivi hivi?

Siamini nadhani naota ndoto
 
Prince William asante kwa uzalendo wako. Tukifanikiwa kuujulipanga umma ukamjua adui huyu tutashinda
 
Tatizo si Rostam bali ni sisi wenyewe, anayolifanyia taifa wabongo Rostam kama tunavyoelekea kuelezwa na mwanzilishi wa hoja hii, tutakuwa tumeyataka wenyewe. Huyo msajili wa hayo makampuni si mtanzania mwenzetu? au katoka Irani. Na mwenye kauli ya kiungu (akisema panda unapanda, akisema zama unazama) si mtanzania pia? au ana damu ya Iran?. Sasa wote hao wameshindwa kumthibiti Ropstam kweli? Pamoja na Mengi kumtaja hivi akina Siwema wamekosa misuli ya kumshughulikia kabia kabisa? na anaachwa aendelee hivi hivi?

Siamini nadhani naota ndoto

Yaani anatokea Rais wa CCM na Mweka Hazina wa CCM wanamwelekeza Gavana wa BoT achote mabilioni ya wananchi, na tatizo unasema ni sisi? Give me break!

Tanzania ina tatizo kubwa, nalo ni CCM. Na wanalindana miaka yote hii. Haitawezekana kuwafikisha kwa Pilato wakati wako bado madarakani. Siku CCM itakapowekwa benchi basi ndio yote haya yatashughulikiwa.

Nashauri CHADEMA iunde, publicly, KAMATI YA KUKUSANYA NA KUHIFADHI USHAHIDI WA UFISADI UNAOFANYWA NA ULIOFANYWA NA VIONGOZ. Hilo litawapa fursa wananchi kufikisha kwenu yale wanayojua.
 
Yote hii haina maana yoyote kwa nchi kama Tanzania.. Mimi mwenyewe jina langu hukosewa mara kibao na kuandikwa kama Mukandara. Mukandala, Mkandala Mkadala na kadhalika tena sehemu nyeti inabidi mimi mwenyewe nifuatilie kuhakikisha makosa hayo yanarekebishwa..Lakini sii wote wanafanya hivyo kwa sababu hakuna msisitizo wowote..
Makosa mengi hutokana na uchapishaji au kutokuwa makini kwa hao makarani wetu.. kisha hakuna sheria imayosisitiza jina moja la cheti cha kuzaliwa ndilo pekee litumike kwa kila nyaraka....Trust me kuna watu wameitwa Rashad jina ktk cheti cha kuzaliwa kimetoka kama Richard na akaweza kwenda kusoma hadi chuo kikuu kwa jina la Rashad lakini cheti kikaandikwa Rashard..Passport ikawa na jina la Rashad..

Ili mradi tu miaka hii ya karibuni watu hawa wamepata taabu sana ktk kuchukua fedha zao benki, Western Union na sehemu nyingi zenye kuchunguza majina kwa uangalifu..

Mkandara, hayo ni majina ya watu watano tofauti waliojaza fomu za umiliki za BRELA wakiwaonesha kuwa ni wana hisa kwenye hiyo kampuni. Hayo si majina ya mtu mmoja. Rostam ni mmoja wao.
 
Ah mi nimeshaanza kuchoka kusikia habari za huyu jamaa kwa kweli maana tunapiga kelele weee mwisho wa siku tunawakuta Rostam na wakulu wapo wanakula kuku, hii nchi ni ya ajabu sana kwa kweli mweh
 
Ndugu zangu mimi naona what we save us from FISADI PAPA Rostam Aziz is ACT OF GOD, najua nimekuwa nimetanda zambi kumuombea mtu kifo lakini kumbukeni kuwa yule achukuaye maisha ya watu naye hastahili kuishi. Rostam kauwa watanzania wengi sana kwa kuiba hela ambazo zingeweza kutumika kununua madawa ambayo yangesaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi
 
ROSTAM Aziz is a criminal who should have been serving life sentence for 'defiling' the country's economy had he not been JK's bedfellow. If he doesn't flee the country we'll make sure we charge him with economic sabotage as soon as we demolish CCM in next year's elections. This guy thinks we are stupid. We are not! We are following up your steps and you will suffer the consequences.
 
Potelea mbali hata tukiitwa wabaguzi. Lakini mbaguzi na muuaji yupi afadhali? Tunachosema hapa ni kwamba huyu RA ameiibia sana nchi yetu na kusababisha mauaji kwa wana wa nchi hii kutokana na kukosa huduma muhimu. Huyu sio mtu wa kutetewa hata kidogo. Kama serikali itashindwa kumkamata sisi wana wa nchi hii tutalazimika tutaji-organise tumkamate na kumfungulia mashitaka kupitia private prosecution. Wanasheria mliomo JF hebu tupeni ushauri. Naona sisi wengine uvumilivu unatuishia.
 
Prince William,

Karibu jamvini Mkuu. Hapa kumkoma giladi kwa kwenda mbele...tunajua RA amechukua hela zetu...inatia moyo wazalendo kama wewe mkija na data kutufahamisha ukweli hapa.

Damn, RA kweli ni Fisadi Papa...aliwafisadi CCM pia..
Ulitarajia nini afanye?
Stake kubwa kachukua yeye,the higher the stake.......
 
Back
Top Bottom