The West Policy on Libya Vs Putin

The West Policy on Libya Vs Putin

Shirika la kujihami la NATO sasa limekbali kuchukua jukumu la kuthibiti anga ya Libya ili kuhakikisha marufuku ya ndege kutopaa inatekelezwa.

Hatua hii imeafikiwa kwenye kikao cha waakilishi wa nchi wanachama wa shirika hilo mjini Brussels Ubeljiji.

Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema wanachama wote wa shirika hilo wameunga mkono uamuzi huo.

Marekani ndio imekuwa ikisimamia utekelezaji huo lakini inataka kukabidhi wadhifa huo haraka iwezekanavyo.

Nchi wanachama wa NATO walikubaliana alhamisi usiku kuwa wachukue jukumu hilo na huenda wakakabidhiwa rasmi na Marekani katika siku mbili zijazo.

Kwa sasa shirika hilo linaongoza juhudi za kuzuia silaha kuingia Libya. Lakini bado haijaamuliwa ni nani atakae ongoza harakati za mashambulizi zinazoendelea katika lengo la kulinda raia wa Libya.

Katibu mkuu Rasmussen amesema kuwa wanajadiliana kuhusu uwezekano wa wao kuchukua wadhifa huo.

Kuna baadhi ya wahusika ambao hawapendezwi na kuwa wanajeshi kutoka nchi za magharibi wanaendesha operesheni za kijeshi katika nchi ya Kiislamu.

Kufuatia tashwishi hizo, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Uturuki inasemekani wamekubaliana kimsingi kuwa usimamizi wa harakati zote za kijeshi nchini Libya zinakabidhwa shirika la Nato.

Ikiwa hivyo, baraza la mawaziri kutoka nchi wanachama wa NATO wakiwemo viongozi wa nchi za kiarabu zinazounga mkono hatua zinazochukuliwa dhidi ya Libya, watahusika kikamilifu katika maamuzi ya operesheni hiyo.
 
jamani kitendo ambacho marekani inafanya kwa libya sio kitu ambacho watu kama wao waweza kaa chini nakuangukia kwenye maamuzi kama hayo. swali ni kwamba. je wao wanasaidia hivyo vita vya wapinzani na serikali kuisha au wanavipa vikundi vya upinzani nguvu zaidi kuleta machafuko pia?
vipi kama wangekaa chini nakushauriana na hao waasi waache mapigano nakuweka maswala kama hayo mezani. hata kama gadafi hatakuwa tayari kwa hilo, haina sababu wao kuendelea na mashambulio kwani hata yeye gadafi aweza hayo.
au wenzangu mnasemaje jamani?
 
Kifupi ni kuwa hao wamarekani hawamtaki Gadafi na inaonekana walikuwa wanamsubiri kwa hamu, sasa wamempata!!
 
wanaidharau africa s ndugu yangu, huyu mtoto wa kikenya sema anataka kujitoa ...nampongeza ..ingekuwa GBUSH sa ivi tungekuwa tunaongea mengine kabsa
Kama unamsifia OBAMA ndugu yangu hujui kinachoendelea. Hajajitoa. Ameharibu uwezo wa kijeshi wa Gaddafi na sasa anwaachia wadogo zake wamalizie kazi ya kuiteka Libya na mafuta yake. Hajajitoa kwenye mgao. Ila anaogopa isionekane ni Marekani inayofanya utekaji. Maslahi yake yatalindwa na hao anaowaachia kazi. Na kumuita Obama Mkenya ni kujidanganya. Ni lipi aliloisadia Kenya?
 
Hakika huo ni ubabe wa kutaka mafuta ya libya. Hata kama gadafi anatumia nguvu kuangamiza raia wa nchi yake, mbona raia kama hao huko ivory coast wamepoteza maisha lakini mmarekani hakuweza kumwondoa huyo rais aliyeng'ang'ania madarakani? Hapo ameona kuwa hakuna masilahi yake zaidi.

Viongozi wa africa nao wawe na uwezo au sauti kidogo angalau kumweleza obama kuwa ubabe siyo mwisho wa kila kitu katika mataifa madogo yanayostawi vizuri kiasi kiuchumi na mwisho wanakuja kusambaratisha tena uchumi ule kwa vita zisizokuwa na msingi wowote.
 
