- Sometimes hawa huwa wanachukua habari hapa JF, hizi si tumezisema sana huko nyuma kwamba huyu Rostam hajasajili jina lake kama owner wa kampuni mahali popote, naona habari zinajirudia tena.
____________________________
Field Marshall ES:
Inawezekana wanachukuwa vyanzo hapa lakini wao wamekwenda mbali zaidi. Isitoshe inabidi tuwashukuru kwa kuzimwaga habari kwenye gazeti hilo (Mwanahalisi) lenye circulation kubwa kuliko magazeti yote nchini -- nasikia huchapa nakala 75,000 kila wiki. Wanaoingia humu JF sidhani kama wanafika robo ya hao.
Lakini pia ni dhahiri kabisa kwamba huyu RA daima amekuwa na dhamira zisizo takatifu dhidi ya nchi hii na wananchi wake -- ama sivyo atueleze sababu hasa ya kujificha nyuma ya majina ya wengine iingawa mimi naamini mengi ya majina hayo ni feki tu -- yaani hakuna watu halisi..
Kama ilivyoandikwa huko nyuma hawezi kuthibitisha kinagaubaga majigambo yake kwamba kampuni zake zimeajiri watu 6,000 au kwamba analipa mabilioni kila mwaka kama kodi serikalini. Hawezi, maana tunaweza ku-allege, bila wasiwasi kwamba hizo kampuni siyo zake, na hawezi kulazimisha kusema ni zake wakati hakuna ushahidi wa kimaandishi. Nasikia hata ofisi hana -- anababaisha tu mara hapa, mara kule.
Ni tapeli mkubwa hapa nchini na inasikitisha kuona vyombo vyetu vya dola vinakosa fyoko ya kumgusa.
Kwa mfano, inaaminika kwamba iwapo Mengi angewataja tu "mapapa" wa kizalendo (yaani siyo hao wenye asili ya Kiasia), sidhani kama akina Mkuchika, Maelezo, TCRA etc wangemsumbua Mengi. Kilichomponza Mengi ni kuwagusa wasiogusika katika nchi hii -- hao weupe.
Hawa na wengine wanaomtetea RA wanadhihirisha kweli ule usemi "Miafrika ndiyo tulivyo!" Hatutaendelea daima kwani bado tuko wanyonge sana. Nyerere angalau alijaribu kuondoa unyonge huu lakini sasa unarudi kwa kasi.