The way how I know Mr. Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The way how I know Mr. Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joshua Bukuru, Oct 10, 2012.

 1. J

  Joshua Bukuru Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Sijawahi kutana naye uso kwa uso japo wote ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma. Lakini, nafurahishwa sana na jinsi anavyobeba mawazo ya vijana wengi wa kitanzania ambao wamesahauliwa na serikali yao kwa miaka nenda rudi. Somewhere something went wrong na viongozi wetu hawajaliona hili. Na hili ndilo limeifanya vijana kuichukia CCM na ari ya kuingiza viongozi vijana katika nyadhifa mbalimbali za uongozi limewadia. Leo sizungumzii hili bali nataka nijikite kwa yale ambayo yanasomeka magazetini juu ya mh. Zitto.

  Ndoto ya viongozi wengi ni kuwa rais japo wote hawawezi kuupata urais huo. Hivyo basi, ni lazima mtu mmoja aaminiwe na kutumainiwa na wananchi ili abebe jukumu hili kuu. Viongozi wetu ni wale wanaouwaza urais na ni wale wanaoutaka urais. Na viongozi wetu wanautaka urais kisiri siri na wengine wakisingizia kuwa wametumwa na wazee. Usiutake uongozi kisiri siri kama unataka kuwa kiongozi kweli. Tangaza hadharani harafu uje tukuulize kwa nini unataka kuwa rais au kiongozi wetu? Maneno haya si yangu kwa kuwa mwalimu Nyerere aliwahi kuyatamka. Nayarudia tena kwa mara nyingine. Kwanini?

  Hivi karibuni mh. Zitto Kabwe kwa kulifahamu hili aliamua kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa tiketi ya chama chake. Ni haki yake ya msingi na kikatiba. Maana katika maisha yapo mawili, kuongoza au kuongozwa. Anadai, ipo siku atatoa sababu kwa nini ataka kupeperusha bendera ya chama chake katika wadhifa huu mkuu katika utumishi wa umma. Hivyo basi, badala ya kuwa wavumilivu, wengi wameamua kumshambulia eti ni mapema mno kutangaza wakati angejikita katika siasa za kukijenga chama na hivyo kusababisha misuguano ndani ya chama chake.

  Mimi sioni misuguano ndani ya chama ambayo imekuja baada ya zitto kutangaza nia yake ya kuwania urais. Kama ipo, ikifuatilia kwa undani zaidi utakuta ni misuguano ambayo ilikuwepo hata kabla ya yeye kutangaza nia hii. Si kwamba nampiagia upatu au kumtetea? La hasha, siwezi kufanya hivyo kwa kuwa mimi si swahiba wake. Mbali na hilo hajawahi na sijawahi kukutana naye, na hivyo hanifahamu japo wote tunatoka mkoa wa Kigoma. Nalazimika kutoa maoni haya kwa kuwa vyombo vya habari nchini vimeacha kuandika mambo yanayohusu matatizo ya taifa na watanzania, badala yake kujikita kuamwandika Zitto. Zitto amekuwa gumzo nchini kuliko hata rais wa nchi. Najiuliza mwingine vipi kesho asipopita kwenye mchujo ndani ya chama au akatokea mtu mwingine ambaye chama kinamwona kuwa ni bora kuliko zitto. Mtasemaje?

  Mimi nadhani zitto ametangaza nia hiyo kwa lengo moja. Kwanza, anataka wanachama wa chama chake wampime na kumchunguza kama anafaa kupewa jukumu la kupeperusha bendera ya chama mwaka 2015. Lengo lake ni watanzania wampime. Mtampimaje? Wanachama wa Chadema jielekezeni katika utendaji kazi wake. Je anajituma ipasavyo ndani ya chama na nje ya chama? . Lingine, tumpime katika kuyatambua matatizo yanayolikabili taifa na umma wa wananchi, na hapa yapo mengi rukuki. Je anatoa masuluhisho ya matatizo hayo? Masuluhisho hayo yanajibu hoja za wengi hasa asilimia 80 ya watanzania maskini waishio vijijini na ambao wamesahaurika? Muhimu ni kwamba, je kuna tuhuma zozote zinamkabili hasa katika hasa katika utendaji kazi wake, vipi rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, ufujaji wa mali za umma katika nafasi zake za uongozi na mengine mengi. Tuhuma ziwe zimethibitishwa na vyombo husika.

  Kuna watu wengine wamediriki hata kusema eti hajishughulishi na shughuli za kukijenga chama, sijui kama kweli wanamfahamu Zitto Kabwe? Japo sipo nyumbani kwa kipindi kirefu na ninavyoandika maoni haya naishi nje ya nchi, lakini nimeshuhudia kupitia mitandao ya kijamii akishiriki kikamilifu kukijenga chama; kama vile kufanya mikutano ya hadhara hasa katika kutangaza sera za chama, zipo video nyingi na hotuba nyingi tu zinazomhusisha yeye na viongozi wengine wa chama. Ameshirika barabara katika kampeni mbalimbali za uchaguzi kuanzia udiwani na ubunge katika maeneo yetu ya nchi. Labda nyie mnaona kuwa haitoshi lakini lazima mseme ni nani kafanya zaidi yake na wapi? Au ni ile methali kwamba akutukanaye hakuchagulii tusi…

  Suala lingine la kujadili ni mapungufu ya katiba yetu ya chama, ambayo haiko wazi katika kutoa muda mwafaka wa wanachama wa kutangaza (mimi sijui ni lini mtu anatakiwa atangaze). Katiba ya nchi nayo ipo kimya ingawaje haihusiki kwa lolote katika hili, wanachama wa vyama vya siasa na vyama vyao wameachwa waamue wenyewe. Sasa basi, inakuwaje mtu amwandame Zitto badala ya katiba ya chama ambayo ipo bubu. Ndugu zangu wana-Chadema na watanzania kwa ujumla tujikite katika kujadili masuala ni si majina au watu binafsi. Mbona John Shibuda alitangaza na hakuandamwa kama anavyoandamwa Zitto? Mbona, Deogratius Kisangu katibu Bavicha-Tanga ametangaza na haandamwi? Iweje Zitto Kabwe?

  Mimi naona aibu sana kwa mwasisi wetu wa chama Edwin Mtei kujikita katika kujadili jina la mtu badala ya kujikita katika kujadili masuala. Mh. Mtei amekwazika sana baada ya Zitto kutangaza, ni kama alikuwa hategemei mtu kama Zitto angefanya hivyo. Hoja yake anadai wakati wake bado, sijui alitaka afanye hivyo lini wakati katiba nayo ya chama ipo kimya. Mimi naonelea kabla ya kumtuhumu mtu, tutuhumu kwanza katiba yetu ya chama na vilevile pia tutuhumu vyombo vya habari kwa vile navyo vinachochea migogoro ndani ya vyama vya siasa kwa lengo tu la kutaka kuuza magazeti.

  Wengine wamesema zitto ni mbaguzi eti asingesema kuwa mapinduzi ya kiuchumi Tanzania yataletwa na mtu wa kizazi cha baada ya uhuru. Hili tusingelijadili leo, tungesubiri siku ya kuchuja wagombea harafu tukamwuliza; ulikuwa na maana gani kutoa kauli ya kibaguzi kama hiyo. Huenda anazo sababu za msingi na akipewa muda anaweza kutufafanulia na tukamwelewa.

  Mwisho, ningependa kusema kuwa tuziangalie upya sifa za kumpata mgombea wetu kwa nafasi yoyote ya uongozi. Tuhakikishe tunaingiza sifa hizi ndani ya katiba yetu kwamba "yeyote ambaye anatuhumiwa katika matumizi mabaya ya fedha za chama na serikali (lakini tuhuma hizi ziwe zimethibitishwa na mahakama au kamati teule za bunge au tume za uchunguzi na vyombo vya dola), ubadhilifu wa mali za umma, rushwa na ufisadi" asilogwe kuchukua fomu yetu. Lazima tujifunze kutoka chama cha CCM ambapo wao hayo yamekuwa ni vigezo vya kuwapata viongozi. Hili likifanikiwa, hakuna mtu atakayethubutu kutangaza au kujigamba kugombea kupitia chama chetu.

  Suala la kumpata mgombea kwa kiti cha urais, tusiwaachie viongozi wetu wa chama na kufanya hivyo ni kujitakia matatizo. Mkutano mkuu au halmashauri kuu ya chama washiriki tu katika kuyachuja majina ya wagombea ili mwisho watuletee majina matatu au mawili ambayo yatapigiwa kura na wanachama nchi nzima. Atakayeshinda, ndiye awe mgombea wetu. Suala hili si lao, ni letu. Na kama ni letu basi, tuwaache wanachama wenyewe wafanye maamuzi ya mwisho. Hawa watatu wazunguke nchi kwa kampeni kushawishi wanachama wetu na kuwe na public endorsement kutoka kwenye party leaders kumwunga mkono mgombea anayeona anafaa.

  Zipo hoja hapa zitajitokeza kuwa gharama za kuendesha kampeni hizi zitatoka wapi? Tuwe wakweli na tueleze umaskini wa chama chetu, wao wajigharimie kwa gharama zao wenyewe. Hapa tutakuwa tumeepuka suala la viongozi kupatika kwa njia za rushwa, tusiiandame CCM pekee katika hili, kwani laweza kutokea kwetu. Madhara ya viongozi wanaopatika kwa njia za rushwa ni makubwa na watanzania tumeyaona, rais baada ya kutumikia watu... Anatumikia wenye noti. Never again…

  Nimalizie tu kwa kutoa wito kwamba tuwaache watu wetu na yeyote mwenye nia ya kutangaza atangaze hata kesho. Tutawahukumu kwa matendo yao na si kwa kauli zao. Yeyote anayetanguliza maslahi ya chama mbele, anaye poteza muda wake mwingi katika kukijenga chama usiku na mchana, anatufaa kutuongoza katika kinyanganyiro cha kuisaka IKULU.

  Ikulu ni yetu hapo 2015. Peeeeooooppppplllllleeeeee's Pooooowwwwweeeeeeeer!!!!

  Joshua Bukuru
  Belgium.
   

  Attached Files:

 2. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi cha miaka 10 mfululizo nimekuwa nikiwafuatilia kwa karibu sana hawa wanasiasa wawili. Kwa kipindi chote hicho Mbowe hajawahi kumfunika kijana kwa mambo yafuatayo:

  1. Uwezo wa kujenga hoja zenye akili
  2. Uwezo wa kufafanua mambo ya kisiasa ya nchi bila kutumia matusi
  3. Haiba ya kisiasa na uwezo mkubwa wa kufikisha ujumbe kwa wananchi
  4. Anaweza kuvuta umma peke yake bila kubebwa na Dr. Slaa

  Zitto has bright future compared to Mzee Mbowe.
   
 3. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  naunga mkono hoja yako mkuu.
   
 4. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Unataka kumaanisha nini...hueleweki
   
 5. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Eventually, you will get married. Ooh?
   
 6. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kuanza kuchangia naunga mkono uzi kwa 100%
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  CCM mnahangaika kama mtu anayekufa maji..hamna pa kushikia isipokuwa Mbowe na Zitto ili mradi mnashindwa kuzungumzia yenu chumbani. Hivi JK na Mwandosya sijui nani mwenye bright future?.
   
 8. Root

  Root JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,199
  Likes Received: 12,912
  Trophy Points: 280
  Jamani mwaka 2005 mbowe akifanya kila jitihada,Mbowe anaubusara kumbuka kupitia speech zake alipokuwa UK,speech zake baada ya Lema kuvuliwa Ubunge,fuatilia speech zake bungeni.
  Nakubali zitto ni mzuri ila kila mmoja ana uzuri wake hapo ila busara ziko kwa Mbowe.
  Tusiharibu kwa kuwafananisha

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 9. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ofcourse zito anamzidi mbowe kukusanya wanamziki na kutoa single
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nani kakubishia na kama ni bora hakuna shida sie wanachadema tunadhani Mbowe bado anafaa kuwa kiongozi wetu.
  Zitto pia tunamheshimu kwa uongozi wake uliotukuka sawa na viongozi wengine wengi tu wa Chadema. Asante kwamba na wewe umeandika kitu JF
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  .............................????????????????????????????

  Wajenzi wazuri wa HOJA tu ni watu wa muhimu kweli kweli ila kwa Tanzania hii ambayo jua linamwakia karibia kila mtu mfukoni, wenye kuhitajika safari hii ni WAJENZI WAZURI WA UCHUMI na wale wenye kuchukia UFISADI KAMA PAULO KAGAME WA RWANDA, na mwenye kutokuhusishwa na shombo zozote za UBAGUZI wa aina yoyote ile period.

  Kuchagua tu mtu kwa ufundi tu wa kupanga maneno matupu yasiomsaidia mwananchi kuongeza ukubwa wa ugali mezani kwake hayo ni mawazo ya miaka ya 47 ambayo ki-ajali tu kijana mwenzetu mdogo kama wewe hapo bado umeyageuza kuwa misaafu stahiki kwako. Kama ninakosea kalete hoja bora zaidi.

  Huku tuendako uchaguzi utakua ukishindanishwa kwa misingi ya MIKAKATI YENYE KUTEKELEZEKA na wala si tu kuchagua tu mtu eti huyu hapa ni Kitila Mkumbo ambaye ni rafiki yangu wa miaka nenda rudi, mcha Mungu na yule aliyejaliwa kutema maneno matamu kama asali tena kwa kasi ya cherehani; bure kabisa na wala hamna kitu hapo!!!

  Usiniambie mtu tumchague kwa uchanga au ukuu wa umri wake; kalete programu yake tukaipime hapa ...
   
 12. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  ni mtazamo wako kwa akili yako ilipofikia, ni sawa na mimi ninavyoamini kitimoto ni bora kuliko kuku, si lazima na wewe huamini!
   
 13. b

  blueray JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo? hayo si ni mawazo yako, ngojea uchaguzi ukifika umpigie kura. sasa hivi wana CDM wana kazi ni kujenga chama, we unakalia kuongelea watu, au umetumwa?
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,743
  Trophy Points: 280
  Jk na lusinde nani zaidi?

  Hahahahahahha
  sisimweli bwana, yani hawana pakushika wanajichanganya kila leo, na hamtoweza kuwa gombanisha wana cdm!

  Ni bora kupuuza uzi kama huu wenye nia ya kuwachonganisha wana cdm!
   
 15. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  naanza kwa kuunga hoja mkuu maharage ni matamu kuliko kunde
   
 16. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Kila mtu ana nafasi yake na uwezo wake. Sidhani kama mleta huu uzi alimaanisha kutafuta mshindi. Anyways, hawa wote ni viongozi wetu, kwa hiyo tuwapendeni wote, utakapofika wakati wa kuwachagua kuwapa madaraka fulani fulani, tutaamua nani akae wapi. Ikumbukwe sisi wapiga kura ndo tuna nguvu ya kuamua nani akae wapi kupitia taratibu na chaguzi zetu ndani ya chama.
   
 17. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja nia kwa mia , watakusambulia sana, watakudharau sana ila siku ukweli ukijulikana watakuheshimu sana. Namuungamkono zitto he can read, research and write. Kuna watu humu JF hata kusoma kitabu chenye kurasa kumi hawajawahi, hawajawahi kufanya tafiti na kuandika analysis kazi yao ni siasa za umbea na magazeti, nasema sio aina ya siasa za kuisadia tanzania leo. pamoja na umasikini wa tanzania na kuungwa mkono kwa chadema , lazima tuwaeleze watanzania njia mbadala za kuleta maendeleo yao kama zitto anavyofanya sio kina heche unaweza kufikiri ni tape iliyorekodiwa anaongea ufisadi, mara polisi kila siku lakini hasemi tunatatatua vipi matatizo ya watanzania.
   
 18. S

  SIR JAPHET Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KIVULI CHA PHd SLAA KINAWATESA,KILA SIKU ZITTO,ZITTO?
   
 19. G

  G. Activist JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Waliozaliwa kabla ya Uhuru hawawezi kulikomboa Taifa hili kiuchumi!! mwisho wa kunukuu!!!

  Mbowe anabusara sana, kuliko huyo mpayukaji!!
   
 20. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Yaani maara hii Mbowe amekuwa Mzee? Ndio maana wenye busara wanasema kutangaza nia ya kugombea Urais sasa ni kutengeneza makundi ndani ya Chama. Leo Habib Mchange kaandika makala ndefu sana kwenye gazeti la Raia Mwema akimnadi na kumtetea Zitto, Kitila Mkumbo naye katoa msimamo wake (sijui kama amemtetea pia au la) na baadae Mchange kamnukuu Kitila Mkumbo na kuweka kwenye ukurasa wake wa facebook. Haikuishia hapo ZZK naye kaandika kuwajibu kwa pamoja Mayage S. Mayage, Mbwambo na Chahali akilalamika kwamba makala tatu za toleo lililopita zilimlenga yeye. Bahati mbaya leo makala tatu pia kwenye gazeti hilo hilo leo zimmtetea yeye....Makundi!!!! Zitto kama binadamu na kama Mwanasiasa aneweza kuwa na nia dhabiti ya kusukuma mbele gurudumu la mabadiliko lakini hofu yangu ni wafuasi wake. Wapo wanaodhani Zitto lazima awe Rais kupitia Chadema jua liwake mvua inyeshe. Hawa ni hatari kuliko ukoma na watanzania hatutawasamehe wakisababisha CCM ishinde mwaka 2015
   
Loading...