1.Jamani no-fly zone sio uamuzi wa USA bali ni wa umoja wa mataifa (UN). Kwa hiyo watu mnaoilaumu US nadhani hamjalifuatilia nakuliewa vizuri hili suala.
2. Mbona wanaolaumiwa ni wamarekani peke yako katika hili wakati wapo wengi tu wanaotekeleza hili ikiwemo UK, France, Qatar, Jordan (UAE), NATO(except Turkey) etc. vilevile nchi nyingi duniani zinasupport hili suala wakiwemo viongozi wa Africa kama Rwanda na Botswana(kama sikosei)
3. Tanzania na nchi nyingi tu duniani ni wanachama wa UN, lakini nchi ambazo nimebahatika kusikia kuwa zinapinga wazi no-fly zone ni Russia, China na Uganda. Sijui kuhusu nchi yetu Tanzania (unaweza ukakuta ni moja wapo ya wanaounga mkono)
4. Watu wamekuwa wepesi kujibu kuwa marekani imefuata mafuta libya. Je vipi kuhusu UN, UAE(Qatar Jordan), NATO, UK, France na mataifa mengine yanayoshiriki yanatafuta nini huko..?(usitoe jibu jepesi kuwa hawa wote ni vibaraka wa marekani coz kama ndio hivyo basi ni dunia nzima)
5. Hivi ni kweli uchumi wa USA unategemea sana mafuta kiasi hiki (wataalamu wa uchumi wa dunia tusaidieni katika hili)? Je ni kweli kuwa USA huwa inaiba au kuchimba mafuta kule Iraq na Afghanistan au ni uzushi tu huu?(wikileaks mko wapi?)
Tupeana facts waheshimiwa, stick to the topic, its hard bt try not to be biased an Feel at home.