Its always bussines playing curtains behind the scene.
Mbona hawaingilii nchi zingine?
Wanafwata masilahi yao,haki unaijua weye.
 
Wanataka Mafuta hao wamarekani wamezoea kunywa damu za watu kwa hiyo sishangai hapo ...ila siku yao ipo inakuja
 
Hao jamaa walikuwa wakimuwinda Gadafi siku nyingi sana na sasa wamepata kisingizio...ila wakae wakijua wanatengeneza maelfu ya kina Osama na siku moja huko mbeleni 9/11 itawarudia tu. Nalaani vitendo vyote vya mabavu vinavyofanywa na westerns kwani havijengi ila vinaandaa anguko lao wenyewe siku moja.
Mungu waokoe Walibya na wote waonewao duniani,Amin.
 
Je sasa hawa wanasiasa wanaosema kuwa hata maandamano ya amani ya Chadema yanaweza leta vagi kama hilo je ni kweli? au niupumbavu wa fikra zao zimekuwa transmitted through midomo yao kutoa output ya faida zao.
 
mi naona gadafi ailpue marekan kisha amalzane na wapinzan wake kama ndo 3rd war poa 2 mbna wachina wamegoma kumsaidia mUSA kumtoa gadafi na istoshe wachna wanamdai mUSA ndo mana anajipendkeza kwa mchina MUNGU IBARKI LIBYA
MUNGU IBARKI AFRIKA
 
Mbona Somalia wamepigana weweee hawa wamarekani hawaendi huko
Wanajua Libya kuna masilahi ..Visima vya Mafuta
 
Mbona Somalia wamepigana weweee hawa wamarekani hawaendi huko
Wanajua Libya kuna masilahi ..Visima vya Mafuta

Well said...; Kwa wamarekani the so-called "national interests" zinachukua precedence juu ya haki - double standards of the highest order..
 
jamani kitendo ambacho marekani inafanya kwa libya sio kitu ambacho watu kama wao waweza kaa chini nakuangukia kwenye maamuzi kama hayo. swali ni kwamba. je wao wanasaidia hivyo vita vya wapinzani na serikali kuisha au wanavipa vikundi vya upinzani nguvu zaidi kuleta machafuko pia?
vipi kama wangekaa chini nakushauriana na hao waasi waache mapigano nakuweka maswala kama hayo mezani. hata kama gadafi hatakuwa tayari kwa hilo, haina sababu wao kuendelea na mashambulio kwani hata yeye gadafi aweza hayo.
au wenzangu mnasemaje jamani?
kweli marekani anaonea ila Gadaff naye hakuwatendea haki wanainxhi walipoandamana na kuamua kutumia jeshi.
As Gadaff alipoanza kutumia jeshi baadhi ya kambi zilasi na kupelekea machafuko.
To me:1. Marekani waache mara mmoja hii hujuma
2.Gadaff akabidhi madaraka kwa mwingine ili kushusha joto la machafuko (Ni upuuzi kusema Gadaff sio tatizo Libya ya leo)
 
Hao jamaa walikuwa wakimuwinda Gadafi siku nyingi sana na sasa wamepata kisingizio...ila wakae wakijua wanatengeneza maelfu ya kina Osama na siku moja huko mbeleni 9/11 itawarudia tu. Nalaani vitendo vyote vya mabavu vinavyofanywa na westerns kwani havijengi ila vinaandaa anguko lao wenyewe siku moja.
Mungu waokoe Walibya na wote waonewao duniani,Amin.
Mkuu.
911 ni wamarekani wenyewe ,ni covert operation kama ile pearl harbor.
Osama ni bogey man tu. Nani aliunda Al qaeda?
http://www.globalresearch.ca/index.php?context=va&aid=7718

kama una muda angalia hizo coincidences ,ziko 1 to 19 halafu kaa , fikiria utaona mpango ule ulikuwa ni wao waingie Iraq na afghanistan. na nchi za kiarabu kwa ujumla. hata zile balozi za East Africa ni wenyewe tu.utaelewa kadiri ya siku zinavyokwenda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom